Manyara: Mama aua watoto 3 kwa kuwalisha sumu kutokana na ugomvi wa kifamilia na mume wake

Manyara: Mama aua watoto 3 kwa kuwalisha sumu kutokana na ugomvi wa kifamilia na mume wake

Hasira iliyopitiliza uamabatana na roho ya shetani

Kwa mwanaume haikai mda mrefu
kwa mwanamke uchukua mda mrefu

Tiba yake ya halaka ukiwa na hasira kali ni kulaa usingizi na usifanye maamuzi siku hiyo
 
Mama mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Regina Daniel (24) mkazi wa Louxmanda Kijiji cha Bashnet Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, anatuhumiwa kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwalisha maembe yenye sumu inayodaiwa ni ya Panya .

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Desemba 5 mwaka huu ambapo mtuhumiwa aliyapaka sumu maembe mawili kisha kuwapatia watoto hao.

Leo Jumatatu Desemba 7,2020 Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ACP Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema chanzo cha Mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati ya mama huyo na mume wake ambao umesababisha mke kuchoshwa na maisha hayo na kuamua kufanya tukio hilo kwa lengo la kumuokoa mume wake.

Kamanda amewataja watoto waliopoteza maisha ni Emmauel Agustino (7), Emiliana Agustino (4) na Elisha Agustino ambaye umri wake ni mwaka mmoja (1).

Kasabago ameeleza kuwa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya kumfanyia mahojiano.
Aisee..kiasi mpaka nafikiria watoto wangu ndivyo waivyo kama hawa,hapa sheria haihitaji uchunguzi, huyu nae ni afadhari wampoteze tu maana mnyama asiye faa hata kukaa jela kutumia gharama za wengine kwa kula chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom