Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli huu nao ni ushauri!!!Mama Samia usinisahau Bujibuji kwenye ufalme wako.
Tulete mzani au tusubiri kidogo?Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya....
Sijui kama kuna la maana na la kweli zaidi ya uchawa la kumpongeza huyu muungu wenu anayekula na kunonihino.Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli amefariki, lakini spirit yake inaishi. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi, iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli amefariki lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana, usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili, lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli inaishi. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60 kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mama Samia angepumzika nafasi ya uRais imemzidi kimo.Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Uko sahihi kimo alichozisiwa ni hiki hapa 👇 👇Mama Samia angepumzika nafasi ya uRais imemzidi kimo.
Kukodisha Bandari za Tanganyika na kuziacha Bandari za Zanzibar ilikuwa kosa kubwa ambalo Watanganyika hatuwezi kumsamehe.
Uko sawa kabisa ,la maana hakuna haya yote ni hasara tupu na ndio uchawa wenyewe 🤣🤣👇👇Sijui kama kuna la maana na la kweli zaidi ya uchawa la kumpongeza huyu muungu wenu anayekula na kunonihino.
Katiba Mpya haileti chakula mezani au wewe itakisaidiaje kuongeza kipato chako kama mwananchi?Raisi Samia angeleta katiba mpya na chaguzi ziwe huru angepewa Nobel Peace Prize. Lakini sidhani kama ana weza bado kufikiria nchi juu ya matakwa binafsi.
Kwa hili kutokea inabidi tupate Rais ambaye Tanzania ni muhimu kuliko madaraka binafsi kama yule wa Botwasana.
Tuiombee nchi hii na tamaduni za ubinafsi kwa uongozi
Na Samia hajawahi kuwa na shoo mbovu kamwe 👇👇Mtapata taabu saana maana Mama Samia is the 'iron lady'! Ukiingia anga zake tu kuvuruga serikali iliyoyaanzisha chini ya JPM, ambayo yy naye alikuwa sehemu ya serikali hiyo lazima apite na weye!
Hamtaamini huyu mama atakavyokuwa zaidi ya Magufuli kwa kutokucheka na nyani! Mama Samia atapandisha viwango vya uongozi kiasi kwamba tutatamani aendelee kutawala kwa muda mrefu!
Nafasi ya mwanamke kuchukua madaraka makubwa inaenda kuhakikishwa kwa utendani bora wa Mama Samia! Wezi mmeula wa chuya! Hamna chenu hapa!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
😭😭😭
Katiba Mpya haileti chakula mezani au wewe itakisaidiaje kuongeza kipato chako kama mwananchi?
Rais anatakiwa kuongeza juhudi zaidi kwenye sekta zinazogusa maisha ya wengi eg Kilimo 👇👇
View: https://x.com/TanzaniaYaMama/status/1887788912895988067?t=2gR0TWd-cM3ldeMKQ4HOKw&s=19
Katiba haileti ugali na kwani hayo uliyosema hayapo Kwa Sasa?Katiba ni mfumo wa uendeshaji shughuli zote za nchi. Kwa sasa kila mtu hata CCM wenyewe wanakubali mfumo wa Tanzania kwenye sehemu zote si mzuri au umepitwa na wakati. Kubadilisha mfumo ndiyo kubadilisha katiba. Mfano modogo tu ambao hauna uhusiano na siasa maana nyie mkisikia katiba mnafikiri chaguzi tu.
Uchumi
Kwa nchi zinazoendelea mfano bank kuu imepewa mandate kwenye katiba kushughulikia ajira. Kwasababu hii bank kuu zinahakikisha mikopo ipo chini ili biashara ziweze kukopa na kuongeza ajira. Hii mandate bank ya Tanzania haina hivyo ajira sio agenda yake. Hivyo kwa sasa bank kuu haijali ajira badala yake inajali faida za mabank tu na hii inasababisha mikopo riba kuwa juu kila mara na kukoshesha ajira vijana. Hii ni ngumu kuielewa kama hujui uchumi.
Kilimo
Migogoro wa Ardhi pia ni tatizo la kikatiba kwa ardhi kumilikiwa na vijiji. Hii inaweka utaratibu wa ununuzi kuwa mrefu na kupunguza uwekezaji. Uwekezaji wa kilimo ndiyo chakula chenyewe
Mahakama
Kwa utaratibu wa sasa kesi za chaguzi zinaweza kuchukuwa zaidi ya miaka 5 ! wakati nafasi za nyeo hazizidi miaka mitano. Yaani mtu anaweza kushinda kinyemela ukaenda kumshitaki halafu ukamshinda miaka mitano ambayo amepata pesa na mshahara bila kuwa na haki. Hii inatakiwa ibadilishwe kwenye katiba
Uraia sheria zimepitwa na wakati
siasa
Tume inatakiwa kuwa huru na wateuliwa wasiwe wateuliwa wa Raisi wapewe budget kikatiba kama mahakama. Kwa faida ya vyama vyote ili chaguzi ziwe huru
Muundo wa serikali idadi ya mawaziri ipunguzwe kikatiba.
serikali za zone zipewe nguvu badala ya kusubiri pesa kutoka Dar au Dodoma
Haya yote yanahusu pesa , uwekezaji na miradi. Yanahusu uchumi ambao ni chakula . Hii ndiyo maana sisi bado ni masikini ni miundo.
Katiba iweke sheria imara za rushwa
Sasa hayo yote hapo ni mifano tu. Katiba ndiyo chakula ndugu yangu acheni kujifanya wajinga
Mwigulu ametamkwa kwenye Katiba ipi kwamba anaweza kupanga mipango bila kuhojiwa?Hizo tender nyingine anapanga mwigulu na hakuna wa kumuhoji! na ndiyo maana kuwe na katiba na sheria nzuri na mifumo mizuri kwasasa matajiri ni mawaziri tu