Manispaa ya Shinyanga ihamishie stand kuu ya mabasi jirani na viwanja vilivyopimwa Nhelegani Mashariki ili kupanua mji

TPKitula

Senior Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
125
Reaction score
80
Ninashauri viongozi wanaohusika na masuala ya usafirishaji mkoani Shinyanga akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa, wakae chini na kujadili namna bora ya kuitoa stand ya mabasi "manyoni" pale Ibinzamata waihamishie Nhelegani mashariki jirani na viwanja vilivyopimwa ili kurahisisha ukuaji wa mji pamoja na kupunguza msongamano wa mabasi kwenye njia za kuingilia na kutokea stand mahali ilipo sasa.

Pia hii itasaidia kuukuza mji wa Shinyanga kwa kasi zaidi maana wawekezaji mbalimbali watajitokea sehemu zenye nafasi pale Nhelegani ili kuwekeza huduma mbalimbali kwa ajili ya wasafiri na wenyeji. Vilevile itaongeza mapato ya halmashauri na serikali kuu kwa namna moja au nyingine kutokana na mji kukua kwa haraka zaidi tofauti na ilivyo sasa.

Ni matumaini yangu uzi huu utafanyiwa kazi maana ninaamini wanapita humu na kusoma maandiko.

Mungu awabariki!
 
Na kwa nini mji uke? Ukue ili nini? Kwa nininwasiboreshe kwanza huo uliopo ili uwe na kila kitu badala ya kujenga maeneo mengine?
 
Mnataka kuwatesa Wananchi bila sababu. Manyoni penyewe ni mbali na mji halafu upeleke Nhelegani karibu na Jambo huko zaidi ya km 10 toka mjini?
 
Mtoa mada hapo panatosha ilipo stand kwa sasa,mazingira ni rafiki kabisa ,stand ipo nje kabisa na mjini na msongamano hakuna pale.

stand ni pana na inatosha,mtoa mada kama una sababu zingine useme ,ila suala la kupeleka stand nelegani unataka watu waliwe na fisi wakiwahi usafiri?
Hilo haliwezekani ,hakuna changamoto zozote za kiutendaji katika maeneo ilipo stand kwa sasa.

Mtoa mada tafuta kivuli ukae kwanza, jua ni kali
 
Na kwa nini mji uke? Ukue ili nini? Kwa nininwasiboreshe kwanza huo uliopo ili uwe na kila kitu badala ya kujenga maeneo mengine?
Ndugu. Kujenga maeneo mengineyo ndio ukuaji wa mji wenyewe. Karibu sana!
 
Back
Top Bottom