Heaven on Earth
JF-Expert Member
- Mar 21, 2013
- 37,226
- 26,687
Tena kipindi kile alikua anatukana watu waliotag tu IG!
Anatukana watoto, mmeo, wakwe hadi vimbwa!
Ila yeye hataki aguswe kabisaa, wala hataki mashambulizi.Alitoa mawasiliano hadi ya wanaume wa watu kwenye blog akisema eti watu wajichukulie mwanaume huyo.
Leo hii mie nimwone jasiri? Eti sijui wa pekee sijui wa kuigwa kweli?Eti yupo real!
Kuwa real ni kukosa staha na maisha ya watu walowahi kuwa sehemu ya maisha yako? Kuwa real ni kuwachafua watu walokuumiza ili kila mtu awaone wana roho mbaya, wanafiki na hawafai hata kwa kurumagia kisa wewe ulishindwana nao?
Anatumia iyo kama shield ila deep unside naona yeye kutoka katika lile group inamuuma kiyama na inamkosesha raha na hataki urafiki wa wenzie uendelee eti wapo fake?
Whats being fake labda sijui mie..
Mwanamke jasiri kwangu ni yule anaefikisha ujumbe wake bila kuwa biased wala kuangalia upepo unaendaje, angeandaa makala ya changamoto za kirafiki na costs zake ningekua na la kumpongeza,
Mwanamke jasiri ni yule anaejali hisia za wengine, hususani walowahi kuwa sehemu ya maisha yake.
Mwanamke jasiri anajua kuachilia vinyongo na kutunza siri za wengine.
Mwanamke jasiri anajua kujizuia na kuheshimu maisha ya wengine.
Ana ujasiri gani zaidi ya kutaka kuwafurahisha anony.
Hao x friends zake pia wana maadui wao ambao wanabenefit kwa kupitia songombingo hili kuweza kujipa credit.
Kama mtu ulishamalizana naye urafiki kuna haja ya kufurahia mabaya yake kuwa ameachwa au kumpaka kuwa ana roho mbaya sana na kumwombea mabaya?
Nimemaliza.
Umeona ujumbe wako u turn??? Lol