Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

1. Mama ahakikishe watu wanaendelea kufanya kazi kama inavyotakiwa wakiwa watumishi wa umma. Hii ya kwenda kwenye ofisi za umma bila kuhudumiwa sababu watumishi hawapo sio sahihi. Tunaposikia mfano foleni zimerudi bandarini sababu hakuna vibali vinavyotoka nayo haijakaa vizuri.
2. Kuhudumia kwenye level yake sio rahisi kumfurahisha kila mtu. Afanye kazi kwa weledi na amuombe Mwenyezi Mungu amoe hekima ili tusonge mbele. Tanzania ni yetu sote
 
Haya ni maoni yangu binafsi kwako muheshimiwa Rais. Anza na mambo haya matano kwanza.

1. Ajira kwa vijana. Toa ajira za kutosha huku mitaani maelfu kama sio malaki ya vijana hawana ajira.

2. Lipa mafao ya wazee waliostaafu kuanzia 2017 hadi leo kuna wazee wanamaliza soli za viatu bila kupata mafao yao.

3. Weka mazingira borana rafiki ya uwekezaji na ufanyaji biashara. Kaa na wafanyabiashara,TRA, TCCIA, CTI, BRELA, TIC, OSHA, n.k muwekane sawa. Sekta binafsi italeta kodi pamoja na ajira kwa mamilioni ya watu.

4. Serikali ikusanye kodi biashara iyaachie makampuni binafsi. Pia hela zisifichwe benki kuu zikae kwenye mabenki ya biashara ili watu waweze kukopa na mzunguko wa fedha uwe mkubwa.

5. Nidhamu ya watumishi wa umma iwe ya kiwango cha juu mfano Polisi, Manesi, Masijala, wakuu wa idara n.k ni kitu cha kawaida watumishi wa serikali kudai rushwa au kukataa kutoa huduma kwa wananchi bila sababu za msingi. Ukienda maofisini utaambiwa huduma haipo bosi yupo kwenye kikao, kasafiri au ameenda kunywa chai. Utasubiri huduma kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9 mchana kisha unaambiwa njoo kesho.
 
4.Serikali ikusanye kodi biashara iyaachie makampuni binafsi. Pia hela zisifichwe benki kuu zikae kwenye mabenki ya biashara ili watu waweze kukopa na mzunguko wa fedha uwe mkubwa.
Katika yote uliyoweka hapo, hii ndiyo dhaifu zaidi kwa upande wako.

Kwa nini usihimize serikali iyadhibiti/ iyaboreshe mashirika hayo yafanye kazi kwa ufanisi zaidi. Kwani kuna kosa gani kwa serikali kuendesha mashirika, au kwa vile tumekaririr tu "serikali haifanyi biashara"?

Kwanza kukusanya kodi kwenyewe ni biashara, mbona unaihimiza serikali ifanye kazi hiyo?
 
Viongozi wa Tanzania wana mambo ya kushangaza sana.Nakumbuka huu mzaha uliondoka na watu lakini bado umerudiwa tena!

Imagine viongozi badala ya kuweka mikakati ya muda mrefu (Long-run strategies)ya kupambana na kirusi cha Corona ili kukizuia kisifanye mutations halafu kiwe hatari kama kile cha India, badala yake wanafanya mizahaa kama hii![emoji1][emoji1][emoji1]

Mtu hujavaa hata barakoa halafu unajifanya kuwa unajali sana juu ya Corona kwa kufanya salaam ya kudance eti unajizuia kuambukizwa Corona!Hivi kama Taifa tuna tatizo gani?Tulikosea wapi?Tuna laana gani?

Gettyimages.jpg
987654-1.jpg
 
Viongozi wa Tanzania wana mambo ya kushangaza sana.Nakumbuka huu mzaha uliondoka na watu lakini bado umerudiwa tena!

Imagine viongozi badala ya kuweka mikakati ya muda mrefu (Long-run strategies)ya kupambana na kirusi cha Corona ili kukizuia kisifanye mutations halafu kiwe hatari kama kile cha India, badala yake wanafanya mizahaa kama hii![emoji1][emoji1][emoji1]

Hivi kama Taifa tuna tatizo gani?Tulikosea wapi?Tuna laana?View attachment 1781239View attachment 1781240
Neno laana umelitumia ndivyo sivyo....anyway uonavyo machoni pako ndivyo ulivyo rohoni mwako.
 
Back
Top Bottom