Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Suala la maziko halina kuelimishwa kwani maziko yanahitaji utashi, uwezo na ulazima( marehemu alitaka azikwe wapi na aliacha pesa ya kutimiza takwa lake). Mfano, wewe ni mchaga uko Dar familia haina uwezo kifedha na eneo huko Kilimanjaro ni wazi utazikwa Manzese. Utashi ni pale familia inapoona huko kijijini kwenu hawakufahamu kwani ulikua hauendi itaamua kukuzika hapo unapoishi ili isiingie hasara, kabla ya kufariki ulisema ukifariki ukazikwe Paris ambako si kwenu na hakuna anayewajua pia haukuacha pesa na matakwa ya sheria za uhamiaji ya kutimiza hilo, utazikwa ulipofia.Ungetoa elimu kidogo kuhusu mazishi ya Yusuph Manji huko USA ili wengi wajifunze.