Maoni: Ifanyike tathmini ya Uchaguzi wa 2019/2020 kabla ya kufanyika uchaguzi 2024/2025

Afadhali uchaguzi usifanyike ikiwa hatutapata Tume huru ya Uchaguzi.

Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kwanza, uchaguzi baadae.
 
2024 itatupa majibu sahihi.
 
Nadhani suala la Katiba Mpya liendewe kimkakati kwa kuanza na reformation kwa maeneo kadhaa kabla ya kulivaa mazima. Issue za muundo wa Tume ya Uchaguzi,matokeo ya Rais kupingwa mahakamani, na maeneo mengi katiba pendekezwa ya Samwel Sitta ingefaa.
Uko sawa, reform zinahitajika,

Lakini Watawala hata hizo reforms zinazolenga kumpunguzia Rais mamlaka kuingilia uchaguzi hawazitaki.

Tume huru bila mabadiliko makubwa kwenye Katiba Bado ni kiinimacho.

Uchaguzi bila Tume huru ya Uchaguzi wa KAZI Gani?
 
Tunawezaje kuanza kupanga safu za 2024/2025 bila kujua tumeondoa vipi sintofahamu ya 2019/2020!!!
 
Hapana 2024 tuna uchaguzi muhimu sana wa serikali za mtaa nchi nzima, hatuwezi kuchanganya jambo hili na katiba mpya ambayo ni muhimu zaidi pia.

Maandalizi ya vyote hivi yanahitaji utulivu, mipango, fedha na muda wa kutosha kujiandaa.
Muwe na subra, muwe wastahimilivu.
Mambo mazuri hataki haraka.
 
Kwamba tupuuzie kilichotokea 2020?
Yeah,tupuuzie kwa kuwa majibu yake tayari tunayajua.

Kwa nchi maskini kama hii hizo gharama za kufanya Tathmini, ziende zikafanye kazi nyingine, zijenge daraja kule Lindi walikofariki watoto wa shule wa darasa la 4 wakati wakijivusha kwa mtumbwi.
 
Pesa ya tathimini utatoa ww. Na hapo bado tena pesa ya uchaguzi wa 2025
 
Yeah,tupuuzie kwa kuwa majibu yake tayari tunayajua.

Kwa nchi maskini kama hii hizo gharama za kufanya Tathmini, ziende zikafanye kazi nyingine, zijenge daraja kule Lindi walikofariki watoto wa shule wa darasa la 4 wakati wakijivusha kwa mtumbwi.
Si lazima kutumia pesa mingi kufanya TATHMINI,

Unaitishwa mdahalo hapo UD, wazalendo wanahudhuria Bure kabisa tunayaongea ya nchi yetu tun ayamaliza.

Madaraja miaka sitini sasa Bado mnajenga madaraja kana kwamba Nchi inatanuka na kuongezeka ukubwa.
 
Uwezekano wa chaguzi zetu kuwa za haki hautakuwepo iwapo Bado ccm inaamini inastahili kubaki madarakani no matter what. Kitakachofanyika ni kupitisha Sheria za hadaa kwa lengo la kupata idadi ya kuridhisha ya wapiga kura ili iwe hadaa ya kuombea mikopo na misaada huko nje.

Hakuna uwezekano wa ccm kuheshimu uchaguzi wakati wanajua kizazi hiki hakiwezi kuichagua. Ninatarajia chaguzi zetu zitazidi kuwa na idadi ndogo sana ya wapiga kura, Hadi yatokee mabadiliko ya kweli kwenye katiba na tume ya uchaguzi. Ama machafuko au mapinduzi ya kijeshi na mifumo ya uchaguzi kurekibishwa, hapo Imani ya box la kura itarejea.
 
Idadi ya wpiga kura kujitokeza kwa wingi ama kwa uchche sio ishu,
Issue ni kwamba watakaoshiriki kupiga kura hata kama ni10, atakae pata kura nyingi zaidi ya mwingine, ndie atakae pata fursa ya ya kuunda serikali na kuliongoza Taifa, kwa mujibu wa sheria, kanuni na katiba ya nchi.
Hilo lazima lieleweke vizuri.
Ukifura, Ukizira, wengine wanasonga barabara bila mbambamba....

if you don"t want to take part into political administration, don"t blame to be ruled by fool.
 
 
Hakuna mtu anayejitambua ataendelea kushiriki kwenye uchaguzi usioheshimiwa. Na aliyekuambia uongozi lazima upatikane kwa njia ya kura ni nani? Hiyo njia ya kura ilikuwa ndio njia sahihi ya kupata viongozi, lakini kama haiheshimiwi, itatafutwa njia nyingine bila kujali athari zake.
 
Tunayo miaka 2 full kabla ya Uchaguzi 2025.

Uchaguzi wa MITAA utasogea 2025.

Miaka 2, yaani 2024 na 2025 inatosha kukamilisha Tume HURU na KATIBA mpya kabla ya kufanyika uchaguzi wowote.

Muda unatosha.
 
Tunayo miaka 2 full kabla ya Uchaguzi 2025.

Uchaguzi wa MITAA utasogea 2025.

Miaka 2, yaani 2024 na 2025 inatosha kukamilisha Tume HURU na KATIBA mpya kabla ya kufanyika uchaguzi wowote.

Muda unatosha.
Haitakua Katiba mpya hiyo ya mwaka moja, itakua Katiba viraka yakurekebisha kila leo.

Kumbuka tunatengeneza Katiba ya nchi sio Katiba ya vikoba.
Ni Lazima wananchi wapate fursa na muda wa kutosha kujadiliana kwa uhuru na kuamua kwa haki kwa pamoja na umoja na kuja na andiko moja la kudumu vizazi na vizazi kwa maslahi mapana ya waTanzania kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni, sayansi na Technolojia.
 
IPO haja ya kusogeza uchaguzi wa MITAA isimamiwe na Tume huru ya Uchaguzi 2025 Badala ya kusimamia na Tamisemi under Mchengerwa.
 
Miaka ni 2 Si mmoja.

Na Elimu ya Katiba mpya tulishaelimishwa na Samia akiwa na Warioba 2011-2014.
 
Ila sio kwa ubaya, hakuna chama cha waenda kwa upepo kama CHADEMA πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Zito kabwe mwanzo kabisa alisisitiza sana umuhimu wa Tume huru kwanza kabla ya katiba mpya, CHADEMA wakaja juu sana wakidai jamaa katumwa, leo hii hao hao CHADEMA ndio namba moja kudai tume huru πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mm Si CHADEMA ni Mwananchi mzalendo.

Tunataka KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Miaka 2 ilobaki inatosha.
 
IPO haja ya kusogeza uchaguzi wa MITAA isimamiwe na Tume huru ya Uchaguzi 2025 Badala ya kusimamia na Yamisemi under Mchengerwea.
Kwenye katiba mypya ambayo mchakato utaanza 2026, chaguzi zote nchini zitakua define very well kwenye katiba hiyo mypya mpaka kura za maoni zitasimamiwaje wakati huo

So,
I can confirm to you without fear of contradiction, uchaguzi wa serikali za mtaa ni mwishoni mwa mwaka2024 na utasimamiwa na TAMISEMI bila mbambamba na ule uchaguzi Mkuu ni October 2025 na utasimamiwa na Tume huru ya uchaguzi ya sasa bila tashwishwi yeyote.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…