Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu.
Samia ameapishwa Machi 19, 2021 kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 baada ya Rais aliyekuwapo, John Magufuli kufariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.
Rais Samia mara baada ya kuapishwa jana alilihutubia taifa na kuwataka Watanzania kuzika tofauti zao na kuwa wamoja, kudumisha amani kwakuwa si wakati wa kutizama yaliyopita, bali ni wakati wa kutazama yajayo.
"Si wakati wa kunyoosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele. Ni wakati wa kufutana machozi na kufarijiana. Ni wakati wa kuweka nguvu za pamoja ili kujenga Tanzania mpya…” alisema Rais Samia.
Kwa mkutadha huo Rais Samia atakabiliwa na mambo saba mbele yake, Mambo haya ni kama ifuatavyo.
1. Kupanga safu ya watakaomsaidia ili kutimiza ndoto na maono yake kama walivyofanya watangulizi wake. Lazima atafute safu ya uongozi atakayoshabihiana nayo. Katika nchi yetu yeye ni mtu wa juu kabisa mwenye uamuzi. Dhamira yake na mwelekeo wake unategemea safu hii.
2. Kuenzi miradi, mipango na mikakati mizuri ya kimaendeleo iliyoanzishwa na hayati Magufuli. Miongoni mwa mambo anayotazamiwa kuyaendeleza kwa kasi ni ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme la Nyerere, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ujenzi wa miundombinu ya barabara.
3. Kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano ulitetereka kutokana na tofauti za kisiasa, kidini na kimaeneo.
4. Kufufua Mchakoto wa Katiba Mpya
5. Kufugua misingi ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao hawajaongezewa mishahara tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani 2015.
6. Kuimarisha misingi ya utawala bora uliotikiswa na mfano ni baadhi vitendo vya viongozi kutoa amri za kukamatwa na kuswekwa ndani watu bila sababu za msingi. Kuna upungufu wa kiutawala ambao labda pengine sasa Rais Samia anatakiwa akae chini na kutathmini na kuboresha ili utawala wake uwe bora zaidi, hasa katika utawala bora na mambo ya demokrasia.
7. Kurejesha imani kwa wafanyabiashara wanaolalamikia mfumo wa kodi kuwa unaua biashara. Kuboresha mazingira rafiki ya biashara na ulipaji kodi.
8. Kuendeleza mapambano ya Rushwa na nidhamu kazini.