Manyara: Simanjiro walia kwa uhaba wa mvua, mifugo 62,500 imekufa

Manyara: Simanjiro walia kwa uhaba wa mvua, mifugo 62,500 imekufa

Serikali inapaswa kuchimba mabwawa kadhaa yatakayohifadhi maji ya mvua ili kusaidia mifugo isife wakati wankiangazi maana kwa wakati wa jua ng'ombe hunywa maji hata ndoo nne hadi tano kwa siku.
 
Lakini mkuu ukizingatia Utunzaji wa miundo mbinu hii katika Jamii lengwa utakata tamaa. Yaani inakuwa kama hawaithamini vile....... Wao wanataka malambo ili ng'ombe waingie humo wanywe, Binadamu aingie humo aoge, afue na achote maji hayo hayo kwa matumizi ya nyumbani. Kwa hiyo usishangae kisima kirefu (Bore-hole) kikahujumiwa kwa kujazwa mawe,kokoto, miti n.k. au mabomba ya usambazaji yakakatwa kwa sime/panga au kuchomwa kwa mkuki ili maji yatiririke ngombe wanywe.
Ukijenga mbauti (Water au Cattle trough) hawataitumia. Yaani itoshe tu kusema suala la maji huku kwa kipindi cha Ukame (ambacho hutokea kila mwaka) ni vurugu tupu.
eeh bwana eeh
 
Serikali inapaswa kuchimba mabwawa kadhaa yatakayohifadhi maji ya mvua ili kusaidia mifugo isife wakati wankiangazi maana kwa wakati wa jua ng'ombe hunywa maji hata ndoo nne hadi tano kwa siku.
na vipi kuhusu majan ambayo ndiyo chakula
 
Wenzetu wamefanikiwa sana kwa sababu wamewekeza kwenye ranch huu ufugaji wa tokea enzi hizo ushapitwa na wakat
images (6).jpg
 
Pamoja na hayo serikali badala ya kuhimiza kupanda miti sa hivi watu wanakata miti asubuhi na jioni na hakuna mwenye habari na uchomaji wa mkaa umeshamiri kwa mkoa wa manyara sijajua sehemu nyingine hali ikoje
 
Tafsiri ya utajiri utegemeana na mahali.
Kwa wafugaji utajiri ni ng'ombe wengi.
Mfugaji awazi tunavyowaza sisi
Na sio mmasai tu wafugaji wakubwa wote ng'ombe kwao ana thamani sana,kuna mzee alitaka kujinyonga kipindi cha kiangazi maana anaona mifugo inakufa tu
 
Na sio mmasai tu wafugaji wakubwa wote ng'ombe kwao ana thamani sana,kuna mzee alitaka kujinyonga kipindi cha kiangazi maana anaona mifugo inakufa tu
sasa safari hii watajinyonga wengi mvua isiponyesha
 
Pamoja na hayo serikali badala ya kuhimiza kupanda miti sa hivi watu wanakata miti asubuhi na jioni na hakuna mwenye habari na uchomaji wa mkaa umeshamiri kwa mkoa wa manyara sijajua sehemu nyingine hali ikoje
gesi ingekuwa affordable kwa angalau 90% ya watz ingesaidia sana sasa gesi yenyewe bajeti ya wiki mbili msosi
 
eeh bwana eeh
Wacha tu ndg. yangu. Ukichanganya Ujinga + Umaskini wa kujitakia + Ujeuri/Ubabe bila maarifa ukiongezea na Mabadiliko ya Tabianchi hupati picha ya nini matokeo yake. Hili lilishawahi kutokea na Serikali sikumbuki vizuri mwaka 2005-2006? (ng'ombe aliuzwa Tshs.Elfu tano tu i.e. 5,000/= per head na bado hakupatikana mnunuzi) Serikali iliwasaidia/ikawapiga tafu kwa kutoa chanjo ya ECF bure au kwa gharama ndogo mno ili kuwajengea tena uwezo kwa ng'ombe wachache waliosalia. Baadhi ya Mashirika e.g. CORDS walinunua na kugawa ng'ombe (ndama) kwa baadhi ya waliofilisika kabisa na hawana tegemeo tena. Lakini ona sasa wamegeuka na kuisakama Serikali. - Acha wakomae hivyo-hivyo na hali yao.
 
na vipi kuhusu majan ambayo ndiyo chakula
Ongezea .. Na vipi kuhusu utunzaji wa hayo mabwawa/ malambo ili yaweze kutumika muda wote hadi kiangazi ?? Na vipi kuhusu matumizi Endelevu ya maeneo au Nyanda za Malisho??
 
Ongezea .. Na vipi kuhusu utunzaji wa hayo mabwawa/ malambo ili yaweze kutumika muda wote hadi kiangazi ?? Na vipi kuhusu matumizi Endelevu ya maeneo au Nyanda za Malisho??
huyu jamaa hapajui vizur huko Simanjiro palivyo
 
Wacha tu ndg. yangu. Ukichanganya Ujinga + Umaskini wa kujitakia + Ujeuri/Ubabe bila maarifa ukiongezea na Mabadiliko ya Tabianchi hupati picha ya nini matokeo yake. Hili lilishawahi kutokea na Serikali sikumbuki vizuri mwaka 2005-2006? (ng'ombe aliuzwa Tshs.Elfu tano tu i.e. 5,000/= per head na bado hakupatikana mnunuzi) Serikali iliwasaidia/ikawapiga tafu kwa kutoa chanjo ya ECF bure au kwa gharama ndogo mno ili kuwajengea tena uwezo kwa ng'ombe wachache waliosalia. Baadhi ya Mashirika e.g. CORDS walinunua na kugawa ng'ombe (ndama) kwa baadhi ya waliofilisika kabisa na hawana tegemeo tena. Lakini ona sasa wamegeuka na kuisakama Serikali. - Acha wakomae hivyo-hivyo na hali yao.
hali ikiendelea hiv ndipo tunapoelekea huko kuuza ng'ombe bei ya kuku wa kisasa
 
View attachment 2080443
Mifugo 62,593 imekufa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame. Kati ya mifugo hiyo;

Ng'ombe - 35,746
Kondoo - 15,136
Mbuzi - 10,033
Punda - 1,670

======

Hali ya ukame inayoendelea wilayani Simanjiro mkoani Manyara imesababisha mifugo mbalimbali ikiwemo ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda kufa.

Simanjiro. Mifugo 62,593 imekufa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kutokana kukosa maji na malisho baada ya ukame kuvikumba vijiji mbalimbali katika wilaya hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Sendeu Laizer ameyasema hayo Januari 13 kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo.

Sendeu ameitaja mifugo hiyo iliyokufa kuwa ni ng'ombe 35,746, kondoo 15,136, mbuzi 10,033 na punda 1,670.

Amesema katika kipindi hiki hali ya mifugo katika maeneo mengi ya Simanjiro siyo ya kuridhisha kutokana na uhaba wa maji na malisho.

Amesema ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za vifo vya mifugo kutokana na athari za ukame unaendelea katika vijiji vyote.

"Hali hii imesababisha baadhi ya mifugo kufa na wafugaji wengi kuhama na kurundika katika maeneo machache yenye maji na malisho," amesema Sendeu.

Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema kutokana na ukame huo jamii nyingi zimeingia kwenye umaskini kutokana na mifugo yao kufa.

Ole Sendeka amesema kwa sababu ya ukame uliopo nchini baadhi ya wafugaji wamehamisha mifugo yao nje ya nchi ili zipate malisho.

Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian ametoa ombi kwa Serikali kuruhusu mifugo kuingia ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite ili kupata malisho.

"Mifugo ni benki ya jamii za kifugaji sasa inapokufa kwa ukame inakuwa tatizo tunaiomba Serikali iruhusu mifugo kuingia ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite kwani haitadhiriana," amesema Taiko.

Simanjiro yapitisha Sh25.2 bilioni

Wakati huo, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wamepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya Sh25.2 bilioni kwa ajili ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Ofisa mipango wa halmashauri hiyo, Heri Kuria amesema bajeti hiyo imelenga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu.

Amesema katika bajeti ya 2022/2023 halmashauri hiyo itatekekeleza miradi mbalimbali na katika bajeti hiyo itaongeza ujenzi wa madarasa ya shule za msingi 20, shule mpya ya sekondar na kituo cha afya.
NAOMBA SERIKALI INIKOPESHE MILIONI 500 , wa nope ardhi hekari 1000! Nikomeshe hii njaa na vifo vya mifugo!
Nikama utani lakini mtastaajabu
 
Wamasai wapo nyuma Sana kielimu mamlaka ya utabiri wa Hali ya hewa walishatoa taadhari hivyo sikutegemea mifugo itakufa mingi kiasi hichi
 
Back
Top Bottom