Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nipo na wananzengo hapa wanasema mitandao imeona mzee amekufa wameamua kupandisha bei na wanaenda mbali zaid kwamba kama mambo ndo hayo sio mda na ada zitarudi.

Mama hebu tupia jicho suala hili kwa haraka maana linagusa watanzania wengi sana moja kwa moja.
 
Kwa hiyo vifurushi vikishushwa bei ndio CCM iendelee kututawala?

CCM siku zote ina jihujumu yenyewe, haihujumiwi na mwingine yeyote.
 
Ndugai atakuwa amefurahi sana! Kwa akili yake finyu anaamini baada ya kupandisha gharama, vijana wengi watatumia muda wao mwingi sasa kufanya kazi! badala ya kuchati tu mitandaoni!

Utadhani hizo hela za kununulia hivyo vifurushi anawapa yeye! Zero brain kabisa!
 
Habari wanajf, Leo ni lazima niliongelee hili ili roho yangu itulie.

Nimemfatilia mama muda mrefu Sana toka enzi za JPM Hadi sasa yeye kuwa raisi.

Mama Samia nathubutu kusema ni shujaa na ni chuma, jinsi anavyofanya kazi zake na jinsi ambavyo anaimudu hadhira.

Teuzi zake zote zipo vizuri na atawamudu, naiona Tanzania ikipaa zaidi kiuchumi. Hivyo Mimi bila kushawishiwa na Mtu yoyote naunga mkono mama Samia akae hata miaka 20 kwenye uraisi.

Ana maono, ana uthubutu na ana uwezo, ninamuona Kama malaika.

Kongole mama Samia, shikilia hapohapo na nitakuwa mkali kwa yoyote ambaye atakuwa na dhamira ya kukwamisha na kukuchafua
 
Hivi sifa/kigezo kikuu cha kuwa mataga ni nini? Uwezo wa kuimba mapambio! Uwezo wa kusifu na kuabudu watu! Uwezo wa kulamba watu wengine miguu! Unafiki ulio pitiliza, au!🤔
 
Ni mapema sana kumtabiria huyu mama mambo mazuri lakini muda utasema.
 
Hivi sifa/kigezo kikuu cha kuwa mataga ni nini? Uwezo wa kuimba mapambio! Uwezo wa kusifu na kuabudu watu! Uwezo wa kulamba watu wengine miguu! Unafiki ulio pitiliza, au!!! [emoji848]
Tulia hivyohivyo dawa safari hii inaingia taratibu sana
 
Mh. Rais, kwanza nikupe pole kwa majukumu mazito uliyonayo ya kutuongoza. Pia naelewa una washauri wengi sana na muda mchache wa kusikiliza kila kitu kinachoongelewa mitaani.

Sina uhakika hata haya ninayoyaandika kama yatakufikia, lakini nimeona nijaribu bahati yangu.

Binafsi nafikiri umeanza vizuri, lakini kwenye haya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri nilipata mshangao mkubwa kwenye uteuzi ulioufanya kwenye wizara moja. Mtu mmoja uliyemchagua kushika wizara hiyo muhimu (sitomtaja) hakubaliki na watu wengi sana kutokana na tabia yake ya majivuno na kutokuwa na adabu.

Kama kweli una nia ya kuleta umoja wa kitaifa ningekushauri uwachague watu wanaokubalika na Watanzania wengi.

Sasa ili kuthibitisha haya niliyoyaandika ni ya kweli huyo jamaa sijamtaja kwa jina lakini utajionea mwenyeowe ni nani atatajwa, watu wengi wanajua tabia zake hata kama hujamtaja kwa jina! Kama ni hiyo fani yake Tanzania ina watu wengi waliyoisomea pia.

Basi kwa leo ningepeda niishie hapo na nakutakia kazi njema.
 
Usimfundishe kazi mzee.

Kauka hvohvo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nilitamani kuwa na fursa kama hii ya kutoa ushauri kwa viongozi wetu juu ya masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yanayoihusu nchi yetu. Bahati mbaya jambo hili nililolitamani halikuwezekana kipindi cha awamu ya tano. Sio kwamba sikupenda ila nilikuwa nimebanwa na majukumu mengi. Nashukuru kwa sasa imebidi nijitahidi kufanya hili.

Katika jumbe zangu fupi fupi za maoni, nimedhamiria kutoa maoni 100 kwa kuanzia kwa viongozi wan chi yangu kwa kadiri Mwenyezi Mungu atakavyonijalia uzima, nguvu na afya.

Maoni haya mawazo binafsi hivyo si lazima yafuatwe kwa namna yeyote ile ila yaweza kuchukuliwa kama sehemu ya kujifunza na pengine likaboreshwa zaidi na hata kuachwa kama yalivyo.

Maoni yangu haya yatakuwa mafupi kadiri iwezekanavyo ili nisimchoshe yeyote kusoma na nitakuwa nayotoa kidogo kidogo.

Ikiwa maoni haya yameshawahi kutolewa basi ichukuliwe ni sehemu ya msisitizo kwa jambo husika.

Karibuni watanzania wenzangu tuijenge nchi yetu.
 
Rais wangu wa sasa hakuwahi kutegemea kuwa atakuja kuwa Rais. Hakuwa kabisa na ndoto hiyo na kwa maana hiyo hakuwa hata na wanamtandao. Sheria nyingi zilikuwa zinaelekeza teuzi za viongozi zinafanywa na Rais au Waziri. Hakuna Sheria inayompa nguvu Makamu wa Rais kuteua nafasi ya uongozi wowote. Sheria hizo pia hazikusema kuwa wakati Rais akiteua anapaswa kushauriana na Makamu wa Rais. Hapana - hazisemi hivyo.

Ni ukweli kuwa Makamu wa Rais ni ngumu sana kuwa alikuwa na mtandao wake wa kiuongozi au matarajio kuwa katika kipindi Fulani ataingia kwenye madaraka ya URais - hakuwa amejiandaa kabisa kwa hilo.

Ndiyo maana mie sioni tatizo kwa teuzi anazofanya sasa hata kama anakosea au kurudisha watu wale wale. Huyu Mama yetu Mpendwa hana mtandao na hana watu wengi aliowaandaa au kuwafikiria kuwa watakuwa viongozi. Ni lazima awatumie wale wale na apate wachache ambao alikuwa anawafahamu yeye.

Ninamshauri Rais wangu hata kama baada ya kuteua anagundua amekosea asiwe mnyonge na asisikitike kamwe. Ndiyo uongozi ulivyo! Kikubwa awe mtulivu na sifanye faster faster - anaweza itisha hata CV nyiiiiingi za watendaji waandamizi then akatumia watu anaowaamini kufanya uchunguzi kdg then atapata watu bomba kabisa. Asifanye kutegemea sana watu waliokuwa karibu na mtangulizi wake - hawa watamlisha tango pori tena na tena, kwa sababu tayari walimlisha tango pori kuhusu siku 14 badala ya 21 za maombolezo na jana wamemsababishia ameteua mtu anayefaa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM au Mkuu wa Wilaya.

Kwa Taasisi hizi kama NSSF, TPA, TASAC n.k anaweza kufanya kama Enzi za JK - tangazo linatoka waTanzania wanashindanishwa anayeshawishi Zaidi anapewa. Teuzi teuzi hizi za majina ya kutoka kwenye Mfuko wa Koti zimetufikisha pabaya sana Rais Wangu Mpendwa SSH.
 
Kwanza nikupongeze madam President kwa kuwa Rais wetu , naona umeanza kupanga safu yako mpya itakayo fanya kazi na wewe safi sana, ila naomba nikupe ushauri kidogo si lazima uufanyie kazi ila kama utaona inafaa, tunapata ukakasi kdgo.

Awamu iliopita tumeona sekta binafsi ikiachwa sana kama yatima kumbe ndio inabeba watu wengi sana na kuongeza wigo wa kodi, sasa basi tunaomba rudisha heshima ya hii sekta, ntakupa mfano mmoja mdogo sana ambao hata hauhitaji phd,

kuna shirika kama TASAC hyu ni regulator wa shipping lines, kampuni za wakala wa forodha ( CLEARING/ FORWARDING) kazi zao ni kutoa mizigo na kusafirisha, iweje leo tena huyo tasac nae anatoa mizigo bandarini kazi ambazo zinafanywa tyr na CFA? tena anachukua kazi zao na kuijipangia mizigo yake, je huoni hapo kama kuna conflict of interest?je yeye nani ana mregulate?

Hya leo LATRA nae anunue mabasi yake ajipangie route kama moshi na arusha hakuna basi jingine kwenda route hyo, TCRA Nao wauze airtime na vocha basi !Nafhani ifike muda kurevised hizi sheria za haya mashirika hasa tasac.Tuwe na uwanja sawa wote isiwe mtu mmoja ana monopoly biashara tu, tasac iwepo ifanye kazi yake ya kuregulate tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…