Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kama ndoto huja kweli, kuna uwezekano mkubwa wa mama kuhurumia wafaidika wa mifuko ya jamii na kurejesha FAO hili lililokuwa msaada mkubwa kwa wanachama
Endelea kuota. Ila kwenye ndoto ukiona choo usikitumiee😉
 
Kitu ambacho Maadam atacheza kama pele ni hiki cha kuruhusu FAO LA kujitoa. 2025 wala hatapata tabu wapiga kampeni wake wakujitolea bila malipo tupo hapa tumejaa tele.
 
Habari wana Kilabu,

Nimekaa na kutafakari sana dira ya Utawala Wa Rais Mama Samia (Kipenzi Chetu Raia) na mwelekeo wake. Hakika taifa limepata taa ya kuangaza njia baada ya giza nene kutanda kwa miaka 5 iliopita. Katika hio miaka 5 iliopita;

● Taifa limetoka katika hali ya kupoteza mwelekeo, na sasa limerudi katika mstari wenye muelekeo.

● Taifa lilikosa matumaini na kujikatia tamaa, na sasa taifa lina matumaini ambayo yamerudi kwa speed ya ajabu.

● Taifa lilikosa upendo na mshikamano sambamba na utaifa, uadui ulipandikizwa na utawala uliopita, uadui baina yetu sisi kwa sisi raia ndio ulikua kama dini yetu na ulishika hatama, na hatimae sasa upendo na mshikamano kwa Raia umerudi.

● Taifa lilikosa usawa na haki, Dhuluma/Uonevu/Unyanyasaji/Ukandamizwaji/Udhalilishaji/Uongo ndio zilikua sifa za kuwa kiongozi bora kwa wilaya na mikoa nchini, ndio zilikua CV za kupata ajira ya uongozi katika serikali ya Awamu ya 5. Na sasa usawa na haki zimerudi.

● Taifa lilikosa uoga wa mwenyezi mungu, kufikia hatua viongozi wetu wa ibada kutukanwa na kutolewa maneno ya dharau/dhihaka/kejeli mbele za waumini wao katika nyumba za ibada (Wengine kufikia hatua kuvuliwa uraia wao ili wanyanyaswe na kutaabishwa). Uoga na Imani ya mungu kupotea ulipelekea hata sisi waumini kushindwa kuwatetea viongozi wetu wa dini hayo yalipotokea, uoga wa mungu ulikua midomoni kwa maneno tu, na si kutoka moyoni na kwa matendo. Sasa mungu ameingilia kati na kulirudisha taifa mahali salama anapoona linafaa.

Nukuu;

"Mungu alisema hakuna mtu mwenye uwezo wa kuilinda dini yangu na kitabu changu, mimi mwenyewe ndio ntazilinda"

Nirudi kwenye mada husika,

Miongoni mwa mambo ambayo natamani Rais Samia Suluhu angeyafanya (Japo nafahamu kwamba mengine ni magumu sana kufanyika kutokana na serikali kutokua na fedha za kutosha, taharuki ya ubadhirifu wa mali za umma kuepuka baadhi ya wanasiasa hasa wa CCM kumponda na kumpinga na mengineyo mengi); ila ni busara kama yangeweza kufanyika;

1) Kuvunja "BUNGE LOTE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA" na kuitisha uchaguzi upya wa wabunge. Najua ni jambo lisilowezekana, kwasababu bunge limejaa fisi wenye njaa kali sana.

Hii ni kwasababu bunge lililopo ni "MAALUM KWAAJILI YA MASLAHI YA MAGUFULI & UTAWALA WAKE" na sio kwaajili ya "WANANCHI WA TANZANIA NA MASLAHI YAO". Hii, ingemsaidia Rais Samia kuwa na bunge imara lenye wabunge mahiri waliochaguliwa na wananchi (Sio wa wabunge walio chaguliwa na Magufuli) kuisaidia, kuishauri na kuisimamia serikali yake vizuri.

2) Kuvunja "BARAZA LA MAWAZIRI LOTE" na kuchagua baraza jipya lenye maono na uwajibikaji. Baraza lililopo amelifanyia baadhi ya mabadiliko mazuri, na ninayotegemea baada ya muda kidogo atalifanyia mabadiliko tena, ila kutokana na kutokua na wabunge mahiri nina amini imempelekea kushindwa kubadili baadhi ya Mawaziri kwa kukosa wabunge mahiri wenye sifa za kushika nyadhifa hizo.

Baraza la Mawaziri lililopo, likiongozwa na Waziri Mkuu, ndio Baraza lililovunja rekodi ya matumizi mabaya ya hela za wananchi kuwahi kutokea tangu tumepata uhuru wa nchi hii.

3) kuweka wazi "GHARAMA NA NYARAKA ZOTE ZA UNUNUZI WA NDEGE, SGR, STIEGLER'S GORGE, PROJECT ZA KIWANJA CHA NDEGE CHATO, FLYOVER", ili raia na wabunge waweze kuzichambua kwa uwazi. Hii itasaidia kuondoa minong'ono ya kisiasa, pia itamsaidia kumweka mahali salama kisiasa Rais wetu mpendwa (Atapata stara ya kutokutolewa maneno ya hasara, madeni na ufisadi uliofanyika baada ya yeye kuondoka - Atadhihirisha madudu hayo hakufanya yeye, japo hilo liko wazi).

4) Kuwashirikisha "WANASIASA WA UPINZANI NA WASOMI MAHIRI". kwa ushauri kwenye mambo ambayo serikali inataka kuyafanya. Tukumbuke hayati Rais Mkapa alivyosema katika kitabu chake "My Life, My Purpose" kwamba upinzani bungeni ni sawa na "JICHO LA PILI LA SERIKALI (Mimi nina amini Upinzani ni jicho la pili kweli, bila upinzani serikali inakua na jicho moja tu, kwa lugha fasaha serikali inakua Kilema/Chongo/Ngurumo - Hii imedhihirishwa na Utawala Wa Magufuli uliokuwa Kilema/Chongo/Ngurumo)".

5) Kuwawajibisha kimaadili na kisheria "WAO KAMA WAO PERSONALY" viongozi wote wa umma waliofanya ufisadi katika Wizara/Ofisi Zao. Wapelekwe kwenye Baraza La Maadili wajieleze na TAKUKURU wapepeleze personal mali wanazo miliki sambamba na hasara walioitia serikali. Wawajibishwe.

6) Kuboresha "MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA NA MATAIFA MENGINE/WADHAMINI", mataifa tulioyakosea kama Kenya na mengineyo, tuyaombe radhi na tuanze ukurasa mpya. Wadhamini waliokua wakitusaidia kwa misaada ya fedha za kusimamia uchaguzi na madawa na kadhalika, pia tuwaombe radhi. Kuomba radhi unapokosea sio udhaifu ni ujasiri.

7) Waliodhulumiwa na kuvunjiwa "MIKATABA YA KAZI/AJIRA/BIASHARA/PROJECT" kienyeji na utawala wa magufuli, wapi ni raia/wafanyakazi wa umma/makampuni/taasisi/nchi pia tuwaombe radhi ili wasije kutuwajibisha na kutudai fidia. Zipo kesi katika mahakama za kimataifa ambazo tumeshtakiwa kwa kukurupuka kwetu, tunaweza kufanya nao suluhu kabla ya kupewa hukumu zitakazo tuzamisha kitaifa, pengine wakatusamehe na kuachana na kesi hizo.

8) KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA. Ili kuepusha kuja tena kutawaliwa na Utawala wa Kikoloni & Utumwa (The Colonialism & Slavery Of Magufuli Era).

Si maanishi tuifungue nchi iwe shamba la bibi kwa mataifa ya nje, hapana, ninacho maanisha tuweke sawa kasoro zetu na mataifa mengine.


Ahsante,
 
1.Kuunda timu ya uchunguzi wa watu wote
Waliopotea. Ben Saanane na AZORY NA wengine na tupate muafaka kama waliuwawa
Tujue walizikwa wapi
Ndugu zao wafanye ibada ya kuzika tufunge ukurasa

2.iundwe timu ya wataalam kutathmini miradi
Ya JPM ..best way ya kuimaliza Ile ya manufaa Tu kama sgr na bandari ya Bagamoyo..

Kuhakikisha uchaguzi huru na haki wa serikali za mitaa ..na chaguzi zitakazo kuja
 
Mimi kitu ninachotamani kifanyike kwa lazima
1.BIMA NAFUU YA AFYA
2.AJIRA (Hata mshahara kidogo kidogo)

NB: mimi sijui SIASA lakini hayo mawili ni muhimu kuliko yooooote Tanzania/africa
 
Mh!
 
Salam kwa jina la jamhuri ya muungano, topic inajieleza, tumeshaona sifa na kashfa kede lundo, sasa zamu ya kuonyesha utu.
 
Muda muafaka wa kusema umefika ama yaliyo tukera au tulivyo yafurahia. Tutafika nyongo tuone.

Wengi wamechangia vizuri sana ufisadi wa Dkt. Magufuli na kwa upeo wa akili zao na muono wao, wako sahihi.

Hili lilikuwa fisadi sana na lilitulipa katika Ufisadi wake yafuatayo:

1) Miji yote ilipata bahati ya kurekebisha barabara za lami mijini.
2) Kuboresha vituo vya afya nchi nzima, sasa mama weka vivenda kazi na madawa.
3) Kurudisha Utendaji wa uwajibikaji katika utumishi wa Umma.
4) Kutamalaki kwa Usalama, Usalama, Usalama, Usalama, Usalama.
5) miradi Mikubwa ya mkakati, umeme, reli, vituo vya usafiri Mikoa yote.
6) Malipo ya mishahara kila tarehe 23 ya mwezi.
7) Kutengeneza mfumo wa kuwa adabisha watumishi wa umma.
8) Ku repair barabara kubwa zote nchini.
9) Kurekebisha mfumo wa uwekezaji kwenye mali asili zetu hasa madini.

10) kuripair shule zote kongwe nchini.

Na mengine mengi.

Mama Samia tunaamini wewe mtu safi sana na bora, umejifundisha mengi kwa fisadi mkubwa kwa hiyo tunakuomba uyafanye makubwa kuliko fisadi Mwendazake.

Ukifanya haya machache nilio andika chini pekee itafanya tuuchukie zaidi Ufisadi wa Mwendazake zake.

Wapeleke semina wabunge wote na waelekeze wafanye kinyume na ufisadi uliokithiri wa Mwenda zake ili nchi iende mbele.

Wabague Wasukuma na kanda nzima ya Magharibi kwa kuwa hawana maana tena kwa nchi yetu kwa kuwa fisadi lao limekwisha enda zake.

Sioni sababu ya kuwaomba kura kanda ya Magharibi( Mara Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Tabora, Rukwa, Katavi na Kigoma) kwa kuwa sioni maana yao kwa utawala wa leo hata uchaguzi ujao, Magufuli Mwendazake ilikuwa bahati mbaya tuu.

Anazisha kitengo cha mitandao na tutakusaidia maoni ya kutawala vyema, kwa sababu hata miaka yote ya nyuma, tumekuwa tukiielezea Ubaya wa Mwendazake Magufuli.

Na usiwa jengee nyumba família ya Magufuli kwa kuwa nyumba hujengewa Rais na sio família yake.
Na sio vibaya nyumba ya Mwinyi na Kikwete zika taifishwa, zili jenga kwa ufisadi wa Mwendazake. Kwani sasa hivi Mwinyi na Kikwete wanalala njee?

Hakikisha unafungulia Mbwa kuhusu usalama, tunakuomba Kibiti I rudi haraka. Tumeanza kuimiss ilikuwa hali ile, ilikuwa ikitupatia raha.

Madawa ya kulevya yalitupatia maisha bora na kuimarisha afya za vijana wetu. Pamoja na hayo pesa ilikuwepo kila mahala.

Halalisha wizi wa mali ya uma ili tusisutane kila mtawala akiondoka madarakani, tulimsakama Kikwete kumbe ni kitu cha kawaida.

Ondoa msisitizo wa Kiswahili katika nchi zetu, na utumishi wa umma. Sio lugha ya lazima.

Ikulu ipo Dar es Salaam na ya Dodoma in manufaa gani?

SIMAMISHA KUHIFADHI FEDHA.

Turuhusu uvuvi kama siku za nyumba kwa nini tujibane bane wakati Bahari, Maziwa, mito na mabaya na samaki ni wa kwetu. Kuvua tuu kwa kwenda mbele?.

Fukuza Machinga wote mijini, wapatiwe sehemu ya kufanya biashara ikishindikana wewe Fukuza tuu kwani kabla ya Mwendazake waliishije.

Wizi wa bandarini ni kitu tulikwisha kuzoea miaka nenda rudi, hatuna maumivu tena hata kama hali hiyo ikirudi kwa nguvu.

Sio lazima baba na mama wafanye kazi ili watoto waishi, peleka maendeleo Unguja na Pamba kwa budgeting yetu, ni watoto wetu hao na wala usihofu.

Usihofu Mama yetu, CCM ilichoka vibaya wakati wa Utawala wa Kikwete na bado Wewe na Mwendazake Milishinda.

Jumapili njema.
 
Kwani vipi tena,maji yamezidi unga ama.
 
Hata mtoto wa chekechea ukimuambia Magufuli fisadi atakucheka!Acheni ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…