MANGE FUNDIKA HAPA, ACHA UMBUMBUMBU.
CAG RIPOTI, MWENDOKASI, TOTO AFYA KADI NA AJIRA.
Na, Suphian Juma Nkuwi
Mange Kimambi baada ya kuonesha mdhaifu na mwoga kwa kukimbia mjadala nami kwa kuni-block baada ya kukosa ushahidi wa shutuma zako dhidi ya Rais wetu na mwanae Abdul, leo naona umekuja na hoja ucharwa kwamba Rais wetu kipenzi cha Watanzania Dkt ameshindwa kuongoza nchi ukirejea hoja za Mwendo kasi, ripoti ya CAG, NHIF, Toto afya kadi na Ajira.
Wewe ni mbumbumbu hujui kitu na anapotoshwa na wajinga wachache wa hapa nchini, sasa ngoja nikuelimishe maana upo nje ya nchi, mageuzi yanayofanywa na Rais Dkt Samia huyajui unasubiri hadi uhadithiwe.
RIPOTI YA CAG.
Kuhusu Ripoti ya CAG mwaka 2022/2023 Taasisi za Serikali 475 zilizokaguliwa kati yake 471 zilipata Hati zinazoridhisha.. Kuonyesha kwamba utendaji kazi wa Taasisi nyingi za umma umebadilika.
Soma ripoti ya CAG ukurasa wa 5.
Hadi Kufikia Juni 2023 Mapendekezo yaliyotolewa na CAG yafanyiwe kazi na Serikali yalikua ni 7,342. CAG anakiri Mapendekezo 2,946 yametekelezwa kikamilifu, Mapendekezo yake 2725 yanaendelea kutekelezwa na mapendekezo mengine yalikua yamepitwa na wakati kutekelezwa.
Soma ripoti ya CAG ukurasa wa 11. Hoja ya kwamba Ripoti ya CAG haifanyiwi kazi na mapendekezo yake ni UONGO Mkubwa!!!
MWENDOKASI
Kuhusu Hoja ya Mradi wa Mwendokasi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu ilitoa Miezi 7 kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Kuhakikisha inapatikana Kampuni Binafsi itakayotoa huduma hii ya Usafiri kwa umma.
Tayari Kampuni 30 zimejitokeza kuwania Zabuni ya uendeshaji wa mradi huu na mchakato wa Zabuni unaendelea.
Wakati Huo Huo Mradi wa Mwendokasi uliojengwa kwa awamu moja ya Kwanza, sasa hivi Awamu ya Sita Mradi wa Mwendokasi unaendelea kupanuliwa na sasa utekelezaji wa Ujenzi unaendelea hadi awamu ya Sita ya Mradi wa DART lengo la mradi huu ni maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam kufikiwa na Mabasi Yaendayo Haraka!
TOTO AFYA KADI
Toto afya kadi ambayo ilikua inahudumia watoto Laki 2 wakati kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi Tanzania ina watoto zaidi ya Milioni 20 haijafutwa
NHIF ilifanya maboresho ya utaratibu wa usajili na huduma za watoto waliokuwa wanasajiliwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya ya TOTO AFYA KADI Ambapo watoto wanasajiliwa kama wategemezi kupitia vifurushi vya Bima ya Afya au kupitia Shule wanazosoma. Kwa mujibu wa taarifa za NHIF watoto wote waliokuwa wanasajiliwa kifurushi hiki tayari wamesajiliwa vifurushi vingine vya Bima.
Hakuna Mtoto aliyekuwa anapata huduma kupitia Toto Afya kadi anateseka wala kukosa Matibabu tena!!
AJIRA
Watumishi zaidi ya Elfu 375,319 wamepandishwa vyeo kwa gharama ya Shilingi bilioni 85.89.
Watumishi zaidi ya Elfu 142,793 wamelipwa malimbikizo ya Mishahara jumla ya Shilingi bilioni 240.7 zimetumika, watumishi 81,561 watapandishwa vyeo kabla ya Mwaka huu wa Fedha kukamilika jumla ya Shilingi bilioni 90.85 zitatumika. Ndani ya Kipindi kifupi cha Rais Samia Watumishi wa umma wapya Elfu 81,137 wameajiriwa katika Taasisi mbalimbali za umma.
Kubwa Zaidi Rais Samia ametenga Bilioni 230.03 kuajiri watumishi wengine Elfu 47,374 hii haijapata kutokea!!!
Nimalizie kwa kukumbusha na kukuhakikishia kwamba awamu hii umefeli na utafeli big time unahangaika bure kumtukana Mhe. Rais Dkt Samia na familia yake, tupo nae Ikulu hadi 2030 na nakuhakikishia;
1) App yako ya kudhalilisha watu hutarudishiwa
2) Punde utarejeshwa nchini Tanzania kujibu mashtaka zaidi ya manne yanayokukukabili.
Suphian Juma Nkuwi,
Singida,
Juni 6, 2024
View attachment 3009547