Maombi yenu tafadhali

Maombi yenu tafadhali

Habari za asubuhi ndugu zangu wa JF,

Leo asubuhi tarehe 29/03 ni siku ya furaha kwangu kwa sababu kuu mbili. Kwanza kabisa ni siku ya kuzaliwa mke wangu mpendwa, ametimiza miaka 29🙂. Namtakia kheri ya kuzaliwa na ningependa kusheherekea nanyi ndugu zangu.

Pili, Leo hii tuko hospital magomeni hapa. Mda huu amepangiwa c section (kujifungua kwa operation). Huyu akiwa mtoto wetu wa pili. Hivi navyoandika hapa yuko chumba cha upasuaji (Theatre) na mimi niko nje nasubiri.

Ndugu zangu huu ni mwezi wa Kwaresma na pia ni mwezi wa Ramadhani. Tuwe pamoja na kheri njema ya maombi yenu.

Ndugu yenu Gily . .

Updates:
07:41 Nimefurahi sana ndugu zangu nimepata mtoto wa kiume. Niko nae hapa analia kinyama mpaka natamani nilie. Mungu kanipa hitaji la moyo wangu, nilikuwa natamanj sana kuwa na mtoto wa kiume. .

Mke wangu bado yuko chumba cha upasuaji. Nimepewa taarifa she is doing fine ila bado wanamshona na kumsafisha. I can't wait to see her.
Hongera sana sana
 
Zaburi 23:1-6

"BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu"
Hongera tena na tena Gily
Shukrani sana shangazi Leo umekuwa bibi😀
 
Back
Top Bottom