Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Kama itapendeza baada ya shughuli zote za mazishi ya Mpendwa wetu aliyekuwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli basi kwa heshima na taadhima tunaiomba Serikali iagize chanjo ya corona ili wananchi wapate kuchanjwa. Ikumbukwe kuwa majirani zetu tayari wameagiza chanjo na sisi tusione aibu kuagiza chanjo. Serikali iliyopo madarakani imewekwa na wananchi na hivyo mnatakiwa kutusikiliza.
Usituingize mkenge!! Hii chanjo bado iko kwenye majaribio! Tujipe muda wa kuona hao waliochanjwa kama miaka miwili hivi! Hata baadhi ya nchi za ulaya zimesitisha hata baada ya kushauriwa ziendelee na chanjo!! Hasira ya makaburu na mabeberu iko hapo!

Mama SAMIA (Rais) chonde chonde, tujipe muda! Si hatari kivile kama wanavyofanya tuamini!! Watatumaliza hawa tukiwapa mwanya!
 
Huyu Mama miluzi itamchanganya sana aachwe achukue ushauri wa Mzee Mwinyi wa kurudisha mzunguko wa fedha.

Kama tulivyoshuhudia hali ya Watanzania wakiomboleza bila kula na hatimae wengine wanaishia kudondoka.

Wengine walikuwa wanaila zaidi kutokana na njaa iliyotalamaki.

Mzee Kikwete na Mzee Mwinyi mshaurini Mama Samia awaombe Watanzania waliohamishia Mitaji yao nje ya Nchi kwa kuogopa matamko.

Fedha irudi kitaa sio siasa za kijinga za kukaa na njaa

Siasa safi ni Ugali mezani Vitumbua kinywani
 
Mama Bi SAMIA SULUHU (Rais), mtu asikupangie, Taifa lolote lisikupangie! Mungu amekuchagua wewe!! Hajakuchagua leo!! Ila leo ndio imedhihirika kuwa Mungu alikuchagua.

Amini kuwa Mungu amekuandaa, amekupika ukaiva vilivyo!! Sikiliza ushauri lakini usishinikizwe kukubali ushauri wowote maana mwisho wa siku wewe ndiwe utakayewajibika kwa Mungu kwanza, pili kwa watanzania ambao umepewa kuwaongoza.

Usiogope Mungu yu pamoja nawe na watanzania wote wapo pamoja nawe!! Maadui wa Tanzania waliokuwa wamebanwa vilivyo na Magufuli wana matumaini potofu ya kupata mpenyo sasa!! Mama wakatishe tamaa! Waambie hapa Kazi tu!! Kazi bado haijaisha!
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu.

Samia ameapishwa Machi 19, 2021 kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 baada ya Rais aliyekuwapo, John Magufuli kufariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.

Rais Samia mara baada ya kuapishwa jana alilihutubia taifa na kuwataka Watanzania kuzika tofauti zao na kuwa wamoja, kudumisha amani kwakuwa si wakati wa kutizama yaliyopita, bali ni wakati wa kutazama yajayo.

"Si wakati wa kunyoosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele. Ni wakati wa kufutana machozi na kufarijiana. Ni wakati wa kuweka nguvu za pamoja ili kujenga Tanzania mpya…” alisema Rais Samia.

Kwa mkutadha huo Rais Samia atakabiliwa na mambo saba mbele yake, Mambo haya ni kama ifuatavyo.

1. Kupanga safu ya watakaomsaidia ili kutimiza ndoto na maono yake kama walivyofanya watangulizi wake. Lazima atafute safu ya uongozi atakayoshabihiana nayo. Katika nchi yetu yeye ni mtu wa juu kabisa mwenye uamuzi. Dhamira yake na mwelekeo wake unategemea safu hii.

2. Kuenzi miradi, mipango na mikakati mizuri ya kimaendeleo iliyoanzishwa na hayati Magufuli. Miongoni mwa mambo anayotazamiwa kuyaendeleza kwa kasi ni ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme la Nyerere, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

3. Kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano ulitetereka kutokana na tofauti za kisiasa, kidini na kimaeneo.

4. Kufufua Mchakoto wa Katiba Mpya

5. Kufugua misingi ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao hawajaongezewa mishahara tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani 2015.

6. Kuimarisha misingi ya utawala bora uliotikiswa na mfano ni baadhi vitendo vya viongozi kutoa amri za kukamatwa na kuswekwa ndani watu bila sababu za msingi. Kuna upungufu wa kiutawala ambao labda pengine sasa Rais Samia anatakiwa akae chini na kutathmini na kuboresha ili utawala wake uwe bora zaidi, hasa katika utawala bora na mambo ya demokrasia.

7. Kurejesha imani kwa wafanyabiashara wanaolalamikia mfumo wa kodi kuwa unaua biashara. Kuboresha mazingira rafiki ya biashara na ulipaji kodi.

8. Kuendeleza mapambano ya Rushwa na nidhamu kazini.
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu...
Umezunguka sana.
Kikubwa ni KATIBA MPYAA TUU.
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu....
Kwa ufupi kutokana na maoni yangu katika medani ya kisiasa za ndani na nje afuate mfumo wa mzee Kikwete na katika usimamizi wa Serikali na chama afuate mfumo wa mzee wetu Magufuli.
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu....
Katiba mpya ni takwa la wapinzani kupata political mileage, kiuhalisia hatuhitaji katiba mpya.
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu...
Kuna baadhi ya vitu umetaja hapo ndio upuuzi ambao ulifanyika awamu zilizopita na kutufikisha tulipokua tumekwama...
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu.

Samia ameapishwa Machi 19, 2021 kushika wadhifa huo kwa mujibu wa Ibara ya 37(5) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 baada ya Rais aliyekuwapo, John Magufuli kufariki dunia kwa ugonjwa wa moyo Machi 17, 2021.

Rais Samia mara baada ya kuapishwa jana alilihutubia taifa na kuwataka Watanzania kuzika tofauti zao na kuwa wamoja, kudumisha amani kwakuwa si wakati wa kutizama yaliyopita, bali ni wakati wa kutazama yajayo.

"Si wakati wa kunyoosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele. Ni wakati wa kufutana machozi na kufarijiana. Ni wakati wa kuweka nguvu za pamoja ili kujenga Tanzania mpya…” alisema Rais Samia.

Kwa mkutadha huo Rais Samia atakabiliwa na mambo saba mbele yake, Mambo haya ni kama ifuatavyo.

1. Kupanga safu ya watakaomsaidia ili kutimiza ndoto na maono yake kama walivyofanya watangulizi wake. Lazima atafute safu ya uongozi atakayoshabihiana nayo. Katika nchi yetu yeye ni mtu wa juu kabisa mwenye uamuzi. Dhamira yake na mwelekeo wake unategemea safu hii.

2. Kuenzi miradi, mipango na mikakati mizuri ya kimaendeleo iliyoanzishwa na hayati Magufuli. Miongoni mwa mambo anayotazamiwa kuyaendeleza kwa kasi ni ujenzi wa bwawa kubwa la kufua umeme la Nyerere, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

3. Kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano ulitetereka kutokana na tofauti za kisiasa, kidini na kimaeneo.

4. Kufufua Mchakoto wa Katiba Mpya

5. Kufugua misingi ya demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao hawajaongezewa mishahara tangu awamu ya tano ilipoingia madarakani 2015.

6. Kuimarisha misingi ya utawala bora uliotikiswa na mfano ni baadhi vitendo vya viongozi kutoa amri za kukamatwa na kuswekwa ndani watu bila sababu za msingi. Kuna upungufu wa kiutawala ambao labda pengine sasa Rais Samia anatakiwa akae chini na kutathmini na kuboresha ili utawala wake uwe bora zaidi, hasa katika utawala bora na mambo ya demokrasia.

7. Kurejesha imani kwa wafanyabiashara wanaolalamikia mfumo wa kodi kuwa unaua biashara. Kuboresha mazingira rafiki ya biashara na ulipaji kodi.

8. Kuendeleza mapambano ya Rushwa na nidhamu kazini.
Yote hayo sawa Asisahau Ajira kwa vijana Graduate pia asiwasahau
 
Samia Suluhu Hassan sasa ndiye Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini yapo mambo tisa yanayomsubiri ayapatie ufumbuzi katika siku 1,691 atakazohudumu madarakani kutoka sasa hadi mwaka 2025 utakapofanyika uchaguzi mkuu..
Umeacha moja la muhimu sana, nalo ni "Kujitoa sadaka" kwa manufaa ya Nchi. Bila kuji sacrifice, kwa Afrika ni ngumu sana kulinda rasilimali za Nchi kwa manufaa ya Wananchi.

Tukumbuke, mpaka sasa NYANI waliokuwa wanakula mazao shambani, wamejipanga sawasawa kwa kazi hiyo.
 
Kwa kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo ilivyokuwa inazidi kudhihirika kuwa Rais Magufuli ni mzalendo kweli kweli na amejitoa mzima mzima kupambania maendeleo ya nchi yetu.

Katikati ya matumaini makubwa namna hiyo taa kubwa iliyokuwa inaangaza imezimika ghafla! Ni vigumu kuamini lakini ndivyo ilivyotokea! Kwa maneno mengine watanzania tumenyang'anywa tonge mdomoni wakati ndo kwanza tumeanza kufurahia utamu wake na kujiandaa kumeza.

Lakini Mungu ni mwema! Mungu ametupa Joshua wetu, (Mama Bi Salma Suluhu). Mungu hakosei. Kama ambavyo ilikuwa ni vigumu kwa Wana wa Israel kumlinganisha Joshua na Musa, ndivyo itakavyokuwa vigumu kwa watanzania kumlinganisha Bi Samia Suluhu(Rais) na Magufuli!

Lakini katika mipango ya Mungu pamoja na ushujaa wa Musa lakini jukumu lake lilikuwa ni kuwatoa tu wana wa Israeli toka Misri utumwani lakini si kuwaingiza.

Wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi imiminikayo maziwa na asali!

Jukumu la kuwaingiza Wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi lilikuwa ni la Joshua mwana wa Nini! Hali kadhalika Jukumu la Rais Magufuli ilikuwa ni kututoa utumwani (mikono ya mabeberu iliyoshikilia uchumi wetu), kumbuka alivyofuta Sheria ya madini iliyokuwa ya kifisadi na kuweka Sheria mpya inayotoa mwanya wa kufanya marejeo ya mikataba ya madini ili watanzania wafaidike!

Kumbuka Magufuli alivyokataa kupokea amri ya kutushinikiza tufuate matakwa yao namna ya kushughulika na covid-19.
Magufuli amemaliza kwa ukamilifu ngwe yake!

Bi Samia Suluhu(Rais), umepokea kijiti usiogope! Jukumu lako ni kuwaingiza watanzania kwenye nchi ya ahadi! Mama utuvushe!! Mungu yu pamoja nawe utuvushe! Ndivyo Mungu alivyopanga! Paisha uchumi wetu! msingi umeshawekwa. Miradi mingi ya maendeleo uisimamie ikamilike! Watanzania tutakuunga mkono! Tutakuheshimu, Tunakupenda! TUNA IMANI NA Bi SAMIA SULUHU HASSAN (RAIS).

Watanzania tuna JAMBO LETU na Bi SAMIA SULUHU, nalo ni kutuingiza kwenye nchi ya ahadi! Watanzania tuchape Kazi! Tulipe kodi! Tuwafichue maadui wa ndani na nje! Mungu ametupa Joshua wetu, wala tusiogope!
Umenyang'anywa hilo tonge mdomoni na nani? Na shetani, au!! Mara ndani ya maelezo unasema ndiyo Mungu alivyo panga! Kufa kupo tu my friend. Ingawa sikatai kifo kinaleta maumivu makali kwa wanafamilia wa karibu na marehemu.

Yaani wote tuliopo hapa duniani, muda wetu ukifika tutakufa tu! Na kwa bahati nzuri Tanzania ni zaidi ya mtu yeyote yule. Hivyo tujipange kwa maisha mengine, na tusahau yaliyopita.
 
Back
Top Bottom