Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Magufuli alisema atapandisha salary siku anatoka madarakani na hapa tuna assume kama angekua mkweli maana alikua ana historia ya kusema uongo.
Kwenye taarifa ya uelekeo wa bajeti ya mwaka huu iliyosomwa bungeni mwezi Machi kama sikosei, wakati bado JPM akiwa ni Rais, Waziri wa Fedha wa wakati huo (Philipo Mpango) aligusia jambo hili! Ya kwamba kuna bilioni kadhaa zitatengwa mwaka huu kwa ajili ya kupandisha vyeo (madaraja) watumishi wa umma.

Hivyo siamini kama haya yote yameletwa na Rais Mpya ndani ya huu muda mfupi. Labda ile ishu ya kuondoa zile riba za Bodi ya Mikopo, nakubali ni huyu mama ndiye aliyezitoa.
 
Hata misingi ya uchumi imara na kuhakikisha serikali inakuwa na hela za kulipa ni jitihada za miaka mitano za utawala wa JPM kupitia nidhamu ya hali ya juu kwenye mapato na matumizi ya pesa za umma.
 
Kwa niaba ya watumishi wote tunakushukuru sana. Ni miaka name sasa watumishi waliishi bila matumaini. Tunaomba pia mama na wenzetu ambao hawajapata ajira nao uwafikirie hata kwa awamu awamu hapo huwezi ajiri wote. Watu wote hawawezi kujiajiri mana mitaji ni tatizo.

Mungu akubariki sana.
Kwa kilichowatokea kwa miaka hiyo yote, iwe fundisho kwenu pia. Tukikosea kuchagua viongozi au tujiendekeza unafiki wa kuwapamba viongozo hata wanapokosea, majuto hurudi kwetu.

Mimi naamini matatizo makubwa yalikuwa kwa wananchi kuliko kwa Magufuli. Watu wengi wamejaa ujinga, unafika, hila, uwongo na tamaa. Hawa ndiyo usiku na mchana walimsifia marehemu na kujipendekeza, huku marehemu akibomoa Taifa. Leo wanamgeuka marehemi kwa sababu hayupo madarakani.

Siasa na sifa za unafiki, zinaangamiza Taifa.
 
Mkuu, pongezi za nini sasa! Hata magufuli angebaki hai mpaka leo, bado angetupandisha tu. Maana haki ya mtu inacheleweshwa tu! Ila mwisho wa siku ni lazima ipatikane.

By the way, siyo watumishi wote wenye sifa wamepandishwa mwezi huu. Sasa huoni haujatutendea haki sisi watumishi wenzako ambao tumepokea mshahara ule ule wa miaka yote!! Maana umesema watumishi wote tunampongeza!!
Asingeweza.Alikuwa mvuta bangi.😝😝😝😝
 
Kwanza mimi sio mfuasi wa chama chako Cha CCM na ninaomba usiku na mchana chama chako kianguke.

Lakini hii hainifanyi nisipongeze pale unapofanya vizuri, kwanza shukrani kwa mazuri yote unayofanya japo najua ni wajibu wako.

Kuna jambo naona unaanza kuwa kama mwendazake, kila siku mbele ya camera live kwenye tukio flani.

Kila siku kukiwa na tukio live napo inachosha na inashangaza. Kila siku ni hafla na matukio yako live.

Wiki iliyoisha wiki nzima ulikuwa live na matukio wiki hii imeanza umeanza na tukio la leo live.

FANYA YOTE ILA TAREHE MOJA TUNAOMBA UTU-SUPPORT KATIBA MPYA.

#katiba mpya ni lazima#
 
Mwongo wewe mbona jana hakuwa live!

Halafu huyu mumzoee tu tunae eti mpaka 2035.

Mwacheni Madam afanye yake anafunika AWAMU zote.

Huu ni ufagio eti
 
FANYA YOTE ILA TAREHE MOJA TUNAOMBA UTU-SUPPORT KATIBA MPYA.
Yote kwa yote ameruhusu. Na ndiyo maana hiyo tarehe moja inawezekana hata kukusanyika.

Ingekuwa enzi za mwendazake. Ungesikia kamanda Muroto anatoa kauli za kipigo cha mbwa koko, na anakusanya ving'ora na polisi anapitisha barabarani.
 
Hivi ninyi wapumbafu mnatakia nini mama yetu. Hamkosi Sasa Babu mnagubu Sana. Muache mama achape kazi
 
Yote kwa yote ameruhusu. Na ndiyo maana hiyo tarehe moja inawezekana hata kukusanyika.

Ingekuwa enzi za mwendazake. Ungesikia kamanda Muroto anatoa kauli za kipigo cha mbwa koko, na anakusanya ving'ora na polisi anapitisha barabarani.
Kwani zamani mlikuwa hamkusanyiki? Mbona 2019 mlifanya chaguzi zenu za ndani nzima?
 
Mwongo wewe mbona jana hakuwa live!!!
Halafu huyu mumzoee tu tunae eti mpaka 2035
Mwacheni Madam afanye yake anafunika AWAMU zote
Huu ni ufagio eti
Jana ilikuwa jpili
2035? Na sisi tupo tu tunaangalia anavyovunja katiba?
Subiri moto wa tarehe 1 kama CCM mtakuwa na hamu ya kuendelea kutawala
 
Yote kwa yote ameruhusu. Na ndiyo maana hiyo tarehe moja inawezekana hata kukusanyika.

Ingekuwa enzi za mwendazake. Ungesikia kamanda Muroto anatoa kauli za kipigo cha mbwa koko, na anakusanya ving'ora na polisi anapitisha barabarani.
Safi, katiba mpya ni lazima
Katiba sio hisani
 
Back
Top Bottom