Manyara: Simanjiro walia kwa uhaba wa mvua, mifugo 62,500 imekufa

Manyara: Simanjiro walia kwa uhaba wa mvua, mifugo 62,500 imekufa

Kuna baadhi ya maeneo ya mkoa wa Manyara leo usiku nimeapata taarifa imenyesha mvua ya kutosha...
 
View attachment 2080443
Mifugo 62,593 imekufa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kwa kukosa maji na malisho kutokana na ukame. Kati ya mifugo hiyo;

Ng'ombe - 35,746
Kondoo - 15,136
Mbuzi - 10,033
Punda - 1,670

======

Hali ya ukame inayoendelea wilayani Simanjiro mkoani Manyara imesababisha mifugo mbalimbali ikiwemo ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda kufa.

Simanjiro. Mifugo 62,593 imekufa wilayani Simanjiro mkoani Manyara kutokana kukosa maji na malisho baada ya ukame kuvikumba vijiji mbalimbali katika wilaya hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Sendeu Laizer ameyasema hayo Januari 13 kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo.

Sendeu ameitaja mifugo hiyo iliyokufa kuwa ni ng'ombe 35,746, kondoo 15,136, mbuzi 10,033 na punda 1,670.

Amesema katika kipindi hiki hali ya mifugo katika maeneo mengi ya Simanjiro siyo ya kuridhisha kutokana na uhaba wa maji na malisho.

Amesema ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za vifo vya mifugo kutokana na athari za ukame unaendelea katika vijiji vyote.

"Hali hii imesababisha baadhi ya mifugo kufa na wafugaji wengi kuhama na kurundika katika maeneo machache yenye maji na malisho," amesema Sendeu.

Mbunge wa jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema kutokana na ukame huo jamii nyingi zimeingia kwenye umaskini kutokana na mifugo yao kufa.

Ole Sendeka amesema kwa sababu ya ukame uliopo nchini baadhi ya wafugaji wamehamisha mifugo yao nje ya nchi ili zipate malisho.

Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Kurian ametoa ombi kwa Serikali kuruhusu mifugo kuingia ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite ili kupata malisho.

"Mifugo ni benki ya jamii za kifugaji sasa inapokufa kwa ukame inakuwa tatizo tunaiomba Serikali iruhusu mifugo kuingia ndani ya ukuta wa madini ya Tanzanite kwani haitadhiriana," amesema Taiko.

Simanjiro yapitisha Sh25.2 bilioni

Wakati huo, madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wamepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya Sh25.2 bilioni kwa ajili ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Ofisa mipango wa halmashauri hiyo, Heri Kuria amesema bajeti hiyo imelenga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu.

Amesema katika bajeti ya 2022/2023 halmashauri hiyo itatekekeleza miradi mbalimbali na katika bajeti hiyo itaongeza ujenzi wa madarasa ya shule za msingi 20, shule mpya ya sekondar na kituo cha afya.
Hawakuona kwamba Hali ni mbaya wauze waje kununua baadae? Ngoja zipukutike ndio akili zikae sawa.

Pia huwa wanawaambia wakate bima za majanga huwa hawataki,kiufupi wafugaji Wana uwezo ila huwa ni jeuri.
 
Kuna baadhi ya mkoa wa manyara leo usiku nimeapata taarifa imenyesha mvua ya kutosha...
Shida ya mvua ya mwaka huu imekaa kiswahili Swahili na inanyesha kimafungu.

Yaani inaweza piga leo ya kuzidi eneo x ikawatia tumaini kwamba imerudi,mtalima na mtapanda baada ya hapo tukutane baada ya wiki 3 yanakuja manyunyu.

Kuna maeneo miezi hii huwa hayapotiki kwa maji saizi ukija unanunua kiwanja na utapapenda ila sasa mwaka mwingine utajuta.
 
Tusiende mbali, hapa chalinze na Bagamoyo tu mifugo imekufa sana
 
Hali ya ukame inayoendelea Baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Manyara inatisha !HaI Sasa Simanjiro pekee ng'ombe 35,000 + wamekufa,mbuzi 10,000,kondoo 15,000 !
Hili ni janga!
Hivi Serikali imekosa mbinu za kuwaokoa wanyama Hawa!
mkuu Serikali ndo imeleta ukame? Kwamba unataka serikali iagize mahindi ya msaada ili hao mifugo wawe wanapikiwa ugali?

Ungetoa na mbinunza namna gani serikali iwasaidie hao mifugo,sio kutoa rawama bila ya suruhisho!!

Toa suruhisho mkuu na sio kulalama dhidi ya serikali yako
 
Serikali ambayo inahamasisha ufisadi bila aibu tena kupitia TV ya Taifa haiwezi kuona janga lolote lile katika nchi.
View attachment 2080730
Mkuu mbona uneteseka saana na hii kauli?
4052b00499a8a01d9fbb.jpg
 
hata nikitoa pendekezo halitofanyiwa kazi maana sio kipaumbele chao kwa sasa wamasai nawapa pole tu wakomae hivyo hivyo
Mkuu Kwahiyo malalamiko yako ndo yatafanyiwa kazi?


Kwahiyo wewe kulalama Ni vema kuliko kutoa suruhisho la malalamiko yako?
 
Serikali inapaswa kuchimba mabwawa kadhaa yatakayohifadhi maji ya mvua ili kusaidia mifugo isife wakati wankiangazi maana kwa wakati wa jua ng'ombe hunywa maji hata ndoo nne hadi tano kwa siku.
Mkuu Umeambiwa hata nyasi hakuna, Kwahiyo ngombe atashindia maji?

Toa na suruhisho la upatikanaji wa malisho,kwa tatizo la maji nakuunga mkono ,je malisho serikali isaidie vipi?
 
masai anaona fahari yaan yeye fahari yake n kuwa na ng'ombe nyingi hapo analala kwenye kijumba kilichokandikwa kwa mavi ya ng'ombe yaan utajiri anaulalia [emoji848][emoji848]
umasain ukiwa na ng'ombe nyingi unajeshimika sana
Hao ni ukoo Mollel..wanakaa na ng'ombe hadi anazeeka na kufa..ukoo wa Laizer wajanja, wanauza na kununua mifugo na viwanja pale inapobidi...ndio maana wana mpunga..mara chache utakuta kachoka sana
 
Back
Top Bottom