Maono ni picha inayojengeka ndani ya mtu juu ya jambo anayopaswa kufanya au kutenda na matokeo ya jambo hilo,hivyo kiongozi wa nchi anakuwa na maono pale anapokuwa na uwezo wa kuona picha ya hatma kwa ajili ya maisha ya anaowaongoza na picha ya nchi kwa ujumla itakavyokuwa hapo baadaye.
Kiongozi mwenye maono anabuni mbinu,mikakati,mawazo,sera,mipango au miradi mbalimbali ambayo ina matokeo makubwa na hivyo kuliwezesha taifa lake kupiga hatua kubwa za maendeleo.
Kwakuwa Dr Samia Suluhu Hassan ana maono chanya amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika kuwatia moyo na kuwahamasisha wateule wake na wananchi kwa ujumla katika kufikia maono hayo ya pamoja na kikubwa zaidi anajali ndoto,karama na vipawa vyao na ndio maana amekuwa akipokea ushauri na maono yao na kuyafanyia kazi ili kuleta mabadiliko.
Dr SSH ni kiongozi anayeongoza kwa mfano na ana uwezo wa kujenga uhusiano thabiti na wafuasi wake kwa kuonyesha huruma na kujali ustawi wao na pia ameweza kukuza hali ya kuaminiana na kuheshimiana na hii inawafanya wafuasi wake kujisikia salama kuungwa nkono na kuchukua umiliki.
Dr Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mtumishi ambaye ametanguliza mahitaji ya Watanzania kuliko yake na hana muda wa kutafuta faida ya kibinafsi kwa kutumia taasisi ya urais.
Yafuatayo ni baadhi ya mipango na mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi wa Dr Samia Suluhu Hassan.
1.Bima ya afya kwa wote
Hii itawezesha wananchi wengi kuwa katika mfumo wa Bima ya afya na hivyo kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya pindi mwananchi anapohitaji. Mkakati huu utaboresha sekta ya afya kwani watoa huduma kupitia Bima ya afya hupunguza mlolongo mrefu wa utoaji wa huduma kwa mteja kuanzia anapoingia getini hadi anapotoka ili kuokoa muda wa mteja kwa kupata huduma kwa wakati.
Bima ya afya ni muhimu katika Dunia ya sasa na ndio maana katika nchi zote zilizoendelea wananchi wengi wana Bima ya afya.
2 Elimu bila ada mpaka kidato cha 5 na 6
wakati wa bajeti ya mwaka jana serikali iliamua kuwa Elimu ya kidato cha tano na sita itolewe bure Ili kupunguza adha wanazokumbana nazo wanafunzi hao wa kidato cha 5 na 6.
Hivyo elimu bila ada itakuwa ni kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita. Pia serikali inaangaliwa namna ya kusaidia vyuo vya kati (colleges) kama uwezo wa fedha utaruhusu.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi 10,339,350,000. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza wizara inapendekeza kufuta ADA kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita.
Serikali itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa.waziri wa fedha alitamka maneno hayo wakati akisoma bajeti ya mwaka jana Bungeni.
3 kupitia mpango wa Building Better Tomorrow serikali imeanzisha mfuko wa dhamana kwa vijana na huduma za mikopo nafuu chini ya mfuko wa pembejeo ili kuwavutia kushiriki katika ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo
Katika awamu ya kwanza vijana 812 wanapatiwa mafunzo kwa miezi minne bure kisha wanapatiwa mashamba makubwa ambayo tayari yamewekewa mifumo ya umwagiliaji.
kwa mpango huu Dr SSH anatekeleza ndoto ya Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye katika miaka ya 70 alitaka kuifanya Tanzania kuwa ghala la chakula ili kulilisha Bara la Afrika.
4 Anafanya maridhiano ya kisiasa
Dr Samia Suluhu Hassan anatambua kuwa taifa letu linajengwa na watanzania wote hivyo kwa kuwa ni mwana demokrasia ameona umuhimu mkubwa wa kuwaleta katika meza moja viongozi wa vyama vya upinzani,hili limepelekea kupatikana muafaka wa kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya.
5 Anatoa mikopo nafuu kwa wajisiriamali
Huu ni uamuzi wa kizalendo kwani wajasiriamali wengi hapa nchini bado ni wachanga hivyo mikopo hiyo iawawezesha kupanua biashara zao na hivyo uchumi wao na wa nchi kwa ujumla utaimarika
Mungu akubariki sana Mhe RAIS