Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mia kama mia yaani....!

Uhuru wa habari ruksa!

Uhuru wa kupanda gharama za maisha ruksa!

Uhuru wa kupanda nishati za mafuta ruksa!

Uhuru wa watuhumiwa na makosa mbalimbali ruksa!

Uhuru wa kupunguza gharama za usajili wa vyombo vya habari ikiwamo SU Tv ya ukoo wa kina Suluhu ruksa!

Uhuru wa wanawake wengi kuteuliwa katika nafasi yeyote ile hata kama hana uwezo kwayo ruksa!

Yaani ni Mia kama mia yaani!

Kongole mama mia 🥶

Nilisahau,Ngara diesel ni 2400 na petrol ni 2630.

Aramusiki!
 
Mhe rais SSH una nafasi kubwa sana ya kuliponya taifa hili kutoka kwenye majeraha aliuoyaacha mwendazake.

MOJA. Mwendazake aliikanyaga katiba kwa kiwango cha kutisha. WEWE USIFANYE HIVYO.
Toa Uhuru kwa vyama vya siasa na serikali yako haita athirika kwa chochote. Kwasabb sughuli za kuinua uchumi wa nchi na shughuli za vyama vya siasa wala havigombani.

MBILI. Mwendazake aliwaonea watu. WEWE USIFANYE HIVYO.
Na tunaona ushaonesha mwanzo mzuri katika hili.

TATU. Mwendazake alipuuza sana sauti na vilio vya wananchi. WEWE USIFANYE HIVO.
Wasikilize usipatwe na kiburi cha madaraka. Wanataka katiba wananchi wako. Cha kufanya tengeneza utaratibu katiba mpya ipatikane.

Ni mimi Sexless , nampa ushauri mheshimiwa rais SSH.
 
Hata asipotoa katiba,aache mikutano watu watachoka wenyewe kuongea
 
Naona tayari papa na nyangumi wamesha ishika hatamu...🙆
 
Aaangalie sana swala la uchumi wa watu wa chini, bajeti imesomwa vizur kwa ajil ya kukuza uchumi wetu ilaa kilichofanyika kapunguzaa kodi ha beer akapandisha mafuta, kupanda kwa mafuta kila kitu vitapanda bei maana 80% ya vitu lazima vitumie usafirishaj... Aaangalie hilo
 
Fao la kujitoa sio in

Fao la kujitoa sio interest ya mtu mmoja ni suala la kitaifa na kisera zaidi. Vijana wengi walioajiliwa sekta binafsi ni wahanga wa hili na wanapomaliza mikataba yao ni vyema wakapewa pesa zao ili wakajiajili kuimarisha uchumi...
Huyu jamaa aliyenipinga hajielewi,ama haelewi maana ya fao la kujitoa au ni mbumbumbu asiyejua maana ya interests .Fao la kujitoa linakuwaje interest binafs?
 
Salaam Mh. Rais

Pole na jukumu la kuiongoza nchi,tunakuombea kwa Mungu akupe Afya njema na Hekima kuiongoza nchi yetu pendwa TANZANIA.

Uliagiza kufutwa VRF kwenye madeni ya wadaiwa wa HESLB. Naomba sana sheria hiyo ifute na hicho kitu kisisomeke KABISA kwenye statememt,libaki deni halisi wahusika walilipe.

Nakuomba sana sana,kwenye hilo washauri wako wasikuingize "chaka".

Uliahidi hutaki fedha za dhuluma, simamia kwenye hilo na MUNGU atasimama na wewe!

Namshukuru Mungu nimepanda Daraja, na nimerekebishiwa tayari.

Narudia tena!Mungu akujaalie Afya na Hekima Tele.

Kuhusu wapambe nuksi, kuwa nao makini. Wapige chini mara moja wasikuzoe, unaenda vizuri.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano.
 
Mheshimiwa Rais aliangalie swala la KATIBA Mpya kwa staha sana na maamuzi yake yawekwe kwenye maslahi mapana zaidi ya nchi kuliko chama chake...... [emoji3070] [emoji3070] [emoji3070]
 
Back
Top Bottom