Mheshimiwa rais,
Vijana tuliohitimu vyuo toka mwaka 2015 tuna hali ngumu sana mtaani.
Hima,tunaomba utuangalie(sana) sisi vijana tuliohitimu vyuo toka mwaka 2015 kwani tunateseka katika nchi yetu wenyewe.
Kumbuka tumeandaliwa katika mazingira ya kutegemea kuajiriwa.
Lakini toka mwaka 2015 tumewekwa kando kwa sababu lukuki zikiwemo;
UHAKIKI WA WATUMISHI,KUJENGA MIUNDOMBINU KWANZA na KUUNDA UPYA MFUMO WA AJIRA.
Sasa mama,tunaomba katika utawala wako utupe jicho la kulia.
Halafu pia uone kama ni watoto wako hawa wanaohangaika.
Mungu amekuweka wewe kwenye urais kwa makusudi mengi likiwemo hili suala la ajira.
Basi tunaomba uteekeleze mipango ya Mungu.
NB: Ukimaliza hili,fumuafumua kitu kiitwacho "HESLB".Ni chukizo.