Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Mimi nafurahia mifumo kandamizi inayowezesha CCM kuendelea kuwa madarakani ili jamii ipate akili kwasababu tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo haiwezi kuchakata fikra chanya na hasi jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

Hii itasaidia watu kuendelea kuwa na umasikini uliokithiri ili watawlike kirahisi yaani hakuna kelele, hawa tukiwaambia msiwapigie kura wapinzani kwasababu hawana serikali wataelewa

Hata ukiwambia chadema wanampongo wa kuleta virusi vya epoxy na ebora kupitia michango ya tone tone nimo watashangilia nyuma ya mikamera
 
Raisi Samia Jitoe Kwenye Uchaguzi halafu rudi zako Nyumbani ,waachie mazimwi wanaojuwana ,wewe utabaki kuwa mgeni hawakujui watakula wakakumaliza.

Rudi Zanzibar tulia endelea na maisha ulee wajukuu zako, hayo ya huko waachie .Tupate Raisi wa Tz Mtanganyika Makamo Mzanzibari baada ya mwaka Raisi anakufa waZanzibari kama kawaida tunaongoza tena Tanzania , Kwani mzanzibari kushinda Uchaguzi wa Tanzania ni mtihani ,na hawapendi.
 
Acha tutengeneze historia mpya ya kuwa na raisi mzanzibari Kwa kupigiwa kura
 
Kuna mada nyingi hata mama abduli na abduli wake inawezekana wakawa na washauri wenye tabia za Elon musk.

Unajua ukiwa na mshauri mfano mwijaku kwa alikiba basi ujue alikiba anaweza kuwa na tabia za mwijaku kama baba levo kwa diamond.

Kwa sasa trump anabeba chuki ambazo Elon amefanya afrika yeye na baba yake.
 
Moderator imekuwaje mada yangu kuwa pongezi
 
Kama huamini Samia huu ndiyo mwisho
 
Wewe sio wa kulaumiwa kabisa. Nchi yetu ya TANZANIA ina miaka sitini na nne (64) toka tupate uhuru na wewe ndio kwanza hata miaka minne huna kwenye utawala wako. Hivyo kuna kitu cha kulalamikiwa na sio mtu kama mtu. MFUMO MBOVU wa utawala na sera zenye kubinafsisha mawazo ya nchi kuwa ya watu wachache.

PIGANA NA RUSHWA KWENYE AWAMO YAKO HII YA MWISHO KAMA UTASHINDA UCHAGUZI NA MUNGU AKAKUWEKA HAI.


NA KUSISITIZA SANA PIGANA NA RUSHWA MAMA UTANISHUKURU UKIWA TAABANI SIKU ZAKO ZA MWISHO WA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI.
 
UWEZO WA KUPIGANA NA RUSHWA HANA, NIA WALA DHAMIRA HIYO HAIPO.
 
Anapoongea hana issues za Kitaifa wala Kimataifa. Mweupe sana. Hajui lolote maskini. Labda tu kuwachamba wapinzani. Ila huwezi sema ukae umsikilize. Huwezi mwelewa. Atajisifu tu yeye ni chura kiziwi na Lissu ni Dume la Simba sumbufu.

Hayo tu.mengine hajui labda aseme kuwa kahawa ni nzuri pia kufanyia scrub.uso unang'aa sana n.k

Yaani tuna bahati mbaya sisi...tangu aondoke Mkapa basi maskini tunapata watu wa ndo hivyo hivyo tu.
 
Rais analipwa mshahara, ni kwa nini asitumie mshahara wake kuendeshea maisha yake akiwa Ikulu?
 

Kwanza, namshukuru mheshimiwa rais daktari, profesa, na mbeba maono Samia Suluhu Hassan na, pili, nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa yafuatayo:​

Mosi, kumkamata na kumsweka ndani Tundu Lissu ili kinuke hadi nje ya nchi.​

Pili, kujua kuwa Lissu ni tishio la ulaji na uchawa wake.​

Tatu, kutambua kuwa Lissu analenga kuvuruga amani yetu ya imani iliyotamalaki nchini kiasi cha kila mtu kuwa na uhuru wa kufanya atakavyo isipokuwa kutofautiana naye.​

Nne, kukaa kimya kama chura ili kuacha tujadili tutakavyo.​

Tano, kuunda tume 'huru' ya uchakachuaji itakayomwezesha kushinda kwa kishindo na kwa miujiza.​

Sita, kumteua mkwewe kuwa waziri anayeshughulikia mambo ya uchaguzi.​

Saba, 'kupaisha' uchumi hadi chawa wananenepa, kuzaliana na kutanua.​

Nane, kubuni R nne yaani Ramba, Rarua, Rudisha nyuma, na Rembesha magamba.​

Tisa, 'kufungua' nchi.​

Kumi, kwa royal tour na utanuaji kinomi.​

Si inapendeza??​

 


Si mara moja wala mbili kusikia mashehena wakisema kuwa mheshimiwa rais daktari profesa SSH ni mbeba maono japo hatuyaoni. Yeyote anayejua haya maono atuonyeshe lau tuyajue na kumshukuru sana mheshimiwa rais daktari SSH.​

 
Kwanza, namshukuru mheshimiwa rais daktari profesa SSH. Pia, namuomba akubali nimtunuku cheo cha Profesa Eemerita.

Sambamba na hili, namuomba awaite wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki wakubali kuunganisha nchi zao na mheshimiwa rais awa rais wa Shirikisho la Afrika Mashariki. Zifuatazo ni faida zitakazotokana na hili:

Mosi, ataondoa umaskini kwa kuwapa wananchi wa eneo hili mamilioni ya fedha ili waondokane na umaskini kwa sababu ana roho nzuri sana.

Pili, aweze kufanya miujiza ya kukuza uchumi wa eneo tokana na umahiri na maono yake.

Tatu, aweza kuwakamata na kuwafungulia kesi za uhaini wapinzani kama vile Kiiza Besigye, Righathi Gachagua, Moise Katumbi, Victoire Ingabire, Agaton Rwasa, Riek Machar, na wengine wanaoleta chokochoko ili waungane na mwenzao Tundu Lissu tunduni.

Nne, awajengee miundo mbinu safi na ya kisasa kama alivyofanya Tanzania.
Tano, adumishe amani na mshikamano na mengine mengi.
Si inapendeza?
 
Habarini wakuu wa jamiiforums
Haya ni mambo muhimu ya kumpongeza Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

1. Kuwa Rais wa Kwanza Mwanamke Tanzania

Mama Samia aliandika historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini Tanzania tangu kupata uhuru mwaka 1961. Hii ni hatua kubwa kwa usawa wa kijinsia.



2. Uongozi wa Kidiplomasia na Mshikamano

Amekuwa kiongozi mwenye busara, anayependelea mazungumzo na mshikamano wa kitaifa. Amefanya juhudi za kupunguza migawanyiko ya kisiasa na kijamii.



3. Kufufua Mahusiano ya Kimataifa

Ameboresha uhusiano wa Tanzania na nchi nyingine kwa kufanya ziara mbalimbali za kikazi nje ya nchi, jambo lililoimarisha jina la Tanzania kimataifa.



4. Kuhamasisha Maendeleo ya Uchumi

Ameweka kipaumbele kwenye ujenzi wa miundombinu kama reli ya kisasa (SGR), barabara, na miradi ya nishati kama Bwawa la Mwalimu Nyerere.



5. Kusikiliza na Kushirikisha Wananchi

Anaonekana kuwa kiongozi msikivu na mwenye moyo wa kusikiliza hoja za makundi mbalimbali ya jamii, akiwemo wapinzani, wanawake, na vijana.



6. Kuweka Mkazo kwenye Elimu ya Juu na Ufundi

Ameongeza bajeti ya elimu, na kutoa fursa zaidi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume kupata elimu bora, ikiwemo mikopo ya elimu ya juu.



7. Kujali Afya ya Umma

Ameendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga vituo vya afya, hospitali za wilaya, na kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.



8. Uthubutu na Uvumilivu katika Uongozi

Licha ya changamoto nyingi, Mama Samia ameonyesha uvumilivu mkubwa na uthubutu wa kufanya maamuzi magumu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…