Mange Kimambi ameshindikana kudhibitiwa kabisa?

Mange Kimambi ameshindikana kudhibitiwa kabisa?

Nauliza huyu Mwanamama anayeitwa Mange Kimambi ameshindwa kabisa kudhibitiwa kwa Tabia zake za Kutukana, Kudhalilisha, Kuumiza na hata Kuharibu Maisha ya Watu??

Tangu aanze haya Mambo ya Kutukana Watu ni Zamani sana kuanzia kwenye Blog yake, akaenda Instagram akaitukana sana Serikali iliyokuwepo Madarakani na sasa kahamia kwenye App akiendeleza yale yale,

Huko kwenye App nasikia ameweka Kipengele maalum kabisa cha kuweka Videos za Kudhalilisha Watu, Serikali ya awamu ya Sita imefungia sites zote za Porn ajabu kwenye App ya Mange kuna Videos za aina hizo.

Watu Wamelia, Wameharibu Heshima, Wameharibu Kazi, Wamekosa Kutokujiamini tena mbele ya Jamii, Wamepata Misongo ya Mawazo, Wengine hadi Jela wameenda,

Je Serikali imemshindwa? Au inaona ni sawa anayoyafanya? Hakuna Wanasheria wa kuliweka hili suala lake kisheria??

Binafsi nasikitishwa sana nionapo Mtu anadhalilishwa kwa faragha zake, inafika muda hata Mke na Mume ndani tutaanza kutokuaminiana, Mtu aweza akavujisha videos kwa Mange ili apatiwe Pesa,

Mange ni sikio la Kufa hata akisemwa vipi ni kama ameshakubali liwalo na liwe as long as Pesa inaingia ndio maana nauliza hakuna jinsi ya kumshtaki kisheria hiyo tabia yake ikomeshwe?

UPDATE: Naishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kusikia Vilio vya wengi juu ya yule Dhalimu mwenye Matatizo ya Akili pamoja na genge lake kwa kufungia Malipo ya App yake, tunaomba iwe Permanent ili Tabia hizo chafu zikomeshwe na isiishie hapo tu, kwa Umoja wetu tufanye maandamano huko Insta ili akaunt yake ipigwe Life Ban.
Adhibitiwe kwa kosa gani? Ili iweje? Acheni maovu akose kazi!! Mkiendelea na ushenzi na yeye ata wafichua tu mashimoni.
 
Sijawahi kuona Kosa la Mange....!
Kama wenye Video chafu mlishindwa kutunza Video zenu chafu, yeye kuziachia kosa lake ni lipi...!

Mimi naona toka aanze kufanya hivyo inasaidia wengine kucheza kwa step.
Kabisa ss hivi watu wanajiheshimu wanajua wakizingua watajikuta appuni dadeq 🤣🤣🤣
 
Faragha ni mambo ya mtu binafusi. Ambayo mtu hufanya yeye mwenyewe kwa siri au na watu anao wa amini kuto ya towa hadharani. Kwa mfano mtu na mke wake wanavyo fanya chumbani ni siri Yao wawili.
Upo sahihi kabisa kwa tafsiri ya faragha haya nenda kule juu kasome upya comment yako kisha jipige makonzi ya kichwa huku ukisema "mimi ni punguani wa mwisho" rudia zoezi hilo mara nyingi uwezavyo.
 
Aisee yule manzi kwa sasa nimekubali ni master mind hii app anatengeneza mpunga wa maana amelala geto sema ndo hivyo anaumiza wengi sana... Anyway hata serikali inatupiga mahelaa sisi tunaliaaa tuu
Sema wangeiruhusu wachukue kodi tu.hao wanaojirekodi watajua wenyewe na mabalaa yao.
 
Hapa tunaweza kusema suluhisho ni kukusanya simu zenu pamoja mahala pa wazi,kabla ya show show,ila kumbe jitu lina simu mbili,moja lishaitega kona flani lilipowahi kuchukua chumba.(hii dunia ina wahuni sana hii asee)
 
Hapa tunaweza kusema suluhisho ni kukusanya simu zenu pamoja mahala pa wazi,kabla ya show show,ila kumbe jitu lina simu mbili,moja lishaitega kona flani lilipowahi kuchukua chumba.(hii dunia ina wahuni sana hii asee)
Hata huko mahotelin mchunguze nasikia wanaficha camera kwenye taa, picha za ukutani hadi kwenye maua, mkijichanganya tu mnajikuta kwenye app
 
Ukweli ni kuwa anayosemaga mange kimambi asilimia 95% huwa ni ya kweli kabisa

Mfano mambo mengi nayoyajua nadhani ni mimi tu najua hiyo siri mange huyasema najikuta nashangaa kujiuliza amejuaje

Mange huwa ni mkweli kabisa labda changamoto huwa ni jinsi anavyowasilisha

Kinachomponza mange ni kuwa mkweli, mange ni msema kweli kabisa wala huwa hamsingizii mtu
 
Mambo yao acha tuwaachie wao wenyewe.

Kila mtu atakula alikopeleka mboga
 
kimsboy nakuita mara 3......hapa siyo marekani ujue
Haya mambo magumu, wakati mwingine huwa tunapita kimya kana kwamba hatujaona kitu.

Bora tuendeleze mtanange wa Simba na Yanga, ila haya mambo yao tuwaachie wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom