Uliyoyaandika ni madogo.
Nenda mji wa Pemba nchini Msumbiji uone wafanyabiashara Watanzania walivyo wengi, walioukimbia utawala wa mkono wa chuma.
Nilifika Pemba mara 2 na kukutana na baadhi ya Wafanyabiashara wa kitanzania, wanaongea wazi kabisa kuwa wanamshukuru Magufuli. Maana kama kungekuwa na uongozi mzuri, wasingefikiria kabisa kuondoka nchini Tanzania. Waliondoka kukimbia manyanyaso, lakini sasa wamepata mafanikio makubwa ambayo hawakuwahi kufikiria. Nchini Msumbiji kwa sasa, makampuni yote ya mabasi ya safari ndefu ndani ya nchi yanamilikiwa na Watanzania. Nenda kwenye miji kama Mueda, wamejaa wafanyabiashara wa Tanzania.
Nenda Zambia. Leo kampuni ya Meru ndiyo inayoongoza kwa vituo vingi vizuri kuliko kampuni yoyote nchini humo. Manji naambiwa (sijahakikisha kama ni kweli), mpaka amehamishia makao ya kampuni zake huko Lusaka.
Hapo Burundi tu, BAKHRESA, ameweka kiwanda kikubwa na cha kisasa ambacho huwezi kulinganisha na vilivyopo Tanzania. Halafu kajenga kikubwa zaidi kuliko vyote Afrika Kusini. Huku akipeleka biashara zake Mauritius.
Nchini Msumbiji, pale Nampula, Mo kajenga kiwanda kikubwa cha kisasa cha cemenf. Wakati nimeenda pale kilikuwa kimekamilika, na wakati huo alikuwa ameombwa akajenge kingine Maputo.
Wengine walienda kuwekeza Kenya. Kwa mara ya kwanza, wakati wa utawala wa Magufuli, Watanzania ndiyo walienda kuwekeza Kenya kuliko kipindi chochote.
Wakati wa utawala wa marehemu, mara 4, nilialikwa na Serikali za mataifa manne tofauti ya Afrika, yote yakiniomba nisaidie kuwapeleka wawekezaji wa kigeni nchini mwao. Hao ni wale waliokuwepo Tanzania, na wameamua kuonfoka chini. Mara moja, Waziri wa nchi mojawapo, neno la kwanza nilipokutana naye (sikuwa namfahamu, na sikuwahi kukutana naye kabla) aliniambia, nasikia nkchini kwenu kumeharibika, wawekezaji wa kigeni wanaondoka, sisi tunawahitaji sana hao, tuletee, mazingira yetu ni mazuri sana, na hawatajutia kuwekeza hapa.
Lakini katika mataifa yote, nchi iliyonufaika zaidi na mazingira mabaya ya uwekezaji wakati wa awamu ya 5, ni Msumbiji. Wengi walienda huko, tena wawekezaji wa mitaji ya kati. Wawekezaji wakubwa wa kimataifa, hasa kwenye sekta ya madini, wao walienda zaidi West Afrika, na wengine America ya Kusini.
Watu wanatakiwa wafahamu kuwa, hata katika ubaya, mema yanaweza kumea. Kukitokea changamoto, pambana kupata majibu sahihi kuliko kubakia ukilalamika bila ya kuchukua hatua. Baadhi ya waliondoka nchini na kwenda kuwekeza nje, wengine hata leo uwaambie warudishe biashara zao nchini, hawawezi kukubali kutokana na mafanikio wanayoyapata huko ugenini. Hii ndiyo tafsiri ya ile methali ya Kiswahili: BANIANI MBAYA, KIATU CHAKE DAWA. Maana yake ni kwamba hakuna kilicho kibaya kimakosa uzuri.