Manyara: DC mstaafu amshushia kipigo mkewe, nyumba ndogo yatajwa kuwa chanzo

Manyara: DC mstaafu amshushia kipigo mkewe, nyumba ndogo yatajwa kuwa chanzo

Pole yake mwanamke mwenzetu.Embu afanye mpango aondoke kwa huyo bwana.Mtu anaefikia kutaka kukuua tena zaidi ya mara moja anasubiri nini hapo.Philomena maisha ni matamu usisubiri ukaimbiwa parapanda sa hizi jamani.
 
Huyu mke wa DC aliyepigwa apewe ushauri aje huku jamiiforums jukwaa MU atapata tiba nzuri tu
 
Kwanini mke asiende Mahakamani kuomba talaka na mgawanyo wa machumo? Kuendelea kubaki kwenye ndoa ya aina hiyo(kama alichosema mke ni kweli) ni kutafuta makubwa zaidi.
Ndoa ya kikristo hakuna kuachana watulie hivyohivyo hadi mmoja afe humo ndani
 
Halafu utakuta mtu anafanya dhambi nyingine nyingi tu ikifika ya kuachana ili aepushe uhai wake anadai kusubiria mpaka kifo kiwatenganishe,kama unasubiria kifo kiwatenganishe tulia usiwe mkali kugombania hizo mali,kwani hapo ndipo panapotokea matatizo ya kuambulia vipigo,tumeumbwa na akili timamu,ndoa hiyo kwa hapo ilipofikia inaonekana kabisa ni mahali pa hatari kwa upande wake, lakini bado unang'angania na kulalamika...
Allah alipoweka talaka alikuwa na maana yake si kitu kizuri ila kuna hatua ikifika inakuwa hakuna namna lazma muachane kwa usalama wenu na kuna hadithi mtume anasema talaka ni halali japo Allah haipendi elewa vizuri hapo ni halali ila Allah haipendi
 
Allah alipoweka talaka alikuwa na maana yake si kitu kizuri ila kuna hatua ikifika inakuwa hakuna namna lazma muachane kwa usalama wenu na kuna hadithi mtume anasema talaka ni halali japo Allah haipendi elewa vizuri hapo ni halali ila Allah haipendi
Hata sisi wakristo mkuu,Mungu anasema anachukia kuachana,ni udhaifu wetu wa imani ndio unatufanya tutafute njia nyepesi ya kujiepusha na madhara,ndio tunafikia uamuzi wa kuachana otherwise kama ukisimama imara katika kumtumaini Mungu there is always a way out...
 
Inamaana Philomena hafahamu hata aina moja ya sumu?.
 
Dc mstaafu amshushia kipigo mkewe,amtishia kumtandika bastola.

Philomena Toima ambaye ni mke wa mkuu wa wilaya mstaafu wa wilaya mbalimbali nchini,Peter Toima amelazwa katika kituo cha afya cha Simanjiro kufuatia kipigo cha mmewe akiuguza majeraha mbalimbali mwilini mwake...
Nina uhakika Hii ishu ni pana zaidi ya hichi kilichoripotiwa.
 
Msihukumu kabla ya kusikiliza upande wa pili. Inawezekana huyo mwanamke ndiyo mwenye tatizo
 
Dc mstaafu amshushia kipigo mkewe,amtishia kumtandika bastola.

Philomena Toima ambaye ni mke wa mkuu wa wilaya mstaafu wa wilaya mbalimbali nchini,Peter Toima amelazwa katika kituo cha afya cha Simanjiro kufuatia kipigo cha mmewe akiuguza majeraha mbalimbali mwilini mwake....
We acha ulofa, hayo mambo ya kifamilia tu, unayaweka hapa kwa faida ya nani? Au we ndio umepigwa? Kwendaaaaa!
 
Back
Top Bottom