Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Binafsi nafurahia sana utawala wa Rais wetu mpendwa SAMIA suluhu hasani, humuoni sana mitaani, waziri mkuu anafanya kwa niaba ya Rais

Hatembei na maburungutu ya hela na kugawa hovyo kupitia mlango wa juu wa gari..
Haya tushakusikia na udaku wako!
 
Mh Rais Wetu

Tunakuombea amani ya Bwana.

Tunaamini sasa umeshatulia vizuri na unaendelea na Kazi zako.

Mama tunashukuru Mungu kwa ajili yako na nchi yetu.Ila Tunakuomba Mambo Makuu Mawili.

1. Sikiliza Kilio cha Wafanyakazi wa kada zote kwa maana ya sekta binafsi na wa Serikalini.

SERIKALINI kwa mfano mbali na kilio cha mishahara Midogo, kulikua na wimbi kubwa la unyanyasaji, udhalilishaji,kufunguliwa kesi kubwa kubwa zisizo na dhamana ili kukomoana.

Wapo watumishi waliohamishiwa kutoka ofisi moja kwenda nyingine ili tu mambo flani yafanyike maana walionekana kikwazo.

Wapo waliodhalilishwa sana na wote wanategemea kauli yako iwaamushe mioyo yako kama ulivyowatia matumaini wafanyabiashara.

Iliyokuwa ofisi yako imetuhumiwa kutesa watumishi. Kiongozi mmoja wa Juu ambae sasa imemhamisha alituhumiwa sana kwa kuwanyanyasa Wafanyakazi huku akiwa na kundi lake. wakuu mbali mbali wa mashirika wametuhumiwa kutesa na kuwaumiza watumishi, tunaomba Mama wambie sasa imetosha na kama mtu akimtengenezea mtumishi kesi ikagundulika uongo achukuliwe hatua kali.

2. Jambo la pili ni kupanda vyeo na madaraja hili ni donda ndugu...Serikalini mtu anakaa miaka hapandishwi cheo hii imekatisha tamaa ingawa tumeona mh Mchengerwa anaenda nalo vizuri.

MUNGU AKUBARIKI.
 
Morning Mama.

A. CDA walikuwa corrupt sana. Waliumiza watu wengi sana. Wafanyakazi wa CDA wengi walijimegea viwanja na hata sasa kama Lukuvi akiendelea na idea ya serikali ya ku-link NIDA na umiliki wa viwanja nchi nzima, tutaona hata yasiyotizamwa. Viwanja ambavyo havijalipiwa na ambavyo ni hewa vitauzwa upya na serikali kupata mapato mengi. I always believe kuwa sekta ya ardhi alone can fund Rwanda's and Burundi's annual budgets. Bado tunacheza.

However, nimeona mabadiliko makubwa sana ya kuzuia mianya ya rushwa baada ya katibu mkuu mpya kuingia pale wizarani. Namaanisha yule Dada. Kanafanya mambo kisayansi na siyo mwizi. We need to see such commitments kwenye kila technical desks za wizara and public institutions. JPM aliivunja CDA. Jiji likachukua yale ya CDA. Ulikuwa ni uamuzi mzuri. Bahati mbaya, naiona operational inefficiency ambayo italeta shida. Wamezidiwa. Look at this below.

B. Pale nje ya ofisi za jiji kuna madirisha ya kulipia ambayo yana shida kubwa tatu. Moja ni "network kukatika katika" na mbili ni foleni kubwa sana na tatu ni madirisha kuwa machache kulinganisha na the growing needs ya ardhi Dodoma. Dodoma kwa sasa ni kubwa na mahitaji ya ardhi yamekuwa makubwa. Angalia kituko kingine.

C. Pale nje ya jiji imefunguliwa ofisi ambayo inahusika na mambo ya ardhi. Ofisi ni kubwa na ina wafanyakazi wengi tena vijana ambao look energetic. However, ili uhudumiwe kwenye hiyo ofisi, unatakiwa kupata namba maalum. Hata hivyo, kwa siku zinatolewa namba kwa watu 137 tu. Listen Mama. Wakija wananchi 600 kwa Siku, wananchi 463 hawatahudumiwa siku hiyo maana kadi zitakuwa zimeisha. Yaani kwa siku wale watu wanasema wanahudumia watu 137 tu. Hii inafanya watu wafike pale alfajiri. Ikifika 6am plus kadi zinakuwa zimeisha na mnaambiwa njooni kesho wengine mgombanie namba.

Mama, you worked in an international NGO before joining politics, hivi ukiambiwa hiki kituko na ukakumbuka ulipokuwa employee tena miaka hiyo si utahairisha hotuba yako leo? This is not only operational inefficiency, but highest level of stupidity in delivering public service. Naomba nitoe advice.

D. Ardhi pamoja na relevant infrastructures kwa Dodoma need your special eye. Dodoma is growing. Kuna sehemu jiji limepasahau kabisa mfano mzuri ni baada ya soko la ndugai kuelekea huko kwako. Kama watu wanajipangia kuhudumia 137 people a day bila kujali huyo aliyekuja asubuhi na mapema na kukosa namba ana hali gani, hawawezi ku-manage the growing needs of the city especially a strategic area kama kuanzia stand kwenda chamwino ikulu.

We need to see investments in these areas particularly the infrastructures ili kuongeza mapato na kuchochea enhanced business environment. Ili kuongeza kasi na kumanage growth, naomba Jiji lipunguziwe majukumu lest litakufa na tutapoteza pesa and opportunities. Kuanzia stand na kuendelea mbele hadi leaving room kwako naomba iwe ni Manispaa ya chamwino. Teua a visionary leader ili aibadilishe hiyo municipal in a year. Mjengee miundombinu tu. In a year you will see changes.

All the best Mama.
 
Kama maandalizi yalikua bado kwanini walikimbilia kuhamia huko?

Hapaeleweki hapo nusu jangwa

Itakuja kutokea mtawala atakua anaiendesha zaidi serikali akiwa Daresalam
 
Nasijuwi wamezingatia ratio ipii?

Afisa mmoja anatakiwa kuhudumiya watu wangapi?
 
Badala ya kuongelea namna ya kuboresha technolojia wewe unaongelea kuongeza matumizi, Dodoma ina ukubwa gani wa kutisha?
 
Morning Mama.

A. CDA walikuwa corrupt sana. Waliumiza watu wengi sana. Wafanyakazi wa CDA wengi walijimegea viwanja na hata sasa kama Lukuvi akiendelea na idea ya serikali ya ku-link NIDA na umiliki wa viwanja nchi nzima, tutaona hata yasiyotizamwa...
Una mawazo mazuri, ila umekizungumzia hicho kijiji cha Dodoma utadhani ni bonge la jiji. Halafu huo uandishi wako kwa mtu anayejua kiingereza au kiswahili tu, hawezi kuelewa unaoongea nini. Jirekebishe tafadhali.
 
Back
Top Bottom