Manji kuzikwa Marekani kumedhihirisha kiwango kikubwa cha ujinga. Tuna safari ndefu kama nchi katika katiba na elimu ya uraia

Manji kuzikwa Marekani kumedhihirisha kiwango kikubwa cha ujinga. Tuna safari ndefu kama nchi katika katiba na elimu ya uraia

Ungetoa elimu kidogo kuhusu mazishi ya Yusuph Manji huko USA ili wengi wajifunze.
Suala la maziko halina kuelimishwa kwani maziko yanahitaji utashi, uwezo na ulazima( marehemu alitaka azikwe wapi na aliacha pesa ya kutimiza takwa lake). Mfano, wewe ni mchaga uko Dar familia haina uwezo kifedha na eneo huko Kilimanjaro ni wazi utazikwa Manzese. Utashi ni pale familia inapoona huko kijijini kwenu hawakufahamu kwani ulikua hauendi itaamua kukuzika hapo unapoishi ili isiingie hasara, kabla ya kufariki ulisema ukifariki ukazikwe Paris ambako si kwenu na hakuna anayewajua pia haukuacha pesa na matakwa ya sheria za uhamiaji ya kutimiza hilo, utazikwa ulipofia.
 
Mkuu mtu ukimaliza darasa la saba unatakiwa uwe umefahamu kwa kiwango kikubwa uraia wa Tanzania unapatikanaje, pia unatakiwa ufahamu kuzikiwa nchi fulani hakukufanyi au hakuna uhusiano wowote na uraia.
Uhusiano wa kuzikwa inchi husika na uraia wa marehemu upo sana tu.
Ndy maana balozi zinahusishwa..
Huwezi kuzika raia wa inchi husika bila balozi kujulishwa,

Je Manji alipofariki kuna taarifa zilipekwa ubalozi wa Tanzania kujulishwa kuhusu kifo chake?

Kama haukuhusishwa basi Manji hakuwa Mtanzania,,

Tusipepese macho.
 
Uhusiano wa kuzikwa inchi husika na uraia wa marehemu upo sana tu.
Ndy maana balozi zinahusishwa..
Huwezi kuzika raia wa inchi husika bila balozi kujulishwa,

Je Manji alipofariki kuna taarifa zilipekwa ubalozi wa Tanzania kujulishwa kuhusu kifo chake?

Kama haukuhusishwa basi Manji hakuwa Mtanzania,,

Tusipepese macho.
Kwanza sio kweli kwamba huwezi kuzika raia wa nchi nyingine bila balozi wake kujulishwa, mtu wa nchi nyingine anaweza kuzikwa vizuri tu bila ubalozi wake kupata hata taarifa mradi kifo chake sio cha utata na post-mortem report ipo. Pia hakuna nchi yenye ubalozi au mahusiano ya kibalozi na nchi zote duniani.

Pili kama ubalozi umepata taarifa wewe utajuaje?? Balozi huwa zina taratibu za kutoa taarifa za vifo wa raia wanaofia kwenye nchi nyingine ikiwa aliyefariki anao ndugu, jamaa au rafiki katika hiyo nchi?

Tatu, hata kama ingekuwa ni utaratibu wa kimataifa kwamba kila raia wa nchi nyingine anayefia nchi tofauti na yake lazima ubalozi wake upewe taarifa hizo baasi hao wanaosema Manji sio raia wathibitishe kwamba wamepata taarifa kwamba ubalozi wa Tanzania huko Marekani haukupewa taarifa za kifo chake.
 
Nimeangalia comments za ukurasa mmojawapo wa mitando ya kijamii kuhusu Manji kuzikwa Florida Marekani nimeshangaa kuona kundi kubwa sana la raia Watanzania hawana elimu kabisa kuhusu vigezo vya kuwa raia wa nchi hii au kuna ubaguzi mkubwa sana kwa raia walio wengi.

Wengi katika ukurasa huo wameshangazwa sana na kuuliza maswali kwamba kumbe Manji hakuwa Mtanzania?! Yani tuna raia wengi wanaojua kwamba Mtanzania hawezi kuzikwa nje ya Tanzania akifariki! Kwamba kigezo kimojawapo cha kuthibitisha Utanzania wako ni kuzikiwa katika ardhi ya Tanzania!

Sasa kama mtu amefikia kumiliki smartphone na hajui hata vigezo vya uraia wa nchi yake hao wengine watakuwa anafahamu nini katika masuala ya haki za uraia na mambo mazito ya katiba kwa ujumla?!

Itoshe kusema tuna safari ndefu kama nchi kuhusu katiba na elimu ya uraia.
Kwa kutoa shuhuda zaidi waziri wa fedha wakati wa Mwalimu Habib Jamal alifia na kuzikwa Canada na hapakuwa na kelele zozote.
 
Ishu ya wapi mtu azikwe ni ishu binafsi na ya kifamilia. Kila mtu anaweza kuzikwa marekani akiwa na hela. Wenzetu kuzikwa ni pesa unanunua eneo la kuzikia.
 
Wana hoja wahindi wengi sio wazalendo,wako huku kuchuma tu ila wana passport au nasaba ,mapenzi na nchi zingine,wahindi sio watu wa kuwaamini
Mkuu hata waziri wa zamani wa fedha Habib Jamal alihamia Canada na akazikwa huko,yawezekana alikuwa na urai wa Canada pia.
Lakini sio wahindi tu,ni jambo pana sana.
Wengi wao wana uraia zaidi ya mmoja,.Ufike wakati uraia pacha uruhusiwe bila kificho,tuache kudanhanyana.
 
Huku mnajisifia jinsi mnavyowapiga matajiri na kuwaletea kiburi ndio maana hata wakifa na wao wanagoma kurudi kwenye ardhi ya laana inayokashifu mpaka mitume ya mwenyezi mungu na kusifia viongozi.......yaani ukiwa kiongozi kwenye hii inchi ya tope unajiona una nafasi ya kipekee sana.......huwezi kuishi na walio kuchagua maana wewe tena ni special.......mfn.....kwenda na kiti kanisani.......mpaka huko marekani,Russia,UK, Rwanda na kwengineko watu wanakaria benchi ila hapa tu ndio (swahaba anakuja na siti yake kumuomba mwenyezi mungu)
 
Kunaweza kuwa na ukweli katika hilo.Lakini,nimeona wengi wanaozikwa huko(nchi walizofarikia) huwa ni wa dini ya kiislamu.Nikaelezwa sababu mojawapo ni kwamba,kwa taratibu za dini ya kiislamu,mtu akifariki anatakiwa kuzikwa siku hiyohiyo(kuna muda mchache wa kukaa na maiti)bila kujali nchi yake ya kuzaliwa.Na ninaamini yawezekana kukawa na sababu zingine.
tutolee mfano sasa kama mtu ni mtanzania na kaenda kujitAfuta na kule hana ndugu yupo peke yake na amefriki? Vipi itabidi wamzike tu majirani hivyo hivyo mku hata bila uwepo ww ndugu zake kabisa?
 
Wakuwaamini ni misukule ya CCM hata afie wapi tutachangishana azikwe kizimkaxi
Zanziba kama huelewi Azam anapakia maiti na mpaka watu 10 wanaokwenda kumzika bure, huna haja ya kuchangisha.

Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Manji saa hizi zamani kishazikwa. Waislam hatufanyi maiti zetu kuwa mradi wa watu kuchangishana.

Hayo ni kwenu tu huko.
 
Zanziba kama huelewi Azam anapakia maiti na mpaka watu 10 wanaokwenda kumzika bure, huna haja ya kuchangisha.

Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Manji saa hizi zamani kishazikwa. Waislam hatufanyi maiti zetu kuwa mradi wa watu kuchangishana.

Hayo ni kwenu tu huko.
Kafie congo uone kama kuna boti na bure kukuleta,utazijwa tu kule fasta fasta,nakukumbusha rais wa iran alikaa kwenye jokofu siku nne
 
Ungetoa elimu kidogo kuhusu mazishi ya Yusuph Manji huko USA ili wengi wajifunze.
Amezikwa tu kama Mtanzania yoyote anayekufa nje ya nchi na Amekosa nauli ya kuja kuzikwa kwao mboba Afika kusini wamezikwa watania wengi tu. Ila Manji siyo kama kakosa nauli bali nikama vile mjaluo aamue kuzikwa Makaburi ya Kinondoni badala ya kwao Musoma.
 
Kafie congo uone kama kuna boti na bure kukuleta,utazijwa tu kule fasta fasta,nakukumbusha rais wa iran alikaa kwenye jokofu siku nne
Waislam tunazikwa tulipofia, uletwe kufanya nini na wewe tayari maiti.

Zanzibar wanapelekwa kwa kuwa Dar ni pua na mdomo, wa nje ya Dar hawapelekwi kokote wanazikwa hapo hapo walipofiahata kama kuna usafiri.
 
Back
Top Bottom