Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Leo NI siku ya sikukuu, kusema kweli mama ameupiga mwingi for two years now. Tunapaswa kumpongeza apate hari yakusonga mbele zaidi.

Natoa Uzi huu Leo ambayo ni SIKU ya mapumziko kwake tuweze kumpongeza nakushauri abane wapi na alegeze wapi.

Naamini Leo ana muda karibuni tumsalimie mama
 
Mama ashughulike na ufisadi,Hata hao wanaotupa misaada wanachukizwa sana naubadhirifu wa Fedha wa nazotupa.hawatatupa tena kwa mwendo huu
 
Tumeshaona dhamira ya dhati aliyonayo Mh. Rais kwa kipindi hiki kifupi, Ndugu watanzania, zimwi likujualo...........
"Ni kuomba na kumwombea Mh. Rais Samia, Mungu azidi kumpa neema ya kututumikia zaidi mpaka 2030" AMENI 🙏🏼, INSHALLAH 🙏🏼
 
🚮
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia elfu moja, Samia tumeshamjua tusitafute mwngne tusiyemjua hatujui atakuja na Nini.. wenzetu hapo jirani wamebadili rais tu mpaka Mishahara ya watumishi wanakosa
 
Hili la katiba ndio Mtihani wa kupiima uwezo wa Mama kisiasa na Kidhamira.
NIA ANAYO,
SABABU ANAYO,
NADHANI NA UWEZO ANAO.
LAKNI ASIRUHUSU WATU WA DINI KUMTEMBELEA IKULU DAKKA ZA MWISHO,
WAKITAKA WAKAONANE NA KAMATI PENDEKEZWA YA MCHAKATO WA KATIBA (PINDA COMETEE)
KAZI IENDELEE
 
Maono ni picha inayojengeka ndani ya mtu juu ya jambo anayopaswa kufanya au kutenda na matokeo ya jambo hilo,hivyo kiongozi wa nchi anakuwa na maono pale anapokuwa na uwezo wa kuona picha ya hatma kwa ajili ya maisha ya anaowaongoza na picha ya nchi kwa ujumla itakavyokuwa hapo baadaye.

Kiongozi mwenye maono anabuni mbinu,mikakati,mawazo,sera,mipango au miradi mbalimbali ambayo ina matokeo makubwa na hivyo kuliwezesha taifa lake kupiga hatua kubwa za maendeleo.

Kwakuwa Dr Samia Suluhu Hassan ana maono chanya amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika kuwatia moyo na kuwahamasisha wateule wake na wananchi kwa ujumla katika kufikia maono hayo ya pamoja na kikubwa zaidi anajali ndoto,karama na vipawa vyao na ndio maana amekuwa akipokea ushauri na maono yao na kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko.

Dr SSH ni kiongozi anayeongoza kwa mfano na ana uwezo wa kujenga uhusiano thabiti na wafuasi wake kwa kuonyesha huruma na kujali ustawi wao na pia ameweza kukuza hali ya kuaminiana na kuheshimiana na hii inawafanya wafuasi wake kujisikia salama kuungwa nkono na kuchukua umiliki.

Dr Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mtumishi ambaye ametanguliza mahitaji ya Watanzania kuliko yake na hana muda wa kutafuta faida ya kibinafsi kwa kutumia taasisi ya urais.

Yafuatayo ni baadhi ya mipango na mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi wa Dr Samia Suluhu Hassan.

1.Bima ya afya kwa wote
Hii itawezesha wananchi wengi kuwa katika mfumo wa Bima ya afya na hivyo kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya pindi mwananchi anapohitaji. Mkakati huu utaboresha sekta ya afya kwani watoa huduma kupitia Bima ya afya hupunguza mlolongo mrefu wa utoaji wa huduma kwa mteja kuanzia anapoingia getini hadi anapotoka ili kuokoa muda wa mteja kwa kupata huduma kwa wakati.

Bima ya afya ni muhimu katika Dunia ya sasa na ndio maana katika nchi zote zilizoendelea wananchi wengi wana Bima ya afya.

2 Elimu bila ada mpaka kidato cha 5 na 6
wakati wa bajeti ya mwaka jana serikali iliamua kuwa Elimu ya kidato cha tano na sita itolewe bure Ili kupunguza adha wanazokumbana nazo wanafunzi hao wa kidato cha 5 na 6.

Hivyo elimu bila ada itakuwa ni kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita. Pia serikali inaangaliwa namna ya kusaidia vyuo vya kati (colleges) kama uwezo wa fedha utaruhusu.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi 10,339,350,000. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza wizara inapendekeza kufuta ADA kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita.

Serikali itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa.waziri wa fedha alitamka maneno hayo wakati akisoma bajeti ya mwaka jana Bungeni.

3 kupitia mpango wa Building Better Tomorrow serikali imeanzisha mfuko wa dhamana kwa vijana na huduma za mikopo nafuu chini ya mfuko wa pembejeo ili kuwavutia kushiriki katika ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo

Katika awamu ya kwanza vijana 812 wanapatiwa mafunzo kwa miezi minne bure kisha wanapatiwa mashamba makubwa ambayo tayari yamewekewa mifumo ya umwagiliaji.

kwa mpango huu Dr SSH anatekeleza ndoto ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye katika miaka ya 70 alitaka kuifanya Tanzania kuwa ghala la chakula ili kulilisha Bara la Afrika.

4 Anafanya maridhiano ya kisiasa
Dr Samia Suluhu Hassan anatambua kuwa taifa letu linajengwa na watanzania wote hivyo kwa kuwa ni mwana demokrasia ameona umuhimu mkubwa wa kuwaleta katika meza moja viongozi wa vyama vya upinzani,hili limepelekea kupatikana muafaka wa kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya.

5 Anatoa mikopo nafuu kwa wajisiriamali
Huu ni uamuzi wa kizalendo kwani wajasiriamali wengi hapa nchini bado ni wachanga hivyo mikopo hiyo iawawezesha kupanua biashara zao na hivyo uchumi wao na wa nchi kwa ujumla utaimarika
Mungu akubariki sana Mhe RAIS
 
Nakuandikia Rais Samia.

Naamini unafanya yote bila kushinikizwa na kakikundi furani ka watu wachache .

Hakika unapofanya jambo lililo asisisiwa na mwenzako, aliyekuwa bosi wako, embu fungua moyo na uache kinyongo.

Mmeandaa histori ya Ikulu mkaungaunga na mambo mengine ili tu kuonesha uwepo wa marais wengine. Mpeni mtu maia yake sawasawa na jamii inavyojua.

Bahati nzuri Magufuli alilijua hili na kuweka kila kitu kwenye mtandao.

Uzinduzi wa Leo umeufanya uonekane kama sio wa kuzindua Ikulu, yaani umekuwa kama ngoma ya mchiriku.

Leo ulitakiwa kutaja watu watatu tu; Nyerere, Magufuli na Samia basi.

Shida na wewe umeshalalia sana msoga; historia inaandalia na msaidizi wako afu inamuondoa mtu mhimu.
Nyimbo za hovyo zinaimbwa na watu wasio na maana na unazichekea tu.

Pale Bwawa la Nyerere, hukujifunza kitu? Wakati unazindua Tanzanite hukujifunza kitu?

Tunakusubiri Daraja la Magufuli, SGR na Bwawa la Umeme. Hapa tunataka utaje majina mawili tu! (Magufuli na Samia) - Nyerere abaki pale Bwawa la Nyerere.

Nyoronyoro za akina kikwete achana nao, walikuwa wanasafiri tu hawakufanya haya.
 
Kuna viongozi wazuri zaidi ya Samia tumuombe Mungu atuonyeshe kiongozi sahihi atakae juwa thamani ya watu wa hali ya chini na wale wenye kipato cha juu...

Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hatuja wahi kupata kiongozi mwenye kutafakari jinsi ya kuboresha maisha ya watanzania na njia ya kuboresha maisha ya watanzania...

Akipatikana kiongozi mwenye msimamo anae weza kuwakutanisha matajiri na masikini katikati ndio nchi itapata mafanikio...

Kwa kawaida kiongozi utakuwa wa ovyo kama utapendelea upande mmoja, ukipendelea masikini utafanikiwa kuteka fikra za masikini na ukipendelea matajiri utateka fikra za matajiri, matokeo yake utapata dua kutoka upande mmoja.

Nimalizie kwa kusema kuna uwezekano mkubwa wa kubadili mtazamo wa uongozi na kubadili kiongozi ili kila mwenye matamanio ya kufanikiwa afanikiwe kwa kupitia mfumo bora wa uongozi uliopo.
 
Mama ashughulike na ufisadi,Hata hao wanaotupa misaada wanachukizwa sana naubadhirifu wa Fedha wa nazotupa.hawatatupa tena kwa mwendo huu
Hapa 2025 wananchi tupiganie katiba mpya maana saivi watu wengi awaelewi wako kwenye Hali gani wengine ukijalibu kuwaelekeza wanakuona wewe ndio unahila sijui Tanzania inawatu walio kosa maarifa kiasi gani wakati mambo yanaonekana hadhalani hata hayafichwi utakuta unatoa maoni mkoa fulani wanashida Fulani alafu raisi au wabunge au mawaziri awazingati izo shida wanaangaikia masilahi yao Kama magari ya v8 yanaleta maendelo gani unajaribu kuwajulisha wananchi wajue utasikia wewe unataka uajiliwe au unataka posho Sasa mtu anae kwambia ivo utakuta Ana Maisha mazuri,wastani au ya ovyo lakini anajijali yeye kwakuwa amelizika na kile akipatacho Ila wengine wanao tesekao hataki kujua zaidi ya kupinga ukweli unaowaambia wakati mwengine wanajua ukweli Ila wanatetea ujinga
 
Habari mkuu, nawezaje tumia hiyo 5G km vifaa vyangu havisuport hiyo 5G au ndo itabidi ninunue vipya ili nimtumie hiyo huduma?
 
Habari mkuu, nawezaje tumia hiyo 5G km vifaa vyangu havisuport hiyo 5G au ndo itabidi ninunue vipya ili nimtumie hiyo huduma?
Kwa sasa ni mpaka utumie router za 5G router za kawaida hazina uwezo. Router ndogo 650,000 user 32 na kubwa 850,000 user 256 karibu tupigie 0745015421
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…