Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Katiba haileti ugali na kwani hayo uliyosema hayapo Kwa Sasa?

Katiba ni mfumo na nchi ni zaidi ya ugali. Hata Kenya wana ugali. Kenya, South Africa wakati wanarekebisha katiba yao walifanya kwasababu gani ? kwani wenyewe hawali ugali
 
Mwigulu ametamkwa kwenye Katiba ipi kwamba anaweza kupanga mipango bila kuhojiwa?
naongelea miradi unayo post bila sheria nzuri miradi hii itakuwa na wizi tu kama ilivyo sasa. Kila kitu ni sheria na sheria za Tanzania zimepitwa na wakati. Katiba imepitwa na wakati na CCM wenyewe wanakubali hilo.
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:

Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.

Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.

Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.

Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.

Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Namshauri tu Mama SAMIA asome alama za nyakati. Ni Hilo tu
 
Nilikosea sana kuhoji Dr. Samia kupewa kijiti. Niwieni radhi wanachama wenzangu.

Sababu kwanini Dr Samia aendelee bila kupingwa:

1. Hakuna rais mpya atakaekuja kupambana ili amalize miradi ya awamu zilizopita.
2. Rudia 1, halafu kumbuka uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora.
3. Rudia 1, sgr itachelewa kufika mwanza.

Huu mzigo ni wako na wakwetu Dr Samia. Tupambane tumalize miradi yetu.
 
Huyu ni rafiki wa wajasiriamali, rafiki wa Wafanyabiashara na wao wanajua ndiye mtu wa kukimbiliwa.

Huyu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pakua Samia App kupitia Play Store au App Store.

#samiaapp
#kaziiendelee
#tumejipatanamama
 

Attachments

  • IMG-20250211-WA0128.jpg
    IMG-20250211-WA0128.jpg
    121.5 KB · Views: 2
Hata ukiangalia tu Body Language yake kwa Jicho la Kinjagu (Kimosadi) utagundua kuwa anachoka na hapumziki vizuri.
 
Matukio ndio anapenda.
Waacheni chawa wawe chawa bahasha zina raha yake.
Sio anapenda ndo upepo alioambiwa akiendanao atakonga nyoyo za watu!, ile ni siasa na siasa ni sayansi shida inakuja ni sayansi ipi imetumika!
 
Hata ukiangalia tu Body Language yake kwa Jicho la Kinjagu (Kimosadi) utagundua kuwa anachoka na hapumziki vizuri.
kwa mfano, eti atakuwa mgeni rasmi wa 'mashindano' ya kuhifadhi kuruani. Hilo shindano nalo ni la kumchosha rais kwenda huko wakati sheikh tu wa mkoa anaweza kuwa mgeni rasmi? Itifaki waangalie matukio yenye hadhi ya kuhudhuriwa na rais, sio kumpangiapangia tu matukio ya ajabuajabu yasiyo na tija kwa taifa
 
Hili ni ombi maalum kwa raisi wangu Dr. Samia suluhu Hassan tafadhali okoa biashara yangu inaenda kuanguka vibaya

Mimi ni mfanyabiashara mdogo nilianza biashara baada ya kumaliza elimu ya juu mwaka 2019 hadi sasa ni takriban miaka 6 kwenye hii biashara

Mwaka Jana mwezi wa nne nilikuwa miongoni mwa vijana walioomba mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya kukuza biashara yangu kutokana na ukata wa mtaji lakini hadi kufikia muda huu mikopo hatujapewa japo nasikia halmashauri washakabidhiwa mikopo hiyo

Kwa heshima kubwa namuomba raisi pamoja na wasaidizi wake wanisaidie kupata huu mkopo niokoe biashara yangu kabla haijafa kwani itaniwia vigumu kuja kuanza upya endapo mkopo huo utachelewa. Nipo lushoto kata ya Sunga naomba kuwasilisha
 
Hakuna ubishi. Kila binadamu ana pande mbili. Anapendwa na kuchukiwa. Ana furahisha na kuudhi. Ana ubora na udhaifu. Anavutia na wakati mwingine kuudhi. Je kama utaulizwa ni kwanini unampenda au kutompenda rais Samia nini zitakuwa sababu? Je unapenda au kumponda na kwanini?
 
Hakuna ubishi. Kila binadamu ana pande mbili. Anapendwa na kuchukiwa. Ana furahisha na kuudhi. Ana ubora na udhaifu. Anavutia na wakati mwingine kuudhi. Je kama utaulizwa ni kwanini unampenda au kutompenda rais Sa100 nini zitakuwa sababu? Je unapenda au kumponda na kwanini?
Ninampenda Rais wangu kwa sababu ya mambo mengi ameifungua nchi kimataifa,ameendeleeza miradi mingi iliyoachwa na Magufuli hakika Samia apewe mitano tena
 
Hakuna ubishi. Kila binadamu ana pande mbili. Anapendwa na kuchukiwa. Ana furahisha na kuudhi. Ana ubora na udhaifu. Anavutia na wakati mwingine kuudhi. Je kama utaulizwa ni kwanini unampenda au kutompenda rais Sa100 nini zitakuwa sababu? Je unapenda au kumponda na kwanini?
Amefeli sana, anafanya siasa za uoga, hajiamini, anataka kupendwa na kila mtu
 
Ninampenda Rais wangu kwa kuwa yuko "composed" katikati ya UMMA ambao wengi hawapendi kufikiri kwa mapana kuhusu "integrity of the United republic of Tanzania" kuwa inategemea UMOJA wa wanaume na wanawake ,inategemea kutokuwa na ubaguzi wa kikabila ,kikanda ,kijinsia na kidini......

Wako wanaomchukia Rais wangu kwa jinsi yake....hao ni MISOGYNYISTS!

Wako wanaomchukia Rais wangu kwa Uzanzibari wake....hao ni watu dhaifu na wabaguzi......


Wako wanaomchukia Rais wangu kwa haiba ,mwonekano wa mavazi yake.....hao ni watu dhaifu wasiojitambua kuwa heshima ni kuheshimu wengine walivyo hata kama huwapendi.....

Wako wanaomchukia Rais wangu kwa kukosa tu kufikiri vyema.....

Mimi ninampenda kwa UJASIRI ,KUTOKUYUMBA ,na kuwa na malengo makubwa ya kutuachia ALAMA itakayowafaidisha hata wale WANAOMCHUKIA NA KUMBAGUA !!

#Urais ni TUNU ya taifa ,kumpinga Samia umeipinga tunu ya taifa teule la Tanzania !!

#Punda afe,JMT idumu milele !!

#Tunu za taifa kwanza na kwa njia yoyote iwayo!!
 
Back
Top Bottom