Manunuzi ya nguo zimwi linalomaliza pesa za wanawake

Manunuzi ya nguo zimwi linalomaliza pesa za wanawake

Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari tajwa hapo juu, Kama ilivyo katika watu wanaoongoza kuwa na nguo ni wanawake.

Hii yote hutokana na kutaka kuwa na muonekano mzuri na utanashati.

Pia mavazi hayo yanafanya mwanamke kuwa mrembo zaidi kulingana na aina ya mavazi.

Kuna aina nyingi za mavazi yanayopendwa sana na wanawake.

Mojawapo ya mavazi hayo ni yale ya casual, official na wedding guest.

Leo tutazungumzia mavazi ya aina mbili ya casual ambayo ni suruali za aina mbalimbali, blouse za aina mbali mbali, vigauni.

Haya mavazi ya mitoko ya weekend yaani casual na mitoko ya hapa na pale ni moja ya mavazi yanayonunuliwa bila mpangilio wa pesa, maana mwanamke akiiona tu nguo ukute ni blouse au jeans, zimwi linaamka hata kama hakupanga kununua atanunua tu.

Nguo zingine ananunua lakini havai kabisa utakuta kabati limejaa akitaka kuvaa anavurugwa kichwa mpaka avuruge kabati.

Mavazi mengine ni pamoja na mavazi ya sherehe, ambayo ni yale magauni ambayo wanavaa kama wedding guest.

Huwa magauni hayo yanatumia gharama nyingi sana, ila hata kama pesa akupangilia ananunua wala hajali.

Mbaya zaidi magauni haya yanaendana na rangi husika ya wakati huo au rangi ya ukumbi, pia na fashion husika hivyo humlazimu kila sherehe kununua nguo.

Zimwi hili la kununua nguo limekuwa likiwatesa sana mabinti wengi na wengine wamejikuta wakidanga ili wanunue nguo zinazokwenda na wakati.

Ukija katika ndoa yani wanawake hasa wale wa uswahilini pamoja na mama wa nyumbani ambao hawana kazi wamekuwa wakibana pesa za waume zao za matumizi kama mlo kamili ambazo wanaachiwa wanabana ili wanunue nguo.

Zimwi hili halijaishia hapo linawafanya wanawake kuwa watumwa wa kwenda na wakati ambao wakati huo hauendi na wao.

Isipokuwa wakati huo umegeuka zimwi ambalo limekuwa likipoteza pesa zao.
View attachment 2320322
Kuna viatu pia, mara mchuchumio, mara mosimo, mara raba..!! etc
 
Anapagawa kwanza hajui avae ipi, anavua anavaa
Halafu kabla ya kuanza kupagawa, ANAPIGA BASI NGUO TANO..!! Na ndo zinaenda kumpagawisha vilivyo. Binafsi, kama natoka naye, nahakikisha nakaa kwenye TV mpaka atakapokuwa tayari amemaliza kupagawa. Na wakati anapagawa, OLE wako umuulize au umuhimize kuwahi..!! UTAJUTA kwanini ulimuuliza..!!
 
zaidi ya saa nzima mtu aliniweka eti anatafuta nguo ya kuvaa..

mtu kabati limejaa na kuna nguo zina zaidi ya mwaka hazijavaliwa.

Kimbembe siku nikamwambia embu chambua ambazo hazitakiwi tukazigawe alipata sijui mbili tu.😂 Kila hiyo anaiona nzuri tena, kiruuu....😀
Halafu wakialikwa kwenye sherehe utawasikia..!! YAANI SINA NGUO WALA KIATU CHA KUVAA KWENYE SHEREHE YA FULANI
 
Aiseeee......katika kitu kimenishinda ni kununua nguo hovyo hovyo
 
Umaskini kitu kibaya sana
Omba Mungu akupe pesa uondokane na vimawazo vya kimaskini kama lako na la mleta mada

Mna pepo la umaskini
Aombe Mungu au afanye kazi apate pesa..!!?? Wewe ni sawa na wale wachungaji wanawaombea wafuasi wao wapate magari na huku yeye akitaka gari anawahimiza wafuasi wake wamchangie
 
AOmbe Mungu au afanye kazi apate pea..!!?? Wewe ni sawa na wale wachungaji wanawaombea wafuasi wao wapate magari na huku yeye akitaka gari anawahimiza wafuasi wake wamchangie
Umaskini huanzia kwenye akili
Mtu akiwaza kuwa mwanamke kuwa na nguo nyingi za gharama au kwenda saluni za bei ni.kupoteza pesa huyo anahitaji maombi ana pepo la umaskini
Akili ikiamka ndipo sasa aweza kwenda kuchapa kazi apate pesa za kumpa mkewe anunue nguo za gharama na kwenda saluni za gharama
 
AOmbe Mungu au afanye kazi apate pea..!!?? Wewe ni sawa na wale wachungaji wanawaombea wafuasi wao wapate magari na huku yeye akitaka gari anawahimiza wafuasi wake wamchangie
Hayo yapo dini zote hata mapadri huwaombea waumini baraka ila wao huitisha sadaka za kununuliwa magari na kuishi maisha mazuri

Kanisa lolote nenda mchungaji na padri kuishi kwa sadaka za waumini maisha mazuri tu wao wanachowapa waumini ni baraka tu
 
Mzee wa mbususu mkeo mbususu itakua salama kweli??? Mpe pole sana😆😆
Mbusus yake mbona ipo salama kabisa....ila sii unajua tena lazima mwanaume uwe na wanawake watatu ndio mke ashike adabu
 
Back
Top Bottom