Kwanza nikupongeze madam President kwa kuwa Rais wetu , naona umeanza kupanga safu yako mpya itakayo fanya kazi na wewe safi sana, ila naomba nikupe ushauri kidogo si lazima uufanyie kazi ila kama utaona inafaa, tunapata ukakasi kdgo.
Awamu iliopita tumeona sekta binafsi ikiachwa sana kama yatima kumbe ndio inabeba watu wengi sana na kuongeza wigo wa kodi, sasa basi tunaomba rudisha heshima ya hii sekta, ntakupa mfano mmoja mdogo sana ambao hata hauhitaji phd,
kuna shirika kama TASAC hyu ni regulator wa shipping lines, kampuni za wakala wa forodha ( CLEARING/ FORWARDING) kazi zao ni kutoa mizigo na kusafirisha, iweje leo tena huyo tasac nae anatoa mizigo bandarini kazi ambazo zinafanywa tyr na CFA? tena anachukua kazi zao na kuijipangia mizigo yake, je huoni hapo kama kuna conflict of interest?je yeye nani ana mregulate?
Hya leo LATRA nae anunue mabasi yake ajipangie route kama moshi na arusha hakuna basi jingine kwenda route hyo, TCRA Nao wauze airtime na vocha basi !Nafhani ifike muda kurevised hizi sheria za haya mashirika hasa tasac.Tuwe na uwanja sawa wote isiwe mtu mmoja ana monopoly biashara tu, tasac iwepo ifanye kazi yake ya kuregulate tu.