Maoni, Mapendekezo na Ushauri kwa Walimu
Kuna wakati alifungiwa naona karudi

Yeye kama ualimi haupendi aachie wengine wanaopenda hata vyakula kuna mwingine anapenda hiki kile hapendi

Lakini huyu mwenzetu mleta mada anahitaji tiba ya akili ana dalili za ukichaa.Kitu.kama hukipendi huwezi kuwa kutwa unaongelea hicho tu ni dalili.ya ugonjwa wa akili awahi hospital sio siri na naongea kwa dhati.Hasora ya muda mrefu kwenye kitu.kile kile huzalisha ukichaa

Muda si mrefu atatupa nguo.na kutembea uchi barabarani walio karibu naye wamshauri
Ajabu kasomea ualimu. Ana utukana sababu kakosa ajira kila akiomba
 
Anajua waalim wa leo ndio wa enzi zile za ualimu wito!!. Siku hizi ualimu kazi.
Sawa wapo choka mbaya kama walivyojaa kwenye kila kada nyingine.
Hali jui hilom waalimu wamejiongeza kupitia mikopo wana biashara nzuri zinawapa goodlife. Kenge ambae hata akiambiwa hapo alipo atoe 5M hana na hata dhamana ya kukopa hana.
 
Hizi ndio akili za kimaskini hasa Walimu. Utaskia Bora Mimi Nina hata hiyo laki mbili.

Basi ndugu sio vita TUISHI.
Waoneeni huruma basi hao walimu mnaowadharau na kuwasimanga humu kila siku. Utadhani hamna ndugu zenu ambao kula na kuvaa kwao kunategemea huo huo ualimu na ikitokea umekwenda kumtembelea hicho kinywaji au chakula atakachokuandalia kitakuwa kimetokana na kazi hiyo ya ualimu.
 
Ualimu ni kazi fulani hivi ya hovyo kichizi yaani, ukiwa mwalimu kila mtu ni bosi wako mwanakijiji, mwenyekiti wa kamati ya shule, mwenyekiti wa Kijiji, diwani, mwenyekiti wa ccm, wajumbe wa kamati ya shule, mwalimu mkuu, mwalimu wa taaluma, mwenyekiti wa kitongoji, afisa elimu kata, mtendaji wa Kijiji, mtendaji wa kata, diwani, wachungaji na masheikh, afisa elimu wilaya...n.k

Tena usiombe uwe mwalimu wa vijijini ndo balaa kubwa

TAMISENGA[emoji28]
 
Kibaya zaidi hadi wanafunzi wanapewa ukubwa wasiostahili,
Angalia lile tangazo la haki elimu, wanafunzi wanapewa airtime eti washiriki kwenye vikao vya bodi

Sasa mtu amesoma hadi university halafu akae na mtoto wa form one au four kwenye kikao cha bodi si upumbavu huo

Maana yake walimu pamoja na kusoma hawaaminiki

Mbona vikao vya madaktari hawakai na wagonjwa?

Polisi mbona hawakai na wafungwa?

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hii kazi ni ya kipweke sana, unakuwa mnyonge popote ulipo maana huna nguvu ya pesa kwahiyo huwezi kufanya chochote kwenye watu wengi. Hii kazi inahitaji moyo wa chuma

Haina allowance yoyote ileeee, hata kuhama tu ni bure ukibahatika kupewa pesa basi ni laki tano au million moja. Walimu wanaishi ili wasife tu ila hawana future yoyote ileeee

Poleni sana walimu
Sisi Waalimu tunajivunia kazi yetu na tunaipenda
 
Mbona walimu wanaheshimika sana kitaaa? Wewe unayewadharau ndo kinyaa! Wana kipato halali hawajaja kwako kukopa! Wanatufundishia watoto wetu! Mungu awabariki sana walimu wetu! Nyerere alikuwa mwalimu! Magufuli alikuwa mwalimu! Zaidi ya 50% ya viongozi wetu (mawaziri na wabunge) walipitia ualimu!

Unajua kwanini viongozi wengi walikua walimu?jibu ni moja tu walikimbia maslahi duni katika ualimu.
 
Sio uvumilivu boss ni kukosa namna tu na umaskini.

Kuna jamaa zangu waliamishwaa baadae wakaambiwa hakuna hela za uamisho warudi kwenye vituo vyao vya kwanza, kwa usumbufu huu unadhani madaktari au mwanasheria anaweza ambiwa!?

[emoji28][emoji28] daah
 
Nakumbuka miaka ile wanaweka vigezo vya kupata mikopo ya chuo, course niliyochaguliwa sikupata sifa ya kupewa mkopo.

Nikapewa option nibadili course kwenda ualimu ili nipate mkopo, nikakataa.

Nikalazimika kukaa nyumbani mwaka mzima nikijipanga, mwaka uliofuata nikapata chuo course ile ile niliyochaguliwa mwaka jana. Kwa sababu ndio course nilikua napenda.

Najiuliza, hivi kwa principle zangu hizi, ningekua mwalimu si ningekua nishafukuzwa kazi ama kuacha kazi?

Ualimu bongo ni kazi inayotaka uwe na wito na uwe na moyo.
Mnacomplicate maisha sana!!

Utajiri au kufanikiwa kimaisha ni mind set na sio tu aina ya KAZI unafanya!!


Wenye hela sana na SIO za mawazo ni wanasiasa tu!!

Wengine bila AKILI kichwani na Strong mindset sahau mafanikio maishani!
 
Sasa kwenye hii nchi sehemu kazi gani upande wa serikali inapesaa mnoo..tukiachana na sekta binafsi na taasisi za umma?
 
Back
Top Bottom