Maoni, Mawazo & Ushauri kuhusu biashara ya Rasta na Weaving

Maoni, Mawazo & Ushauri kuhusu biashara ya Rasta na Weaving

Habari za muda huu wanaJF?

Natumai hamjambo!

Leo hii nimejitokeza ili kuweza kupata experience ya biashara za nywele bandia (mawigi) na urembo mbalimbali unaohusu wanawake!

Naomba kujua mambo yafuatayo!

1). Ili kuanzisha biashara hii, inatakiwa uwe na mtaji kiasi gani? Binafsi Nina 6mil
2). Vipi faida Yake inakuwa kwa kasi?
3). Ningependa kujua chochote ( miscellaneous) kuhusiana na biashara hii!

Ningependa kujua zaidi kutoka kwa mtu mwenye uzoefu na biashara hii!

KARIBUNI!
 
Huo mtaji si mdogo kwa kuanzia unatosha sana tu. cha kuzingatia hapo ni eneo. Unajua hizi biashara za wamama ukikosea tu eneo utajuta na ukipatia utaula. Pia ujue aina za mawigi/marasta yanayoenda na wakati.
 
Naomba mtu anaefahamu biashara ya nywele za bandia ikiwa ni rasta pamoja na kofia za kawaida wigi, anielekeze ikiwa utachukulia kariakoo bei nish ngap na utauza vipi, lkn pia soko lake liko vip na changamoto zake katika uendeshaji wake ukoje
 
Ok,ila pia unaweza kwenda huko kariakoo, ili usiishie kuambiwa humu,subili wajuvi wa mambo hayo waje
 
Habarin za mihangaiko wadau. Naombeni mwenye ufahamu kuhusu biashara ya rasta/nywelebandia jumla na rejareja kutoka kiwandani napataje. Ninataka kujikita huko
 
Nenda kwenye keyboard settings halafu deactivate autocorrect, inaweza ikaja kukuharibia
 
Nenda kwenye keyboard settings halafu deactivate autocorrect, inaweza ikaja kukuharibia
haiwezekani hapo awaombe mods.......... huwez badili kichwa cha habari chochote hapa jf kama wewe sio mod
 
Habarini wanajamii...Tafadhali naombeni anaejua biashara ya nywele bandia au maarufu Kama Rasta jumla na rejareja . Zinakopatikana jumla niwapi.nanunuaga kariakoo lakini ninauhakika kunamahali kariakoo wanachukua
Natanguliza shukrani
 
Mi nadhan kariakoo wananunua China lakn huwez jua town hapa machimbo mengi
 
Habarini wanajamii...Tafadhali naombeni anaejua biashara ya nywele bandia au maarufu Kama Rasta jumla na rejareja . Zinakopatikana jumla niwapi.nanunuaga kariakoo lakini ninauhakika kunamahali kariakoo wanachukua
Natanguliza shukrani
Unazoziona kariakoo tunanunua China na South Africa...nenda tuu kkoo changanya Wigi kadhaa na weaving baadhi zingine wananunua Uganda hapo hizo Brazilian.. Nunua lolo rangi nyeusi na Purple (Papo),Jialong ndefu na Fupi ndefu chukua rangi 99j,# 1 na colour 4, lovely lady fupi rangi zote..HP ukipata colour zote changanya chache chache,Wigi za watoto na spray carton hata Mbili za Wigi nazo utauza nunua midoli ya kuwekea Wigi kkoo ipo angalia ukubwa wa fremu yako ndio ununue mikubwa na midogo ujanja mwingine utaupata ukiendelea kufanya hiyo biashara..
 
Unaweza kuchagua brand
Kama ni bongo ama nyinginezo
Ukaenda ofisi za usambazaji ukachukua kwa bei ya kiwandani
 
Hbr za kazi wakuu.
Ndugu zangu naombeni ushauri na mnipe utaalam wa hii biashara ya kuuza rasta na mawigi.

Wapi kwa dar_es_salam nitapata mzigo wa jumla na zenye ubora, biashara hii naipenda naona huku nilipo INA soko sna nataka niuze rasta za jumla hz prima, Darling nk, mabanio ya nywele na mawigi ya kushonea na weaving.

Changamoto kubwa cjui chimbo zao wanapozipata kwa bei nafuu, ili namm nikiuza nipate faida kidogo.

Naombeni msaada kwenye hili mtaji wangu ni mill.2.
 
Back
Top Bottom