Nauliza huyu Mwanamama anayeitwa Mange Kimambi ameshindwa kabisa kudhibitiwa kwa Tabia zake za Kutukana, Kudhalilisha, Kuumiza na hata Kuharibu Maisha ya Watu??
Tangu aanze haya Mambo ya Kutukana Watu ni Zamani sana kuanzia kwenye Blog yake, akaenda Instagram akaitukana sana Serikali iliyokuwepo Madarakani na sasa kahamia kwenye App akiendeleza yale yale,
Huko kwenye App nasikia ameweka Kipengele maalum kabisa cha kuweka Videos za Kudhalilisha Watu, Serikali ya awamu ya Sita imefungia sites zote za Porn ajabu kwenye App ya Mange kuna Videos za aina hizo.
Watu Wamelia, Wameharibu Heshima, Wameharibu Kazi, Wamekosa Kutokujiamini tena mbele ya Jamii, Wamepata Misongo ya Mawazo, Wengine hadi Jela wameenda,
Je Serikali imemshindwa? Au inaona ni sawa anayoyafanya? Hakuna Wanasheria wa kuliweka hili suala lake kisheria??
Binafsi nasikitishwa sana nionapo Mtu anadhalilishwa kwa faragha zake, inafika muda hata Mke na Mume ndani tutaanza kutokuaminiana, Mtu aweza akavujisha videos kwa Mange ili apatiwe Pesa,
Mange ni sikio la Kufa hata akisemwa vipi ni kama ameshakubali liwalo na liwe as long as Pesa inaingia ndio maana nauliza hakuna jinsi ya kumshtaki kisheria hiyo tabia yake ikomeshwe?