Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Kwenye taarifa ya uelekeo wa bajeti ya mwaka huu iliyosomwa bungeni mwezi Machi kama sikosei, wakati bado JPM akiwa ni Rais, Waziri wa Fedha wa wakati huo (Philipo Mpango) aligusia jambo hili! Ya kwamba kuna bilioni kadhaa zitatengwa mwaka huu kwa ajili ya kupandisha vyeo (madaraja) watumishi wa umma.Magufuli alisema atapandisha salary siku anatoka madarakani na hapa tuna assume kama angekua mkweli maana alikua ana historia ya kusema uongo.
Hivyo siamini kama haya yote yameletwa na Rais Mpya ndani ya huu muda mfupi. Labda ile ishu ya kuondoa zile riba za Bodi ya Mikopo, nakubali ni huyu mama ndiye aliyezitoa.