Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kuna mmoja nilikuwa napiga naye story yeye akaniambia yaan mm ile kuona hali haieleweki mwezi wa 10 mwaka jana nilikuwa na ng'ombe 82 nikauza nikabakisha wanne tu kwa ajili ya maziwa ile hela nikaenda kulima zangu Vanilla sasa hivi watu wanaliaHao ni ukoo Mollel..wanakaa na ng'ombe hadi anazeeka na kufa..ukoo wa Laizer wajanja, wanauza na kununua mifugo na viwanja pale inapobidi...ndio maana wana mpunga..mara chache utakuta kachoka sana
so kuna koo janja na koo utopoloHao ni ukoo Mollel..wanakaa na ng'ombe hadi anazeeka na kufa..ukoo wa Laizer wajanja, wanauza na kununua mifugo na viwanja pale inapobidi...ndio maana wana mpunga..mara chache utakuta kachoka sana
kuwe na program endelevu ya kuanzisha misitu iliyoanzishwa na waTz tukiacha ile ya asiliUkipita Kibaha unakutana na jamaa wengi na mabodaboda wamebeba magunia ya mkaa ktk namna unayojiridhisha kabisa miti na mapori ya mvua huko yanateketea.......tusipochukua hatua tutajuta...mkaa wa miti upigwe marufuku tutengeneze mkaa wa taka........kila kijiji kama alivosema mdau hapo kila mwaka angalau wapande miti isiyopungua LAKI MOJA.
Tuokoe vizazi...wasimamiaji SERA ongozeni mapambano
Mali ya mbahili huliwa na mchwaMmasai yupo radhi ng'ombe afe sio kuchinja au kuuza
Serikali itenge maeneo makubwa ya ufugaji,kama Morogoro,Iringa,Kiteto,Muheza ,Kigoma,na Rukwa na Kagera.Then ianzishe kilimo cha nyasi za malisho...zizalushwe kitaalam.ili zisaidie wakati was ukame au kiangazi.Hebu toa pendekezo au Ushauri nini kifanyike.
Kuitaja Serikali haimanishi ,Serikali ndio itengeneze malisho...KAZI ya Serijali ni kuweka mazingira mazuri na kuwezesha kama ulivyohitimisha !Ndugu tupo kwenye Ubebari sio kila kitu Serikali umeona fursa hiyo itumie...Nenda TIC waambie nataka kuwekeza nataka Ardhi...Kwa kuanzia unatakiwa uwe $100,000/-
Serikali iweke Mazingira mazuri ya kuwekeza basi.
Dah imeanza migugo baadae itakuja kwetuView attachment 2080443
Mifugo 62,593 imekufa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame. Kati ya mifugo hiyo;
Ng'ombe - 35,746
Kondoo - 15,136
Mbuzi - 10,033
Punda - 1,670
======
Hali ya ukame inayoendelea wilayani Simanjiro mkoani Manyara imesababisha mifugo mbalimbali ikiwemo ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda kufa.
Simanjiro. Mifugo 62,593 imekufa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kutokana kukosa maji na malisho baada ya ukame kuvikumba vijiji mbalimbali katika wilaya hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Sendeu Laizer ameyasema hayo Januari 13 kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo.
Sendeu ameitaja mifugo hiyo iliyokufa kuwa ni ng'ombe 35,746, kondoo 15,136, mbuzi 10,033 na punda 1,670.
Amesema katika kipindi hiki hali ya mifugo katika maeneo mengi ya Simanjiro siyo ya kuridhisha kutokana na uhaba wa maji na malisho.
Amesema ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za vifo vya mifugo kutokana na athari za ukame unaendelea katika vijiji vyote.
"Hali hii imesababisha baadhi ya mifugo kufa na wafugaji wengi kuhama na kurundika katika maeneo machache yenye maji na malisho," amesema Sendeu.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema kutokana na ukame huo jamii nyingi zimeingia kwenye umaskini kutokana na mifugo yao kufa.
Ole Sendeka amesema kwa sababu ya ukame uliopo nchini baadhi ya wafugaji wamehamisha mifugo yao nje ya nchi ili zipate malisho.
Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian ametoa ombi kwa Serikali kuruhusu mifugo kuingia ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite ili kupata malisho.
"Mifugo ni benki ya jamii za kifugaji sasa inapokufa kwa ukame inakuwa tatizo tunaiomba Serikali iruhusu mifugo kuingia ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite kwani haitadhiriana," amesema Taiko.
Simanjiro yapitisha Sh25.2 bilioni
Wakati huo, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wamepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya Sh25.2 bilioni kwa ajili ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Ofisa mipango wa halmashauri hiyo, Heri Kuria amesema bajeti hiyo imelenga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu.
Amesema katika bajeti ya 2022/2023 halmashauri hiyo itatekekeleza miradi mbalimbali na katika bajeti hiyo itaongeza ujenzi wa madarasa ya shule za msingi 20, shule mpya ya sekondar na kituo cha afya.
Ukijikita Sana kutetea Serikali ,utajikuta hata kufikiri hutumii kichwa Tena!mkuu Serikali ndo imeleta ukame? Kwamba unataka serikali iagize mahindi ya msaada ili hao mifugo wawe wanapikiwa ugali?
Ungetoa na mbinunza namna gani serikali iwasaidie hao mifugo,sio kutoa rawama bila ya suruhisho!!
Toa suruhisho mkuu na sio kulalama dhidi ya serikali yako
Kabisa tena ile ya asili miche ya miti asili ipo inazalishwa Morogoro na kwingineko kwa wingi tu nawaza TAFORI wangeingilia hapo kuona kila pahala nchini panafaa kupandwa miti gani ipandwe kote bila kujali ni singida dodoma au Rombokuwe na program endelevu ya kuanzisha misitu iliyoanzishwa na waTz tukiacha ile ya asili
point point [emoji122][emoji122]Wafugaji wanabidi watambue Mambo yafuatayo alafu wajiongeze akili 1. Hv hali ya hewa inaweza kurudi tena kama zaman. Yaan kuwe na mvua za uhakika kipindi cha masika na vuli? Kwangu Mimi naona hali hiyo haiwezi kurudi tena lamda kwa huruma ya Mungu. 2. Je? Wanatambua kuwa wao ni miongoni mwa jamii haribifu sana wa mazingira. Wanajitihada zozote wanazofanya kurekebisha uharibu wa mazingira wanaoufanya Kila mwaka. Sababu nachoona wao wakishaharibu wanahama kutafuta maeneo mazuri ili kuharibu tena. 3. Je kumiliki mifugo Mingi wasiokuwa na uhakika wa malisho unatija kuliko kuwa na mifugo michache ya kisasa au mbegu mchanganyiko ambao watahitaji eneo ndogo la malisho. 4. Hv ni kweli Kila Jambo ni la kuisubiri serekali? Nilitegemea nisikie kilio cha mkukosekana majani ila sio maji. Wafugaji mpo miambili na Kila mmoja anamili ng'ombe mia Moja hv mnashindwa Kila mmoja kutoa ng'ombe wawili au watatu mkauza mkapata milioni miatatu mkatengeneza malambo kwa ajili ya kutunzia maji. 5. Hv jamii ya ufugaji inajua Siasa Ina mustakabadhi wa maisha Yao. Au wao huwa wanachagua tu viongozi ilimradi bila kujua madhara ya kutokuchagua viongozi Bora.
kabisaKabisa tena ile ya asili miche ya miti asili ipo inazalishwa Morogoro na kwingineko kwa wingi tu nawaza TAFORI wangeingilia hapo kuona kila pahala nchini panafaa kupandwa miti gani ipandwe kote bila kujali ni singida dodoma au Rombo
Nilishajibu kuwa Makini fuatilia threadMkuu Umeambiwa hata nyasi hakuna, Kwahiyo ngombe atashindia maji?
Toa na suruhisho la upatikanaji wa malisho,kwa tatizo la maji nakuunga mkono ,je malisho serikali isaidie vipi?
Nilishajibu kuwa Makini fuatilia thread
safari bado n ndefu sanaKwenye Taifa kama hili Mungu hawezi kuleta mvua kamwe,labda alete kimbunga cha Nzige badala ya mvua[emoji116][emoji1782][emoji1782][emoji1782]
View attachment 2082145