Sio uvumilivu boss ni kukosa namna tu na umaskini.

Kuna jamaa zangu waliamishwaa baadae wakaambiwa hakuna hela za uamisho warudi kwenye vituo vyao vya kwanza, kwa usumbufu huu unadhani madaktari au mwanasheria anaweza ambiwa!?
 
Mpwayungu Mimi natamani ualimu jaman sijaajiriwa na degree yangu hii tangu 2015 hao waalimu wa cheti tuu hapa nyumbani wananidharau na ni ndugu zangu [emoji24][emoji24][emoji24] usiombe najuta hata kusoma
Mkuu mara kadhaa nimekua nasoma jumbe na thread zako mbali mbali sometimes naingiwa na huruma ya kibinadamu maana hustle nazijua njaa naijua + msoto

NB
Toka kwenye Hilo Gerezani (Psych prison) shukuru Kwa hiyo degree ELIMU iwe ngao ya wew kuweza kupambana kutimiza ndoto zako inatakiwa saivi uwe umesha Anza kuwaza nini unataka maishani usipoteze muda kuwaza ualimu utapoteza muda.,
 
Mbona Leo kawasilisha poa sanaa bila matusi.
Kiukweli kabisaaaa ""UALIMU SIO KAZI""
Ni vile raia hawana option sasa WATAFANYAJE??

#YNWA
 
Nashangaa watu wanao sifia kazi ya UALIMU humu ndani halafu kwenye ukoo wao hakuna mwalimu hata mmoja, hakuna mtu mwenye uwezo wa kujisomesha chuo halafu akasomea Ualimu.
 
Umenena vyema. Huko future hakuna kabisa wapo jamaa miaka 20 ni Mwalimu hata PIKIPIKI ya milioni 2 ameshindwa kununua utasema hiyo ni kazi ya kufanya.!!?

Kama mtu anataka apate uhakika wa kula na kuvaa mitumba basi Ualimu utamfaa.
 
 
Childish, silly and illogical.
 
Tatizo ni walezi wananipa pressure wananilinganisha mpaka najiona nimechelewa Yani Kila siku vibonzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…