Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Nimeona mama akihangaika na haya ya huku mitandaoni; nikuombe mama haya ya mitandaoni haya yatakupotezea sana targets ulizo jiwekea na serikali yako.

Haya yaache huku huku hakuna sababu ya kuhangaika kuyajibu kitaasisi, mitandaoni kuna upuuzi mwingi sana ukisema uanze kuhangaika nayo utajikuta una mengi ya kuyajibia kuliko hata kutekeleza yale ya kiuraisi.

Nikuombe haya achana nayo pita yasome ili upate mwanga lakini usihangaike nayo maana maneno ya mitandaoni ni mengi mengi kweli kweli nikuombe sanaa.
 
Habarini Wadau

Tunashukuru serikali kwa wazo linalofanyiwa kazi la kupandisha Madaraja au Vyeo watumishi wa Umma. Lakini hii hoja ya mishahara kupanda ni ya kuangaliwa na inapaswa tushauriane vizuri.​

Serikali inaweza kupandisha mishahara/vyeo kwa wafanyakazi wake lakini kuna mahali mambo hayapo sawa. Mathalani tangu mwaka 2012 mtu hajawahi kabisa kupanda DARAJA mpaka 2021 almost miaka kumi (10). Lakini watumishi hao hao kwenye HALMASHAURI nyingine wameshapandishwa na wapo kwenye madaraja/vyeo husika. Sasa mnakuta mnatofautiana ilihali mliajiriwa pamoja na mna sifa zinazofanana za kiutumishi na hata kielimu.​


Ushauri: Nadhani busara imuongoze Rais kuwa kila mfanyakazi awekwe kwenye DARAJA analostaili kulingana na muda aliofanya kazi provided hakuwa na barua za makosa au hatua za kinidhamu. Hili litasaidia sana kutupa stahiki yetu hasa kama mseleleko wa madaraja/cheo utatumika maana sisi watumishi tulitumika kwa nafasi yetu ila mwajiri ndio hakutekeleza wajibu wake.

Naamini hii tofauti ya kimadaraja su vyeo kihalmashauri litakuwa limeisha kabisa​

Nawasilisha
 
Sahihi kabisa.

Mama SASHA akisema kila analosikia mtandaoni atazidi kuwaapa kichwa wanamitandao kwamba "anhaa kumbe anasoma eee" watazidi kutia maneno ya kumuumiza mama yetu.

Mama yetu ya mitandaoni yasoma na uyawache kwenye hotuba zako jifanye kama huyaoni usiyazungumzie kabisa

,wengine wanakuzushia unajaza waislamu na wazenji ili wakutie upepo uhamaki kwa sababu wanajua unayasoma,sasa yapuuzie mama.

Lakini pia watz tushajua kwamba yanayoongelewa mitandaoni ni propaganda,hivyo sisi tunayaacha huku huku.

Lakini mama ukiyazungumzia huko kwenye hotuba yatazidi kutiliwa nguvu kwamba pengine kuna ukweli fulani.

Uongo hupotezwa kwa kunyamaziwa,na ukweli hupotezwa kwa kukanushwa.
 
Unapoteza tu muda wako Kumwambia (Kumshauri) hivi (haya) kwani hakuna Mtu ambaye si tu anapenda bali pia huwa hata 'anakesha' humu Mitandaoni kama huyu (huyo) unayemshauri hapa.

Usisahau pia kuwa Asili ya Watu wa Pwani (tena hasa hasa wa Jinsia) yake kupenda Umbeya (Ushambenga) ni moja ya 'Tunu' yao walioachiwa na Mabibi zao.
 
Hawezi kuacha kuingia mitandaoni maana huku ndio bunge la kweli la wananchi. Ni jinsi gani anadeal na haya mambo ya huku mitandaoni, hilo linategemea na utashi wake. Ila kwa kiongozi yoyote anayetaka kufahamu ukweli wa watu wake, kwa sasa mitandaoni ndio sehemu sahihi ya kupata ukweli huo.
 
Kuwapandishia mishahara Watumishi wa umma ni sahihi kabisa lakini tukumbuke kwamba ukishapandisha mishahara tu kwa hao Watumishi basi maisha pia hubadulika kwa kuwa na ongezeko la bei la bidhaa na huduma mbalimbali ambapo hata Mfanyakazi wa sekta binafsi ambaye hajaongezewa mshahara anaathirika. Kwa mantiki hiyo basi ni vyema kabisa PAYE na ipungue ili kuleta walau uwiano kwa kiasi fulani.
 
Kuna ajira mpya 2012 ambaye bado hajapanda hadi leo?

Mimi ninachojua ambao hawajapanda ni ajira 2014.
 
Kupandishwa madaraja kuna vigenzo na issue siyo miaka uliyokaa kazini, mathalani wewe ni mtoro, ulisimamishwa kazi, mtovu wa nidhamu unataka upandishwe tu? piga kazi utapandishwa bila shida mama hana tatizo.
 
Hawezi kuacha kuingia mitandaoni maana huku ndio bunge la kweli la wananchi. Ni jinsi gani anadeal na haya mambo ya huku mitandaoni, hilo linategemea na utashi wake. Ila kwa kiongozi yoyote anayetaka kufahamu ukweli wa watu wake, kwa sasa mitandaoni ndio sehemu sahihi ya kupata ukweli huo.
Sahihi kabisa.
 
Serikali lazima kusikiza na kujibu narrative ya mitandaoni. Narrative ya mitandao inayo nguvu ya kujenga positive au negative perception ya mwananchi kuihusu serikali.
 
Back
Top Bottom