Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kipi kizuri kuwa na wawekezaji au kuwafukuza
 
Hakuna kipindi tulichokaa bila Rais Tanzania. Na hakuna kipindi ambacho tulikuwa na Rais aliyesukuma maendeleo mbele kama Rais wa awamu ya tano Rais Magufuli. Katika awamu ya tano Tanzania tuliingia kwenye uchumi wa kati.

Kwenye awamu ya tano miradi iliyokuwa imeshindikana tangu enzi za baba wa Taifa ilifufuka na kuendelea kwa kasi. Kwa mfano mradi wa ujenzi wa makao makuu dodoma ulikuwa umekufa kabisa wala hakuna aliyekuwa analiwaza hilo kuwa linawezekana.

Lakini Rais Magufuli alifufua mradi ule na kufanikiwa kuhamishia makao makuu ya nchi dodoma. Mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere (Stiglers George) ni mradi mkubwa sana wa kufua umeme wa maji. Mradi huu ni wa ukombozi wa nchi dhidi ya mabeberu wanaotuibia pesa kupitia miradi ya umeme tunaolipia kwa capacity charge, hata kama hatujatumia umeme.

Ukweli ni kwamba Magufuli aliwashika pabaya mafisadi na mabeberu hadi kesho hawana hamu naye!! Ukiona mafisadi na mabeb eru wameanza kuichangamkia nchi yetu kwa kisingizio cha "uwekezaji" ujue wamehisi shamba la bibi limerudi!! si dalili njema hata kidogo!!! Watukome!!!
 
Wewe nina mashaka, aidha ulifyatuliwa kwa kuwa na vyeti feki au ulikuwa miongoni wa wafanyakazi hewa! Ikitokea kimojawapo kati ya hivyo lazima utafoka kama ulivyoandika!
 
Miradi huwa inaendeshwa through ppp siyo uzoa pesa zote za serikali halafu unazuia Mambo mengine yasiendelee mfano ajira nk.

Ndiyo maana akaamua kuanza kuua kila anayemkosoa ili tu asikosolewa kwa hayo maamuzi ya kijinga. Hata marekani hawafanyi miradi mikubwa hiyo at par. Ndiyo maana kils kitu lilikuwa mfano masoko ya mazao Kama mbaazi na korofo na ndiyo maana wakaazi wa huo walikasirika wakataka kumuuulia jukwaani maafisa usalama wakamshusha fasta.

Na ndo maana hata hakuwahi kuongeza mishahara ya wafanyakazi licha ya sheria kutaka hivyo. Kifupi alijifanya yuko juu ya Sheria na mungu pia. Marekani haijawahi kununua ndege zake kw cash Mana Ni kuua raia kwa njaa na kuwatesa Kama ambacho katesa greladuates na raia wote five years. Sasa hivi ni ahueni
 
Ajira Sasa hivi kila Kona zimejaa kiasi Cha waajiri Sasa hivi Wana adabu maana ukizingua tu mtu anakuachia li ajira lako na kuhamia mwingine tofatu na kipindi Cha yule shetani ambacho waajiri walikuwa miungo maana ajira zilikuwa chache na hizo chache zinazidi kuisha machinga tu ndo wanafurika mtaani
 
Tanzania imepoteza mwelekeo ndani ya muda mfupi wa awamu ya sita.Laiti kama awamu ya tano ingeendelea

1: Uchumi wa Tanzania ungekuwa wa kati daraja la juu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Tanzania imeporomoka kutoka nafasi yake ya 8 kati ya nchi 10 zenye uchumi bora Africa mpaka nje ya top 10 na kuzidiwa na vinchi kama Ghana na Angola

2: Nidhamu na uwajibikaji kazini ungekuwepo.Leo hii tunashuhudia wananchi wakihoji kuhusu hali ya umeme nchini pasipokuwa na majibu au majibu yenye uwalakini. Lakini pamoja na hayo bado viongozi wamebaki wakiwa maofisini pasipo kuwajibika kwa namna yoyote.

3: Kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa ikiifanya juhudi kubwa kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa na ya kimkakati. Licha ya kwamba tangu Rais S.S.H aingie madarakani hakuna mradi wowote wa kimkakati ulioanzishwa bali pia hata ile miradi iliyokuwa ikiendelea imekuwa ikisuasua

4: Umeme usingekuwa wa mgao.Tangu Rais S.S.H aingie madarakani hali ya upatikanaji wa umeme nchini imekuwa mbaya sana.Hali hii imepelekea kurejea kwa mgao wa umeme ambao watanzania wengi walishausahau tangu miaka kadhaa iliyopita.Hali inayopelekea kuwatesa wananchi hususan wale wanaotegemea umeme kujipatia vipato katika shughuli zao za kila siku.

5; Hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ya kusuasua.Kwa miezi kadhaa hususan katika jiji la Dar es salaam pamekuwa na mgao wa maji.Hali iliyopelekea kukosekana kwa maji kwa muda mrefu katika maeneo mengi.Hali ambayo hakuwahi kushuhudiwa hapo awali.

6: Tozo zisizokuwa na tija na zilizoua uchumi wa wengi.Serikali ya awamu ya sita imedhulumu na kunyang'anya kwa nguvu fedha za wananchi kwa kigezo cha tozo katika miamala ya simu.Mama mjane anapomtumia mgonjwa wake hospitali kwa ajili ya matibabu anakatwa fedha ambayo kimsingi haikuwa ya biashara. Kwa mujibu wa report kutoka Vodacom hivi karibuni miamala ya simu imepungua kwa asilimia zaidi ya 30!.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo kwa uchumi wa nchi.Ni sawa na kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuhamishia Kulia.

7: Kupanda kwa bei ya Mbolea.Mara tu baada ya awamu ya sita kuingia madarakani bei ya mbolea ilipanda karibu mara mbili ya bei ya awali.Hii ni imepelekea uchumi wa watanzania wengi ambao ni masikini na wanategemea kilimo kudhoofika.

8; Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia
9; Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol
10; Kupanda kwa bei ya bidhaa za ujenzi kama cement,Nondo n.k
11; Teuzi za viongozi wasiokuwa na weledi kwa kigezo cha favour/Undugu/Kujuana (Mf. Riziwani Kikwete,Nape Nauye n.k) Tanzania ina vijana wasomi na wenye upeo mpana wa kifikra. Lakini cha kushangaza teuzi zimekuwa hazina matumaini ta kuipeleka Tanzania kule tunapotarajia.

12: Ukosefu wa uzalendo na ubadhirifu miongoni mwa watumishi wa umma.Siku si nyingi tumeshuhudia kiongozi mkuu wa serikali akiwaasa watumishi wake wale kwa urefu wa kamba zao.Hii inaashiria kwamba hata kiongozi mkuu anashiriki katika ulaji huo.Hali hii ni hatari kwa rasilimali za nchi.

13; Wananchi hususan wa hali ya chini kukosa nafasi katika nchi yao.Siku si nyingi tumeshuhudia wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakinyanyaswa kwa kuhamishiwa katika maeneo yasiyokuwa tija kwao.Vuta nikuvute hii imepelekea hali ya unyonge na sintofahamu miongoni mwao na kupelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa watanzania

14; Mikopo isiyokuwa na tija kwa taifa.Tangu Tanzania ipate uhuru viongozi wake wote walisisitiza kufanya mambo yetu kwa fedha zetu wenyewe bila kutegemea wahisani. Tanzania imebarikiwa rasilimali za kila aina.Mito,Maziwa,Bahari,Madini kama Tanzanite,Mbuga za wanyama,Gesi n.k Inashangaza Sana kuona kiongozi badala ya kusisitiza au kubuni namna ya kuzitumia rasilimali hizi ziweze kuwa na tija kwa watanzania,Badala yake tumekuwa tukijivunia mikopo!

15 ; Kuongezeka kwa gharama za uunganishaji umeme kutoka 27,000 iliyokuwepo mpaka zaidi ya 300,000 ya hivi sasa.Hali hii imepunguza mno kasi ya usambaaji wa umeme

16 ; Muingiliano baina ya mihimili kwa kigezo cha uchama.Inasikitisha kuona kiongozi wa mhimili mmoja anakosa uwezo wa kuikosoa na kuurekebisha mhimili mwingine kwa kuhofia kibarua chake.hili tumelishuhudia baada ya kuona spika wa bunge la JMT kujiuzulu baada ya kuhoji kuhusu mikopo na tozo.

17 ; Safari zisizokuwa na tija wala umuhimu kwa taifa.Tumeshuhudia safari nyingi mno za nje ya nchi,Safari hizi zimekuwa zikiigharimu nchi fedha nyingi.Safari za vikao visivyokuwa na tija kama mkutano wa kujadili athari za gesi ya ukaa sidhani kama ina tija hususan kwa nchi ambazo bado uchumi wake ni mdogo

18 ; Kukosekana uhuru na ukandamizaji wa demokrasia. Tunaweza kusema kwamba pia hata katika awamu zilizopita hili lilikuwepo, Lakini hili la sasa limekuja kwa namna tofauti.Wakati mwingine baba anaweza kumpa mtoto adhabu ya kulima shamba,Mtoto akalia na kulaumu sana,Lakini shamba hilohilo baadaye likaleta chakula mezani wote wakala na kufurahia. Ila tofauti iliyopo sasa,Hakuna chakula kinachokuja mezani!

19 ; Kushughulikia zaidi mambo yasiyokuwa na tija kwa wananchi kuliko yale yenye umuhimu na tija kwa watanzania. Imekuwa jambo la kawaida kwa awamu hii kujihusisha zaidi na makongamano,Semina elekezi,Birthday Party pamoja na hafla mbali mbali badala ya kujikita katika kufufua na kubuni miradi ya kimaendeleo itakayosaidia kuwapunguzia wananchi mzigo wa umasikini na kuinua uchumi.Hafla ya machifu na watemi si muhimu kama hafla ya utiaji saini mradi wa uchimbaji na usambazaji wa gesi ya Mtwara!

20 ; Kukosekana ajira. Ubunifu na uibuaji wa miradi mipya si tu umekuwa na tija kiuchumi Bali umekuwa ukiajiri vijana wengi.Kukosekana kwa ubunifu na sera mbovu za serikali zimesababisha kukoseka kwa ajira miongoni mwa vijana wengi

21 ; Kuongezeka matukio ya uhalifu.
Mara tu baada ya awamu ya sita kushika hatamu sote tumeshuhudia jinsi wimbi la uhalifu lilivyoongezeka.Sio tu matukio ya wizi na ujambazi bali mpaka uchomaji wa masoko kama Kariakoo, mchikichini n.k wizi mauaji na utekaji nyara vimeongezeka kwa kasi mno. Hii inaonyesha udhaifu katika usimamizi wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama

22 ; Kuongezeka gharama za simu
Kutokana na kodi za miamala Kuongezeka kampuni za simu zimejikuta zikilazimika kupandisha gharama za muda wa maongezi na huduma zinginezo za simu kama vile huduma za vifurushi ili kuweza kubalance gharama za uendeshaji. Hali hii imesababisha mzigo mzito kwa wananchi hasa ukizingatia mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika shughuli zao za kila siku

Hakika ni mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanyika kinyume na matarajio ya watanzania wengi ambao waliwaamini viongozi wao na kuwaweka madarakani huku wakiwa na matumaini makubwa ya kuondokewa na maradhi, ujinga na umasikini ambao ndio maadui wakuu wa taifa kama ilivyobainishwa na Mwl Nyerere badala yake watanzania hao ambao wengi ni masikini na wameteseka kwa umasikini kiasi cha kusahau tarehe zao za kuzaliwa huku wakishuhudia wale waliowachagua wakikata keki ikulu!

Wacha kazi iendelee!
 
Tanzania haijawi kuingia uchumi wa Kati zile zilikuwa propaganda na fix ndo Mana chombo Cha habari kikihojo lilikuwa kinafungiwa.

Ki ufupi nchi ilie deshwa gizani kwa hiyo alikuwa anaweza kuwadanganya kivyovyote. Kam alivyotupiga uongo eti Kuna mtu anapiga hela mil 7 kwa sekunde.
 
Tanzania haijawahi kosa Rais. Magu alikuwa Rais aliyetaka nchi ijitegemee.

Sema kwenye kujenga mahusiano na mataifa ya nje na sekta binafsi mambo hayakuwa mazuri....ingawa huku ndiko rasilimali za nchi zinapopigwa!

Natamani kuiona Africa na Tanzania iliyosimama yenyewe bila kutegemea msaada wa nje.

Msije dhani kuna nchi yeyote ya magharibi na Asia yote inapenda kuona Africa imesimama...
 
Nyani haoni kundule ujue. Wengine wanaliona na ushahidi ni huu

 
Demokrasi imepanuka we mbumbumbu. Wawekezaji wanapenda kuwekeza sehemu yenye demokrasia siyo pale ambapo mkuu wa wilaya au mkoa akiamua anakukoromea au kukusweka ndani tu Kama ilivyokuwa kwa akina sabaya na makonda.
Rwanda wawekezaji wamejaa, kuna demokrasia? Uchumi wa Rwanda unakua kwa spidi kubwa kuna demokrasia? Wapumbavu kama wewe ndio hua mnadanganywa kwamba kukiwa na demokrasia ndio wawekezaji wanakuja.

Misri haijawahi kua na demokrasia lakini unajua FDI inayomiminika pale kila mwaka? Tanzania na demokrasia yenu ya chief hagaya mnaifikia Misri?

Hii nchi imejaa mataahira.
 
Wewe nina mashaka, aidha ulifyatuliwa kwa kuwa na vyeti feki au ulikuwa miongoni wa wafanyakazi hewa! Ikitokea kimojawapo kati ya hivyo lazima utafoka kama ulivyoandika!
Hakuna aliyewahi kuwa na vyeti hewa ile ilikuwa mbinu ya kupunguza wafanyakazi baada ya uchumi kuwa ICU
 
Japo nilipenda mno mno mno mno rais kutoka kanda ya ziwa, lakinii marais waisilamu nitaendelea kuwakubali. Hususani uyu mama anafaiti sana bandugu

Haya mtoa mada mwenzanko huyu kaeni chini mjadiliane ujinga maana vichwa vyenu wote vina funza
 
Kwa hiyo anavyoua watu Kama nzige kagame ndo furaha yako.
 
Kwa hiyo anavyoua watu Kama nzige kagame ndo furaha yako.
Nimejibu hija yangu ya hovyo hovyo uliyosema eti wawekezaji wanakuja sehemu ina demokrasia, nimekuuliza Rwanda ina demokrasia, mbona wawekezaji wamejaa Rwanda? Jibu hilo swali.
 
Bila shaka elimu yako itakuwa ndogo sana hata uwezo wako kuzitambua taasisi kama worldbank au WEF au walau hata kutumia google kwako ni mtihani. Nitakuwa ninapoteza muda wangu kukujibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…