Haya ni maoni yangu binafsi kwako muheshimiwa Rais. Anza na mambo haya matano kwanza.
1. Ajira kwa vijana. Toa ajira za kutosha huku mitaani maelfu kama sio malaki ya vijana hawana ajira.
2. Lipa mafao ya wazee waliostaafu kuanzia 2017 hadi leo kuna wazee wanamaliza soli za viatu bila kupata mafao yao.
3. Weka mazingira borana rafiki ya uwekezaji na ufanyaji biashara. Kaa na wafanyabiashara,TRA, TCCIA, CTI, BRELA, TIC, OSHA, n.k muwekane sawa. Sekta binafsi italeta kodi pamoja na ajira kwa mamilioni ya watu.
4. Serikali ikusanye kodi biashara iyaachie makampuni binafsi. Pia hela zisifichwe benki kuu zikae kwenye mabenki ya biashara ili watu waweze kukopa na mzunguko wa fedha uwe mkubwa.
5. Nidhamu ya watumishi wa umma iwe ya kiwango cha juu mfano Polisi, Manesi, Masijala, wakuu wa idara n.k ni kitu cha kawaida watumishi wa serikali kudai rushwa au kukataa kutoa huduma kwa wananchi bila sababu za msingi. Ukienda maofisini utaambiwa huduma haipo bosi yupo kwenye kikao, kasafiri au ameenda kunywa chai. Utasubiri huduma kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9 mchana kisha unaambiwa njoo kesho.