Mimi ni mwalimu nakiri kuna muda Mpwayungu Village ana uwasilishaji mbaya wa kuwakera watu


Ila twende mbele turudi nyuma UALIMU sio kazi, tunafanya kwa ajili ya dhiki tu

Anachosema ni ukweli kabisa, tujitafute ualimu sio kazi


Yaani mtu usome hadi degree halafu unakutana na gross salary ya 700,000 ukikatwa makato yote unapata 450,000

H
 
Narudia tena ualimu mnaopigia kelele Ni grade A Kuna watu wanapokea fedha nzuri tunachozidiwa na kada nyingine Ni allowance tu
 
Hamjui chochote mimi Ni mwalimu nimeanza kazi 2012 take home yangu ilikuwa laki nne na point uliza now nachukua shngp Kuna kada nyingi tumewapita kwa mishahara tatizo mnadhani Kila mwalimu grade A
Mkuu

Achana nao.hao hawajui kitu!

Mimi.mwenyewe 2014 nilianza na take home kilo tano na point sasa naogelea kwenye m point!plus vitega uchumi kibao vya zaidi ya kilo sita per month!

Wnafikiri maisha ni kama kufeli kwa mawazo Yao!!
 
Mnacomplicate maisha sana!!

Utajiri au kufanikiwa kimaisha ni mind set na sio tu aina ya KAZI unafanya!!


Wenye hela sana na SIO za mawazo ni wanasiasa tu!!

Wengine bila AKILI kichwani na Strong mindset sahau mafanikio maishani!
Kweli kiongozi, lakini kumbuka walimu 95% wapo kwenye comfort zone, yaani kazi yenyewe inakufanya uwe katika mazingira ya kukufanya ushindwe kufikiria na kufanya mambo makubwa /mabadiliko

Yaani ukiwa katika mazingira ya ualimu/shule hata ufikikiriaji kuhusu maisha yako/hatma au future yako inakuwa limited (job induced comfort zone) kitu ambacho ni ngumu kutoboa


Yaani watu wanaokuzunguka wanaimpact kubwa katika mabadiliko yako

Mtu akiwa mfanya usafi wa benki akawa analipwa 500k ana uwezo wa kumuacha mbali mwalimu kimaendeleo sababu watu anaofanya nao kazi ni somo tosha katika maisha yake (mabadiliko)

Watu na mazingira unayofanywa kazi ni stimulants katika kukufanya udumae au ukue kifikra na maendeleo kwa ujumla


Hasa ukizingatia walimu 98% wametoka katika familia ambazo ni za kimaskini (family induced comfort zone)

NB: Kuna wachache wanatoka katika comfort zone japo ni walimu
 
Uzi ufungwe
 
Nowadays baadhi ya maticha wapo vzr kiuchumi japo weng badooo tia maji tia maji huo ndoo ukwel.... baadhi ya sababu kwa upande wangu..
1. Kuowa au kuolewa mapema mara tu wakiajiriwa..
2. Familia kubwa..
3. Wategemez wengi....
4. Salary bado ndogo sana..
5. Hakuna au wana marupurupu machache sn..
6. Wengi kutoka vjjn wana exposure ndogo..
7. Serikal kuajiri failure miaka flan..zao la kupata walim weng wasio wapambanaj...
8. Etc
 
Sasa kwenye hii nchi sehemu kazi gani upande wa serikali inapesaa mnoo..tukiachana na sekta binafsi na taasisi za umma?
Mwalimu wa degree mshahara wake unaanzia 700k wakati TRA mtu wa degree anaanza na 2M

Sasa hapo unawafananishaje,

Hata hizo taasisi za serikali zinatofautiana mno


Mwalimu wa degree aliajiriwa shuleni ni tofauti na mwalimu wa degree ambaye ataajiriwa NECTA
 
Uzi ufungwe
Mkuu kuna kitu unacho kuhusu walimu sema njia yako unaayotumia mara nyingi huwa si nzuri.


Ila naungana na wewe, ualimu sio kazi ya kuridhika nayo

Kila mwalimu afanye juhudi binafsi ili ahame fani au afanye kitu kingine kinyume na ualimu, yaani kama mtu atafundisha ualimu ubaki kama ni ziada tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…