Maombi, sala na dua za mke wangu ni kero kwangu

Maombi, sala na dua za mke wangu ni kero kwangu

Nina mwaka wa nane wa ndoa na hakika nimekuwa ni mvumilivu Sana na mwaminifu Sana kwa ndoa yetu.
Nimezaliwa na kukulia kwenye familia ya Kikristo yenye msimamo mkali wa kiimani, hivyo Basi sijawahi kuvuta sigara, kunywa Pombe na hata uzinzi sio mzinzi, mke wangu ni mwanamke pekee kulala naye tangu nizaliwe.
Kinachonikera kwa miaka yote hiyo mke wangu amekuwa akitamani Sana kumjua mwanamke ninaye tembea naye nje ya ndoa.
Mara ya Kwanza nikajua ananitania, Mara kwa Mara alikuwa ananiambia darling natamani nimjue mwanamke unayetembea naye, nione kanizidi nini?
Daima jibu langu Mimi nimeokoka siwezi kuwa na mtu mwingine zaidi yako.
Haniamini na haamini majibu yangu, simu zangu na e mails yeye ndiye huset password, ana access nazo muda wote.

Sasa kuanzia juzi Yuko kwenye maombi, anaomba aonyeshwe kwa namna yoyote mwanamke ninayetembea naye, maana anachojua yeye hamna mwanaume asiyechepuka.
Mbaya zaidi anaomba kwa kulia kwa sauti huku akipigapiga ukutani.
Huyu ana kaugonjwa ka akili 100%
Mpeleke kwa wataalam wa saikolojia Hosipitalini, sio kwa hawa kina nanihii
 
Mimi alikuwa anaomba eti niache pombe nikamwambia hiyo sala yako ikifanikiwa utakufa njaa na watoto hawataenda shule kwani kwenye pombe ndio natengeneza mipango ya pesa!

Na nikamwambia sala zako usiku sana ni kero nitakuwa siji mpaka umalize kwani unanikosesha usingizi .sali mapema au nenda kanisani.

Akafyata mkia kwani nilikuwa ikifika saa sita usiku nampigia kama bado anaendelea na kelele zake za maombi ili niendelee kupika stori sitaki kurudi nikute nyumba imebadirishwa kanisa
Asee kuna wanawake wameolewa na wanaume wa ajabu sana. Anyway pols yake
 
Mkuu labda nikushauri tofauti, kama hujawahi kabisa kuwa na mwanamke mwingine, ujue mkeo anataman upate mwanamke atakaelifundisha mambo flani, kuna jambo kama mwanaume hulifanyi kisawasawa, hivo anaona akikuambia atakuvunja moyo so anatafta mtu wa kumtupia zigo ili upate 3xperience. Nashukuru kama utaelewa.
 
Asee kuna wanawake wameolewa na wanaume wa ajabu sana. Anyway pols yake
Pole yako wewe ambaye unajidai mtu wa sala halafu unaingiza hela mara moja kwa mwezi kama period! Hatujawahi kukuomba hela za matumizi we mwema
 
Nina mwaka wa nane wa ndoa na hakika nimekuwa ni mvumilivu Sana na mwaminifu Sana kwa ndoa yetu.

Nimezaliwa na kukulia kwenye familia ya Kikristo yenye msimamo mkali wa kiimani, hivyo Basi sijawahi kuvuta sigara, kunywa Pombe na hata uzinzi sio mzinzi, mke wangu ni mwanamke pekee kulala naye tangu nizaliwe.

Kinachonikera kwa miaka yote hiyo mke wangu amekuwa akitamani Sana kumjua mwanamke ninaye tembea naye nje ya ndoa.

Mara ya Kwanza nikajua ananitania, Mara kwa Mara alikuwa ananiambia darling natamani nimjue mwanamke unayetembea naye, nione kanizidi nini?

Daima jibu langu Mimi nimeokoka siwezi kuwa na mtu mwingine zaidi yako.
Haniamini na haamini majibu yangu, simu zangu na e mails yeye ndiye huset password, ana access nazo muda wote.

Sasa kuanzia juzi Yuko kwenye maombi, anaomba aonyeshwe kwa namna yoyote mwanamke ninayetembea naye, maana anachojua yeye hamna mwanaume asiyechepuka.

Mbaya zaidi anaomba kwa kulia kwa sauti huku akipigapiga ukutani.
Anamtumia Mungu vibaya
 
Bujibuji umeokoka???
Mi alianza kuniombea niache pombe,nikamkalisha chini nikamwambia kwa upole kuwa pombe nimetoka nayo mbali sana kuliko yeye,halafu imeshaniharibia sana maisha maana niliianza bado nasoma labda ningekua na maisha mazuri zaidi kuliko haya sasa nitakua mpumbavu na mjinga wa mwisho kuiacha pombe leo nina kipato changu wakati nilishawahi kunywea hela ya ada.
 
Mwambie analolitafuta atalipata soon
Ni agent wa shetani, anataka kuniangusha dhambini.
Hi ni baadhi ya mistari ninayosimama nayo tangu nikiwa mdogo.

Mithali : Mlango 6​

32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

1 Wakoritho : Mlango 6​

18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
 
Umenifanya nirud kuangalia mleta mada Ni Nani, kumbe Ni buji!!! Chai hii

1 Wakoritho : Mlango 6​

18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
 
Dah......

Huyo mpe anachokitafuta.... Mwambie naona unataka kuniona nikicheat nakuwaje, ngoja nikuonyeshe.

Wanawake wanamajaribu sana. Mimi pia kuna kipindi nafukuzia binti, nilikuwa sijala mzigo kama miwezi minne hivi, nashukuru kazi na majukumu vilinibana nikawa sipati akili ya ashki na ushawishi.
Nakutana na kabinti kanaanza nihoji kuwa muda wote huo kweli nikae bila mwanamke basi nitakuwa mtu wa mechi za kimya kimya.

Namuelekeza ila wapi hilo ndilo swali lake kila siku ananikazania. Alikuwa ananikera.
 
Back
Top Bottom