Jambo MAMA;
Wakati mwingine huwezi jua uchafu wa maji yenye lime mpaka uweke kijiko ukologe, umefanya jambo la hekima sana kukologa glasi kwa hili sakata la bandari ili ujue majii yana taka au la. Sitaki kuzungumzia kishabiki hili, try and error ni sehemu ya maisha ya mwanadamu kwa maana hatujajaliwa kujua hata ya sekunde moja ijayo, hata Baba wa Taifa alikuwa akilifanya makosa kwa namana fulani " alipomwambia Kawawa afunge maduka yababki ya vijiji" kelele zilizopigwa ziliahilisha wazo lake na likalekebishwa. Unaweza kuwa na wazo zuri tu lakini je wale unaowawazia hayo mema wanayapokeaje?
Nimebahatika kuishi kwa awamu zote za uongozi wetu kila kiongozii alikuwa na mazuri yake na madhaifu yake, na wakati mwingine madhaifu ya wakati huo yanaweza yakaonekana strengths kwa wakati wa mbeleni na strength za wakati huo zikaonekana yalikuwa madhaifu baadae mfano haikuwa na ulazima sana wa kujiingiza vita ya Uganda ambayo ilisababisha mseleleko hasi wa uchumi wetu hadi leo hii, uongozi unahitaji hekima sana na kusikiliza ile sauti ya ndani ambayo tunasema ni sauti ya Mungu, na Mungu kwa kawaida haleti sauti ya kukunong'oneza kuamua yale yatakayo waumiza Taifa.
kwa miaka hii miwili uliyoongoza naomba niungane na Rais KiKwete kwamba nuru yako ya uongozi ilionekana toka mbali, uongozi si kiwango cha elimu au mwonekano bali ni kipaji toka kwa Mungu na Mungu ndiye huyaongoza yote hayo kukufikisha kunako nafasi anayoitaka yeye.
Baada ya sakata hili yako mambo yameibuka ambayo naomba usiyafumbie macho yape nafasi tena ya kufaa yanaashilia hatari mbele.
1. tusikimbilie kwenye uchaguzi wa 2025 utaumiza wengi, na unaweza kuleta maafa.
2. kelele za uzanzibari na utanganyika zimeibuka upya na baadhi ya wazanzibari wameanza kusema Muungano ufe tugawane mbao, inawezekana ipo hoja msingi, haijaanzaa leo imeanza toka 1971 zaidi ya miaka 50 wakati wa ADUL JUMBE mpaka leo hajijaisha zinalala zinaamka, fanya Historia, historia si lazima iwe nzuri tu hata Gobachev alisifiwa na mataifa ya magharibi kwa kuvunja muungano wa soviet lakini hakujua kama ushikamano uliokuwepo ungezaa kilichotokea cha kuleta maafa makubwa ya zamani hizi ambazo ndugu wameangamizana
Ukraine na urusi kwa maslahi ya wakubwa hao.
Miaka 60 ya muungano ni mingi sana tusingetegemea uwe na uchanga wa kiasi cha kuendelea kuonyeshana vidole, rudi kwenye mapendekezo ya katiba wape haki watu wanayoidai usiogope kwamba utajenga historia mbaya ya Muungano kufia mikononi mwako mtoto alilia wembe mpe si ajabu anataka kuchonga penseli yake. wakati mwingine the higher the risk the higher the return.
niongeze mapendekezo yafuatao;,
2024 uwe ni mwaka wa kureviw katiba pendekezwa,
2025 tuwe na kipindii cha mpito wa maandalizi na katiba hiyo,
2026 tufanye uchaguzi wa serikali za mitaa kidemograsia,
2027 tufanye uchaguzi mkuu, utakaohusisha katiba mpya.
kwa wakati wote huo uendelee kuwa Raisi wa mpito, ikikupendeza kuwaachia wengine sawa lakini kama utaona vema kuingia kwenye kinyanganyilo sawa tu, lakini mimi naamini unaweza kufanya kazi muda mfupi na legacy yako ikadumu zizazi na vizazi, mf.Thomas Sankala.
Mama wa taifa letu,
Nakuombea Afya njema .
Nakuombea hekima ya Mungu kama aliyojaaliwa mtumishi wake Suleiman
Nakuomgea uongozi mahili kama aliojaliwanao Mtumishi wa Mungu Mussa
Nakuombea uaminifu katika uongozi kama aliyojaaliwa Yusufu,
Mungu akujalie roho ya kumsikiliza kwa umakini maelekezo yake,
ukisha kuwa kiongozi wa watu una dhamana kubwa sana na ni mtihani mkubwa, kuluzukiwa ni jambo moja lakini kutendea haki nafasi uliyopewa ni jambo jingine. Musa kiongozi wa wana wa Israel hakufika Nchi ya ahadi, watu wake walimkosesha akaikosa ahadi, liangalie hilo kwa makini. muda tuliopewa wa kuishi duniani ni mchache sana lakini muda wa kuishi baadae hauna kikomo Mungu atatuulia kwa kadri ya yale aliyotuluzukia na vipawa alivyotupa. vyote tunavyohangaika navyo duniani sina shaka ni vya muda na baadae havina thamani.