MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,019
Kuna hii barabara ambayo inatokea Pasiansi sokoni kupitia Taqwa Sekodari Lumala kwenda Kiseke yenye urefu usiozidi km 1.5 lakini muhimu sana kwa matumizi maana ni eneo lenye wakazi wengi.
Barabara imeharibika sana na ina msongamano mkubwa wa magari hasa mabasi ya wanafunzi ambayo yanawahisha wanafunzi mashuleni.
Zaidi ya mara tatu nimepishana na mabasi ya watoto wa shule yakipita maeneo hatarishi kuanguka na kuweza kuleta madhara makubwa na vilio na hakuna anatejali.
Nasikia barabara hiyo iliwahi kutengewa fedha enzi za mwenda zake iwe lami ili kuongeza diversity katika jiji unapotokea msongamano katika barabara kuu ya Airport lakini zikapigwa na wajanja wakaishia kuweka mitaro tuu.
Hivi sasa magari yetu ili tusiyaue tunazungukia mbali zaidi hadi Sabasaba lakini jee hayo ya watoto wa shule watapita wapi zaidi ya kujaribu humohumo kwenye hatari?
Baraza la madiwani limelala, Mkurugenzi na maafisa wake nao hawataki matengenezo makubwa ya hiyo barabara maana baada ya hapo hakuta kuwa na hela za ulaji wa vifusi na repair.
Jamani mnataka VIFO vya watoto vitokee mkiwa humo maofisini kisha muwe mstari wa mbele kutoa rambirambi?
Kwa kuwa hili limewekwa wazi na fedha zinapotolewa mnakula basi mtalaaniwa