UJENZI WA BOMBA LA GESI TOKA DAR ES SALAAM -MOMBASA KENYA
#NI JAMBO LENYE KUHITAJI UMAKINI NA UTAFITI ZAIDI KULIKO MAAMUZI YA KWENYE MAJUKWAA YA WANASIASA.
HOJA NI HII:-
sote tunaelewa kuwa Tanzania kwa miaka sita iliyopita ya awamu ya Tano chini ya jemedari mzalendo wetu Hayati Dr JPM,ilipambana kwa Hali na Mali kufufua viwanda na kutengeneza Mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuwezesha ujenzi wa viwanda vipya.
Hilo lilifanyika bayana bila kificho na sote tunajua mikakati iliyofanyika ikiwamo Mpango wa viwanda 100 kwa kila mkoa ambao kwa Asilimia kubwa ulifanikiwa.
Nafasi ya viwanda hivi kibiashara ndani ya soko la Africa Mashariki inakabiliwa na upinzani mkubwa toka kea viwanda vya Kenya ambavyo ni vikongwe,vyenye mitaji mikubwa na uzoefu wa soko la Africa Mashariki.pia uzoefu was uzalishaji.
Kiupekee MADHAIFU waliyonayo wakenya katika viwanda vyao ni Upungufu mkubwa wa Nishati hasa ya Umeme na Gesi ,kitu kinachopelekea Mazingira yao ya uwekezaji kuwa magumu na bidhaa zao kuwa za Bei ghali sokoni.
Tanzania tulikuwa PABAYA Sana katika sekta ya viwanda hasa Baada ya Sera ya ubinafsishaji kupita na kuleta matokeo hasi katika sekta hii.
Viwanda vingi vilikufa,na kusimamisha uzalishaji ,watu wakakosa kazi,bidhaa MADE IN TANZANIA sokoni zikawa adimu kuonekana.tukaishia kuwa walanguzi was bidhaa za Mataifa mengine ikiwamo Kenya ,China na kwingineko Duniani.
Serikali ya JPM ikaturudisha kwenye tracks na kutuwezesha kufufua brand yetu "MADE IN TANZANIA" kwa viwanda vingi kuanzishwa na vingine kufufuliwa
Pia JPM akawekeza katika Ujenzi wa Nyerere Dam,na Usambazaji wa Gesi viwandani ili kuwezesha uzalishaji nafuu wenye Tina utakaopelekea bidhaa zetu kuwa za Bei nafuu sokoni.
Suala ambalo wakenya walijua viwanda vyao,na bidhaa zao zinakwenda kupoteza soko.na kushindwa
#Leo hii ile kete ya ushindi ya Nishati ya Gesi tunaipeleka Kenya .itawafanya production cost ya bidhaa zao kuwa nafuu.na bidhaa toka kwenye viwanda vyetu vichanga zitashindwa kushindana na bidhaa za viwanda vyenye uzoefu sokoni toka Kenya.
Ila kitakachotupa ugumu huu ni Gesi yetu na umeme wetu endapo tutaupeleka huko na wao wakautumia kuzalisha bidhaa kwa gharama ya chini.
Suala Hilo litaua viwanda tunavyoanzisha.na kupoteza mwelekeo was matokeo chanya tuliyoyaona katika miaka hii sita iliyopita.
#Narejea wito wangu.suala la Gesi kupelekwa Kenya lifanyiwe Tafiti za faida na hasara zake .na isiwe political agenda ya viongozi wachache wa kisiasa.
Suala hili lihusishe wataalamu wa kitaifa na Maoni ya wadau .
"Sote tutajenga Tanzania [emoji1241] imara"