Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Vigezo vya kirasimu, eti mpaka uonyeshe barua ya mualiko, mkataba wa kazi na maswali kibao kuwa unaenda kufanya nini.
Watu inawashinda hapo, inatakiwa unaenda unawapa namba ya NIDA na laki unusu yao na kesho unapata Passport, tena ujaze tu online.
Kuwa na NIDA sio kuwa raia, passport utolewa kwa aliye raia.

Kama una mwenyeji unaenda mtembelea anashindwa nn kukuandikia barua dakika sifuri tu kwenye email anakutumia.

Hakuna nchi yeyeto unaweza ukaingia tu kama mbuzi lzm utoe sababu zinazowaridhisha wao mfano unakuja kufanya nini, mwenyeji wako ni nani,una pesa kiasi gani ukipata shida zikusaidie,nk.
 
Kuwa na NIDA sio kuwa raia, passport utolewa kwa aliye raia.
Kama una mwenyeji unaenda mtembelea anashindwa nn kukuandikia barua dakika sifuri tu kwenye email anakutumia.
Hakuna nchi yeyeto unaweza ukaingia tu kama mbuzi lzm utoe sababu zinazowaridhisha wao mfano unakuja kufanya nini, mwenyeji wako ni nani,una pesa kiasi gani ukipata shida zikusaidie,nk.
NIDA wanatoa vitambulisho vya uraia , au labda kama tunazungumzia NIDA tofauti. Na hayo mambo na maswali unayoweka wakuuliza ni ubalozi wa nchi unayoenda ili wakupe Visa na si uhamiaji wanaotoa Passport.
 
Afrika nzima ni Maraisi wawili tu ambao walikuwa wakitoa command kuwa hiki kifanyike kwa ajili ya wananchi wanyonge watendaji wa serikali, bunge na mahakama wanatekeleza mara moja

Viongozi hao ni Magufuli na Kagame tu.Wengine hamna kitu.
Mama Samia ndio unaingia kazini kazi kwako.Je utasikilizika?
Hawa ni mabingwa wa propaganda na kuonekana mbele ya camera ni watu wanaojenga fence nzuri nje ya gharama na za kisasa lakini ndani nyumba za udongo tena choka mbovu wanawatumia wanyonge kama toilet paper sababu ni rahisi kuwabrain wash wanyonge.
Hakuna mtetezi wa wanyonge hapa unayaijua dhiki ya maisha ya wanyarwanda.Maghorofa ya kigali sio ndo maisha ya wanyarwanda.
 
Ni kweli ngumu kumesa ila hana namna ili mambo yaende sawa.
Ukiwa mtu wa kufikiri kwa kina, mama Samia anawakati mgumu na hatari sana.

Mosi kama kweli yeye ni mzanzibari na anaipenda Zanzibar basi tunaenda kupata katiba mpya tena ya mzee wetu Warioba.

Mambo ni mengi ila mda mchache.
Sawa maoni yako yamepokelewa mkuu
 
Mama Samia inabidi awaruhusu watu kwenda nje ya nchi kirahisi. Urasimu wa kwenye passport ufe. Yeyote anayetaka passport apewe bila masharti ilmradi tu awe matanzania. Ikibidi nikionyesha tu kadi ya NIDA nipewe passport.

Tuachane na mtindo wa nchi za kijamaa kufungia watu wake.
Uko sahihi Mama aanze na hili kama hawataki awatumbue biashara iishie hapo aweke wengine
Wajinga sana wanauliza maswali ya kumpa mtu Visa yanayotakiwa kuulizwa kwenye ofisi za ubalozi kuendekeza rushwa eti ohhh unaenda chi gani kufanya nini ambatanisha ushahidi!!! hayo ni maswali ya balozi unakoenda sio ya uhamiaji


Hata ukitaka kura za vijana 2025 hii ni pointi kubwa hii peke yake yaweza kukupa credit kubwa mno

Nchi jirani hawaulizi hilo swali .Uhamiaji watoe passport yaliyobaki waachie balozi husika sababu kupata passport sio lazima iwe kupata Visa.

Mama Samia hii ni Kero na wala haihitaji kubadili sheria hizo ni kanuni tu waluzojipangia immigration hakuna sheria inasema ukiomba passport ueleze unaenda wapi na kwa sababu ipi hata kama ipo ipige chini

pili mapato ya serikali yataongezeka mfano watanzania tuko milioni 60 mwaka huu wakisema watoe passport milioni 2 tu kila passport bei ni laki moja na nusu serikali itapata shilingi bilioni 300 zinatosha kusaidia miradi kibao .Waliochukua passport wawe wanasafiri au la sio kazi yao Watajijua kinawauma nini mtu akichukua passport na hasafiri? Wanakomaa tu ohhh passport ni kwa ajili ya anayesafiri sasa mtu akiichukua na hasafiri akakaa nayo ndani mfano kuna tatizo gani hadi wakomae? Mtu umempa passport na hasafiri mfano hadi inaisha muda kinawauma nini?
 
Akifuata ushauri wako yale ya Jumbe yatamuhusu,hakuana mtanganyika mjinga kama wewe,naona ulikuwa unabebwa tu na chuki yako dhidi ya mzee Magufuli
Hio ndio faida y serikali mbili maana nyinyi hua hamuoni mbele. Narudia, Mama Samia ateua IGP, CDF na Boss wa TISS kutoka Zanzibar ili muone faida ya huu Muungano.

Mngekuwa na akili na wenye kuona mbali, msingeendeleza aina hii ya Muungano na hii Katiba tuliyonayo.
 
Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:...
Mbona unamtisha !! Mr zimmerman . Mwache aongoze kwa uelekeo wake .

Mwinyi hakulazimika kumfuata Nyerere , wala Mkapa hakulazimika kumfuata Mwinyi. Kikwete alienda tofauti na mtangulizi wake. Halikadhalika Maghufuli hakuwahi kumuiga Kikwete, alienda ki vyake. So Rais Madame Samia ataonyesha kipaji chake .

Maghufuli Mungu amemuondoa kwa makusudi ili pengine asiharibu yale aliyoyafanya
 
Uko sahihi Mama aanze na hili kama hawataki awatumbue biashara iishie hapo aweke wengine
Wajinga sana wanauliza maswali ya kumpa mtu Visa yanayotakiwa kuulizwa kwenye ofisi za ubalozi kuendekeza rushwa eti ohhh unaenda chi gani kufanya nini ambatanisha ushahidi!!! hayo ni maswali ya balozi unakoenda sio ya uhamiaji....
Wangeweza kupata pesa ya kuendesha hiyo idara ya uhamiaji na kutoa gawio serikalini. Kijana hana kazi, si bora umrahisishie aende nje akuletee remittance!.

Kwaweli waliotunga huu upuuzi na wanaoung'ang'ania wanapaswa kupangiwa majukumu mengine.
 
Naona tayari ameanza kwa mistake ileile ya mtangulizi wake.

Nilijua awali watendaji hawavai barakoa kwa kuhofia kukinzana na Boss wao aliyekuwa ameamua kuukataa ukweli.

Kuna uwezekano mkubwa mpaka 2025 tukapata Rais mwingine au wengine.

Wito wangu kwa Mhe Samia,serikali i-rewind ile miongozo ya COVID 9 iliyoanza nayo mwaka mmoja uliopita kabla ya kuitekeleza siyo lazima muwafungie watu ndani.

Kwa kuanzia kwenye hizi shughuli za kuaga mwili wa JPM, otherwise mid April itakuwa na misiba yakutosha.
 
Ushauri mwingine kila wizara hasa zinazosababisha kero kwa wananchi walio wengi zijieleze kila week yaani weekly report kuwa zimefikia wapi kutatua kero za walio wengi mfano TRA ,Traffic na Rushwa zao na kitengo cha passport humu mumeandikwa sana malalamiko ya hawa watu Wampelekee weekly report
 
Leo tarehe 19 Machi 2021 Mama yetu Mh Samia Suluhu Hassan ameapishwa kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kuapishwa kama ilivyo ada Rais alitoa hotuba yake. Naweza kusema ilikuwa ni hotuba inayosisimua, inayotia matumaini, inayoonyesha mwelekeo mpya km taifa, pambazuko jipya.

Hotuba ya kuponya majeraha, Mheshimiwa amatuasa tusiangalie nyuma bali tushikamane km taifa tuwe wamoja tuijenge Tanzania mpya. Naamini kila mmoja alimuelewa MH Rais.

ÑAKUOMBENI ninyi niliowataja hapo juu,ikiwa Mama Samia anataka kuyaishi maneno yake na ikiwa ana NIA YA DHATI ya kuijenga Tanzania basi tutakapopata wasaa wa kuteta nae jambo letu la kwanza au SWALI LA KWANZA tutake kuujua msimamo wake juu ya KUANZA UPYA MCHAKATO WA KATIBA MPYA INAYOTOKANA NA MAONI YA WATANZANIA. Kama hayuko tayari kwa hili basi tujue hakuna jipya Ni siasa zile zile za kudanganyana,KUOMBA AMANI WAKATI NYUMA MIKONO IMESHIKA PANGA.

Suala la KATIBA MPYA ndiyo litakalotufunulia dhamiri yake ya ndani,Ndiyo suala ambalo litatuonyesha km kuna kusonga mbele kwa maridhiano au tumeangukia mle mle.

Tuna kwa mfano TUME YA UCHAGUZI AMBAYO VIONGOZI WAKE WANATEULIWA NA RAISI ALIYEKO MADARAKANI NA RAIS HUYO NAYE NI MSHINDANI KATIKA UCHAGUZI.Ataachaje kutangazwa mshindi wakati viongozi wa Tume Ni wateule wake.(HAYA NI MAHOKA NA UNAYAPATA TZ PEKEE)

Tutumie kipimo hiki kwa sababu KATIBA NDIYO KILA KITU!!
 
Hongera mama Samia. Mungu awe nawe katika utumishi wako.

Kwangu Mimi Jambo la Kwanza la kuangalia utawala ni jinsi serikali itakavyo heshimu mipaka ya kiutumishi na matakwa ya kazi husika. Nipenda kuwe na semina elekezi kwa jeshi la polisi kuhusu wajibu wao kwa watanzania kwavile ndio jicho la Kwanza kwa utawala linapotua. Pia kwa DCs na RCs.
 
Hili la katiba sahauni ndugu zangu. Ccm kutengeneza katiba ni sawa na kunoa kisu ili kiwakate wao wenyewe.


Katiba hutengeneza mara baada ya kuchapana na kuvunjana mikono, shingo na viuno.
 
Back
Top Bottom