Manji kuzikwa Marekani kumedhihirisha kiwango kikubwa cha ujinga. Tuna safari ndefu kama nchi katika katiba na elimu ya uraia

RAis wa iran juzijuzi kafa jumapili kazikwa jumatano nadhani unakumbuka ile ajali ya helicopter
 
Kwani kuwa na nasaba, mapenzi au mahaba na nchi nyingine kunaondoa vipi uraia wa mtu?? Yani Utanzania wa mtu unaondoka kivipi kwa yeye kuwa na mapenzi na Israel, Russia, Kenya au Marekani??
Uzalendo ndio neno nililokusudia,kuwa tayari kuifia nchi
 
Sasa mtanielewa ninaposema mara kwa mara kuwa adui mkubwa ya Watanzania ni ujinga. Watanzania bado ni wajinga sana tena sana..

Shule zetu ni za kusomesha ujinga.
 
Manji hawezi kuwa mtanzania hapa ni sehemu tu yakuchumia hela, kikinuka huwa wananchi zao za kupumzikia na kula utajiri waliouchuna polepole.
 
Huo ni ushamba , mwanakwetu wacha wafu wazike wafu wenzao ndio hii.
Sasa wewe unataka makaburi massfi ili ufanyie nini ?
Unadhani hiyo minyama inaweza kuja fufuliwa katika VVIP,VIP na Ordinary classes ??
I thank God to hold most of religion s in TZ does not support ibada za sanamu,
Hivi wewe unadhani kwamba daaa ngoja nitulie
 
Sasa kama mtu amefikia kumiliki smartphone na hajui hata vigezo vya uraia wa nchi yake hao wengine watakuwa anafahamu nini katika masuala ya haki za uraia na mambo mazito ya katiba kwa ujumla?!
Tunaitumia kwa Ku socialize,kupiga picha tukiwa bichi ama siku tukila samaki ama Kuku na kuposti mtandaoni. Kubetia na kubishana siasa za Cccm and cdm.
Pia tunafuatilia udaku wa kimambi.
Mtu hajui anaweza jaza ama beba vitabu vya kujaza semi trailer mia akawa anajisomea.
 
Mfumo wa elimu na kuficha sheria zisipatikane au kuandikwa kwa kiingereza ndiyo chanzo cha ujinga wa watanzania.
 
Na CCM ndio wanapenda watu waendelee kuwa hivyo hivyo maana elimu wanayotoa ni ya zama za mawe.

Ukitaka kuamini hilo waulize watu kuhusu elimu ya uraia na katiba ya nchi watakuambia mimi sitaki kusikia kuhusu siasa waachie wanasiasa.

Masikini na wajinga wanadanganywa uraia pacha ni kukosa uzalendo huku viongozi wa CCM wengi tu wana pasi mbili.

Nitakupa tu mfano mwepesi fuatilia mazungumzo ya ex- CDF baada ya Magufuli kufariki na eti wakawa hawajui wafanye nini baada ya rais kufia madarakani huoni hapo kuna tatizo?
 
Mbona Daudi Bilal alizikwa huko au watanzania wanahisi naye hakuwa Mtanzania.
Elimu ya kawaida na mawazo ya Watanzania ni ya ajabu sana na utayaelewa kupitia comment zao mtandaoni.
 
Asante sana kwa Madini adimu👊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…