SoC03 Maoni kuhusu uwajibikaji na utawala bora

Stories of Change - 2023 Competition

Erajulim2023

New Member
Joined
May 12, 2023
Posts
2
Reaction score
2
UTANGULIZI:
Ili nchi yoyote iweze kuendelea razima iwe na mifumo mizuri ya kiutawala na uwajibikaji, Utoaji wa Elimu kwa wananchi na usimamizi wa rasilimali za Taifa.

Kwa kuzingatia misingi ya maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 na Masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka
1995, ambayo yanamtaka kila kiongozi wa umma kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili kukuza utu, uwazi,
uadilifu, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu utendaji wa Serikali, na kwasababu hiyo
Nikifatilia Muundo wa serikali na mifumo yake kwa Hapa Tanzania ni dhahiri kwamba kuna mambo mengi yanayo hitaji kufanyiwa mabadiliko au Maboresho makubwa sana.

Changamoto zinazo Likabili Taifa letu

Ni:
1. UWAZI SERIKALINI.
2. WAJIBU WA VIONGOZI WA UMMA.
3. UWAJIBISHWAJI KWA VIONGOZI WA UMMA.
4. USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI.

1. UWAZI:
kwa Mujibu wa Katiba Sehem ya pili kipengele cha 8-(a) "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;" Kwa sababu hii
  • Serikali inapaswa kuwa na uwazi kuhusu mikataba mbalimbali inayo saini kuhusu maslahi ya Taifa na wananchi kwa ujumla ambao ni waajiri wake.
  • Wananchi wapewe Uhuru wakuhoji na kutambua haki zao kuhusu mapato na matumizi kuanzia ngazi ya kijiji hadi serikali kuu, nauhuru huo usitoke kwa maneno na maandishi tu, bali kwa vitendo.
Moja ya sababu inayo wafanya wananchi wawe na hofu yakuhoji nakupoteza uhuru wao ni baadhi ya viongozi wa umma kutumia Mamlaka yao kuweza kutangaza vita dhidi ya mtu au watu wanao wachukia hata kwa chuki binafsi bila kufuata sheria, na ivo mwananchi akihoji jambo ambalo linaweza kuleta uwazi na viongozi kuonekana hawafai kwa makosa hayo huyo atachukuliwa kama adui wa Taifa, au Adui wa umma kwa mazingira husika, ili wananchi waweze kuutumia uhuru wao kama katiba inavyo elekeza, itungwe sheria inayo mtaka Kiongozi wa Umma kutotumia madalaka yake kumtishia mwanchi au kumuadhibu mpaka taratibu za kisheria zifuatwe kikamilifu.
* Itungwe sheria itakayo tumika kuajiri watendaji wa serikali ngazi ya Wizara na sio kuteua kisirisiri, Nafasi hizi za kiutendaji serikalini mfano Waziri, katibu mkuu wa wizara, na baadhi ya wasimamizi wapatikane kwakutuma maombi nawajadiliwe na Bunge, wakiwa na sifa zinazo faa wapewe nafsi hizo, na ijulikane kwa wananchi mchakato mzima ulivyo kwenda, kwani Kiongozi huyo anaajiriwa na taifa sio mtu Binafsi.

2. WAJIBU:
  • Swara la viongozi wakuu wa serikali kutambua nakutimiza wajibu wao limekuwa chini sana, na sababu kubwa ni mfumo mbovu uliopo unao tumika kuwateua kutokea kwa Raisi, ili kuondokana na ilo tunapaswa kuwa na sheria inayo mtaka Kiongozi mkuu wa serikali Asifanye uteuzi wa watu wakusimamia sekta au idara wanaotokana na chama chake cha siasa, kwani hii umfanya mtumishi huyo atumie muda mwingi kushugulika na mambo ya chama (siasa) huku akishindwa kutimiza wajibu wake impasavyo.
  • Viongozi wa serikali hasa katika sekta Muhimu, serikali iwe na mfumo mwingine wa kuwaajiri tofauti na uteuzi hiyo itasadia kupatikana kwa watu wenye taaruma na wanao tambua wajibu wao tofauti na kuteuliwa.

3. UWAJIBIKAJI KWA VIONGOZI UMMA
  • Hapa nchini hatuna kabisa mfumo rafiki unao weza kumuwajibisha Kiongozi wa Umma, Ili kufikia hatua nzuri ya viongozi kuwajibika pale wanapo lipeleka taifa kwenye shida yoyote, Tufumue mifumo ya sheria zinazo walinda viongozi wawapo madarakani na baada ya kutoka madarakani.
  • Itungwe sheria inayo muzuia Kiongozi yeyote wa serikali kuanzia ngazi ya Raisi hadi watendaji wa Chini waserikali kumteuwa ndugu kushika Kitengo chochote, au kumuajiri ndugu kwenye nafasi aliyopo yeye, Hii itasaidia kuondoa tabia ya kulindana kwa viongozi na kumfanya kila mtu awajibike kwa jambo alilolifanya.
  • Itungwe sheria inayo vipatia vyombo vya Ulinzi na usalama uhuru wakutokua chini ya watawala wa kisiasa, au Afisa wa ulinzi na usalama asiweze kuagizwa wala kutii amri za kiongozi wa kisiasa, vile vile kuna shida ya Baadhi ya viongozi wa ulinzi na usalama wanaopewa nafasi kwasababu ya ukada wa chama Frani, basi iwepo sheria itakayo wataka viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuwajibishwa pale wanapo jiingiza kwenye siasa.

4. USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI
  • Wananchi wapewe elimu kuhusu haki zao na wajibu wao juu yakufatilia mapato na matumizi ya serikali, njia nzuri inayo weza kufaa kutoa elimu, ni kuachilia Uhuru wa Vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii kwa maswala mazima ya Kuhabarishana na kupeana elimu.
  • Viongozi wa serikali wanajisahau sana kwasababu ya utengano mkubwa kati ya watendaji wa serikali na wananchi, wananchi hatushirikishwi kwenye mambo yanayo husiana na taifa letu, mikataba ya Alimashauri hadi taifa tunasikia tu mradi Frani serikali imesaini mkataba wa Tsh. Billion kadhaa,
tunasikia serikali imekopa Trion kadhaa
tunaskia serikali imetangaza Tozo kwenye bidhaa hali yakuwa wananchi ambao ni walipaji wa hizo gharama hatujulishwi, na hii ndio sababu Viongozi wanaweza kukosea na hakuna wakushinikiza wawajibishwe, kwani hata muwajibishaji mwenyewe hajui Mwanzo wa tatizo, na hajui aanzie wapi.

HITIMISHO
Itungwe sheria inayo mtaka Raisi na waziri wa Fedha kabla ya taifa kukopa watoe waraka wenye sababu za wazi kwanini nchi ikope wakieleza na njia zitakazo tumika kulipa mkopo, kwa ruhusa ya wananchi wanaweza kusaini mkataba wa mkopo husika.
 
Upvote 4

Vizuri
 
Back
Top Bottom