Hakuna mtu anayependa kulipa kodi, nadhani wewe mwenyewe umeshuhudia lawama unazopokea kwa sasa.
Iko hivi, hakuna mfanyabiashara duniani, anayetoa kodi kwa hirai na furaha, ni kwa sababu tu wanabanwa.
Wanasoka Nguli duniani, matajiri wanakwepa kodi licha ya utajiri wanaomiliki.
Sembuse watanzania?
Mtangulizi wako baada ya kuwabana watu watoe kodi, wakakimbia nchi, nakushutumu mazingira mabaya ya biashara nchini. Mwenzako, akakomaa hivyo hivyo kubana, akapata pesa ya kupeleka maji sehemu zilizosahaurika kama Tabora.
Leo hii waliokimbia kutoa kodi, wanatuambia rais haleti maendeleo kinacholeta ni kodi, kodi ipi kama walikimbia kulipa kodi.
Mwisho, usipokaza utaendelea kuwanyonya maskini (Ambao ni 90%) ya watanzania. Na kuacha wenye kipato kikubwa wakitesa.