Manyara: Simanjiro walia kwa uhaba wa mvua, mifugo 62,500 imekufa

Manyara: Simanjiro walia kwa uhaba wa mvua, mifugo 62,500 imekufa

Serikali ambayo inahamasisha ufisadi bila aibu tena kupitia TV ya Taifa haiwezi kuona janga lolote lile katika nchi.
 
Hali ya ukame inayoendelea Baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Manyara inatisha !HaI Sasa Simanjiro pekee ng'ombe 35,000 + wamekufa,mbuzi 10,000,kondoo 15,000 !
Hili ni janga!
Hivi Serikali imekosa mbinu za kuwaokoa wanyama Hawa!
Hebu toa pendekezo au Ushauri nini kifanyike.
 
Mkiwa mnashangilia kwenye Kampeni kwa kanga na kofia mjuwe kuna kunyolewa....
 
Kama una pesa nenda manyara kasombe ng'ombe ulete mjini upige mara tatu.

Business plan tegemea na nguvu yako kama ni Fuso au semi.

Peleka mashudu na maji nunua ng'ombe walishe mashudu wape maji.waweke kivulini siku tatu wamepata nguvu tafuta daktari wa mifugo pakia kwenye roli walete pwani kwenye Shamba lako wachunge wape mashudu na majani Ili kuongeza uzito kwa miezi mitatu.

Kisha wauzie wamiliki wa bucha pata faida nileteee commission yangu.
 
Ipeleke maji toka ziwa victoria
Mkuu; Umesema Serikali ifanyeje??? Hao ng'ombe wanaishi kwa maji tu??? Hebu nikuulize itachukua siku ngapi Serikali kupeleka maji toka ziwa victoria na ng'ombe ataweza kuchukua siku ngapi kuyasubiri hayo maji kabla hajafa ?? - Naona kama pendekezo lako sio la sasa hivi kwa Tatizo lililopo sasa hivi.
 
Maji ni mpango wa kudumu au ichimbe visima KILA kijiji kunusuru watu na mifugo
 
kabisa na wana umasikini wa kujitakia
Ni kweli Mkuu. Hawapo tayari kuuza baadhi ya mifugo na kujiwekea akiba Benk au kuanzisha mradi, kuwekeza katika shughuli nyingine ya kiuchumi. Wao na Ng'ombe wao basi.

Hawana Utofauti na Mkulima anayewaza shamba kubwa (Ekari nyingi)na mavuno mengi (magunia mengi) lakini haangalii gharama ya uzalishaji (in-put) versus mavuno (Out-put) - analima kwa mazoea. Wakulima wengi huku kwetu kwa wastani wanapata mavuno (Mahindi) gunia 4@ kg 90-100 kwa ekari moja na hawaoni ni shida!
 
hata nikitoa pendekezo halitofanyiwa kazi maana sio kipaumbele chao kwa sasa wamasai nawapa pole tu wakomae hivyo hivyo
Kweli, hata mimi nawahurumia ila nazihurumia ng'ombe zaidi kwani mmiliki wake (mfugaji) hakukumbuka kuchukua tahadhari wakati kulipokuwa na majani mengi kuyavuna bure na akajiwekea akiba kama inavyokuwa akiba ya chakula kwa binadamu.
Alisahau kwamba sio kila siku ni Ijumaa.
NB: Nimetumia neno Wafugaji kwani huku kwetu wapo Wamasai, Warangi, Wagogo, Wakaguru, Wambulu/Wairaqi na Wanguu na wote hao wanafuga na kwa sasa wote wanaathirika na Hali iliyopo. Mungu ni mwema Habagui.
 
Ni kweli Mkuu. Hawapo tayari kuuza baadhi ya mifugo na kujiwekea akiba Benk au kuanzisha mradi, kuwekeza katika shughuli nyingine ya kiuchumi. Wao na Ng'ombe wao basi. Hawana Utofauti na Mkulima anayewaza shamba kubwa (Ekari nyingi)na mavuno mengi (magunia mengi) lakini haangalii gharama ya uzalishaji (in-put) versus mavuno (Out-put) - analima kwa mazoea. Wakulima wengi huku kwetu kwa wastani wanapata mavuno (Mahindi) gunia 4@ kg 90-100 kwa ekari moja na hawaoni ni shida!
kwa gunia hizo shida ipo hapo
 
Kweli, hata mimi nawahurumia ila nazihurumia ng'ombe zaidi kwani mmiliki wake (mfugaji) hakukumbuka kuchukua tahadhari wakati kulipokuwa na majani mengi kuyavuna bure na akajiwekea akiba kama inavyokuwa akiba ya chakula kwa binadamu.
Alisahau kwamba sio kila siku ni Ijumaa.
NB: Nimetumia neno Wafugaji kwani huku kwetu wapo Wamasai, Warangi, Wagogo, Wakaguru, Wambulu/Wairaqi na Wanguu na wote hao wanafuga na kwa sasa wote wanaathirika na Hali iliyopo. Mungu ni mwema Habagui.
duh hatari sana mvua tu inyeshe la sivyo wafugaji watapata stress
Halafu hizo ng'ombe hapo ni wale wakubwa mmasai huwa haesabu ndama kama ng'ombe hata kama ana ndama elfu 10
 
Lakini mkuu ukizingatia Utunzaji wa miundo mbinu hii katika Jamii lengwa utakata tamaa. Yaani inakuwa kama hawaithamini vile....... Wao wanataka malambo ili ng'ombe waingie humo wanywe, Binadamu aingie humo aoge, afue na achote maji hayo hayo kwa matumizi ya nyumbani. Kwa hiyo usishangae kisima kirefu (Bore-hole) kikahujumiwa kwa kujazwa mawe,kokoto, miti n.k. au mabomba ya usambazaji yakakatwa kwa sime/panga au kuchomwa kwa mkuki ili maji yatiririke ngombe wanywe.
Ukijenga mbauti (Water au Cattle trough) hawataitumia. Yaani itoshe tu kusema suala la maji huku kwa kipindi cha Ukame (ambacho hutokea kila mwaka) ni vurugu tupu.
 
Back
Top Bottom