Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushauri Mzuri Aifunge aisikie DuniaNimeona mama akihangaika na haya ya huku mitandaoni; nikuombe mama haya ya mitandaoni haya yatakupotezea sana targets ulizo jiwekea na serikali yako.
Haya yaache huku huku hakuna sababu ya kuhangaika kuyajibu kitaasisi, mitandaoni kuna upuuzi mwingi sana ukisema uanze kuhangaika nayo utajikuta una mengi ya kuyajibia kuliko hata kutekeleza yale ya kiuraisi.
Nikuombe haya achana nayo pita yasome ili upate mwanga lakini usihangaike nayo maana maneno ya mitandaoni ni mengi mengi kweli kweli nikuombe sanaa.
Labda umeme tuu lakini miradi mingine ni liabilities kwa nchiMagufuli huwezi kusema kuwa alifeli kiuchumi kwani aliamua kwa makusudi kujenga misingi ya uchumi kuja kuwa endelevu,
Unapojenga reli ya kisasa unatumia pesa nyingi leo lakini ndani ya miaka kadhaa mbeleni reli hiyo ni muhimu sana kwa kurahisisha uchumi huo huo.
Unapohangaikia umeme leo hii mpaka pesa nyingi zikatumika, unakuwa ukitengeneza mazingira ya upatikanaji wa umeme mwingi utakaoondoa kabisa tatizo la mgao wa mara kwa mara, ni nishati ikiwa ya bei ndogo moja kwa moja umesaidia ukuzaji wa uchumi.
JPM alijikuta analazimika kutengeneza ile hali itakayoukuza uchumi mbeleni. Hakuyafanya aliyoyafanya kwa nia ya kuukomoa uchumi kwa nia ya kuwakomoa watu fulani wachache, alijikuta analazimika kufanya maamuzi magumu yenye tija itakayokuja kuonekana siku za mbeleni.
Alilazimika kufufua shirika la ndege kwa kuzingatia umuhimu wake kiuchumi. Corona ikishakuwa imedhibitiwa na safari za ndege zikaanza tena duniani pote, shirika litasimama na faida zake tutaziona.
JPM alikuwa na matatizo yake kama vile kutotabirika, ni hasira zisizo na sababu wakati mwingine zikifanana na visasi lakini kwa ujumla alikuwa na lengo linalotazama miaka kadhaa mbele.
Liabilities in the short term but long term ni assets.Labda umeme tuu lakini miradi mingine ni liabilities kwa nchi
Na Wewe unarudi lini Kwenu Lilongwe?Usipaniki wala usiwe na lugha za jazba we kama hutaki Samia awe rais wako HAMA NCHI.
Fanya kwanza kauchunguzi utakuja kukubaliana na mimi.Kwa taarifa yako mitandaoni ni mtaani katika digital approach. Usidhani ukiingia mtandaoni basi unahama mtaani. Kwa kukusaidia tu, mtandaoni ni mtaa mkubwa.
Akipitishwa na CCM kugombea tena 2025 upo tayari kumchagua?Hujajua kwamba CCM iko makundi mawili? Hujaona huko bungeni wabunge wa CCM wakiparuana kuonyeshana upendo kwa JPM na wengine kwa SSH hadi mama akaingilia kati kwamba hao wawili ni "kitu kimoja" ??
Nifanye utafiti wa jambo ninalolijua? Huko mtaani kama watu wako kimya ni kwakuwa watu wako kwenye majukumu yao, na kipindi cha Magufuli watu walijazwa hofu, wakawa wako salama kusifia na sio kukosoa. Inawezekana unatembea na hiyo picha ya hofu, kisha unaleta hapa jukwaani kwamba ndio uhalisia. Toka nje ya box.Fanya kwanza kauchunguzi utakuja kukubaliana na mimi.
Achana na mambo ya Magufuli mkuu ndio maana nikakwambia ufanye uchunguzi upate picha halisi huko mitaani, kwahiyo mkuu unataka kusema inawezekana wale waliyokuwa wanatandika kanga kwenye msafara wa kumuaga Magufuli miongoni mwao ni member wa JF ambao walifanya vile vya hofu?Nifanye utafiti wa jambo ninalolijua? Huko mtaani kama watu wako kimya ni kwakuwa watu wako kwenye majukumu yao, na kipindi cha Magufuli watu walijazwa hofu, wakawa wako salama kusifia na sio kukosoa. Inawezekana unatembea na hiyo picha ya hofu, kisha unaleta hapa jukwaani kwamba ndio uhalisia. Toka nje ya box.
Achana na mambo ya Magufuli mkuu ndio maana nikakwambia ufanye uchunguzi upate picha halisi huko mitaani, kwahiyo mkuu unataka kusema inawezekana wale waliyokuwa wanatandika kanga kwenye msafara wa kumuaga Magufuli miongoni mwao ni member wa JF ambao walifanya vile vya hofu?
Boksi uliloingia sio.. kuna moshi humoNifanye utafiti wa jambo ninalolijua? Huko mtaani kama watu wako kimya ni kwakuwa watu wako kwenye majukumu yao, na kipindi cha Magufuli watu walijazwa hofu, wakawa wako salama kusifia na sio kukosoa. Inawezekana unatembea na hiyo picha ya hofu, kisha unaleta hapa jukwaani kwamba ndio uhalisia. Toka nje ya box.
Najifukiza boss ili kupambana na covid.
Ishu iko hivi ni kwamba kwa mtazamo wa mitandaoni tusingetegemea kuwa huko mitaani kuna watu wa kufanya, sasa kufikiri kuwa waliyofurahia kifo chake ni zaidi ya ule umati tuliyokuwa tunauona kwenye kuaga sijui umetizama nini hadi uone kuna uwezekano huo? maana ni sawa na ile issue ya maandamano ya Lissu ambayo huku mitandaoni inaonesha watu wamechoka liwalo na liwe lazima waandamane ila siku ya tukio mtaani palikuwa hakuna dalili kabisa ya watu kuwa walikusudia kuandamana wako bize na mambo yao.Hao wa kutandika kanga mbona walikuwa wachache, ilitakiwa hata wavue nguo ili kuonyesha mapenzi yao kwake, lakini ukweli uko wazi. Na ungetaka kuujua ukweli waliokuwa wanashangilia kifo chake wangeachwa ndio ungepata mrejesho sahihi.
Tusubiri muda utasemaAkipitishwa na CCM kugombea tena 2025 upo tayari kumchagua?
I cannot say more!Hongera sana mama kwa kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.
Sasa baada ya Tanzania kupata uzoefu wa kutosha kutokana na awamu zake za uongozi, na tukaona mazuri na mapungufu yake, na wewe pia kupata uzoefu wa kutosha chini ya Mzee Magufuli ninakuomba haya yafuatayo:
Kwanza, usiturudishe nyuma tena. Awamu ya tano imetuonyesha nini maana ya uhuru na kujitegemea. Tanzania haina mjomba wala shangazi huko nje. Maendeleo ya watanzania yataletwa na watanzania wenyewe. Jukumu lako ni kutupanga, kutuvuvia, kutushawishi na kutuonyesha kwa mfano wako wewe mwenyewe kwamba inawezekana, tunaweza, tusonge mbele.
Pili, Mzee Magufuli kafa, lakini spirit yake haijafa. Ni askari aliyefia vitani akiwa mstari wa mbele, katika kupambania uhuru wetu na kujitegemea kwetu. Usije kufanya kosa kufanya mapungufu ya style ya Magufuli ya uongozi iwe kigezo cha wewe kubadili uelekeo wa nchi yetu, katika kujiamini na kuthubutu. Magufuli kafa lakini kaacha alama na kaacha spirit. Wenye hiyo spirit wamo ndani ya chama tawala, vyama vya upinzani, serikalini, sekta binafsi, na kwa wakulima na wafanyakazi. Hili ni jeshi kubwa sana usicheze nalo.
Tatu, tutakusikiliza kwa umakini, tutakuangalia sana mienendo yako, tutatizama sana namna zako kama zinaturudisha nyuma au zinatupeleka mbele. Nisiseme sana katika hili lakini itoshe tu kwamba spirit ya Mzee Magufuli haijafa. Tukiona tu dalili kwamba unakotupeleka siko hatutakuvumilia. Tushaonjeshwa uhuru hatutarudi tena kwenye utumwa. Tushaonjeshwa kujitegemea hatutarudi kwenye utegemezi tena.
Mwisho, Mungu akupe hekima ya kuongoza watu milioni 60, kwa akili na ujasiri. Ninaamini utatuvusha salama, karama ya uongozi unayo, itendee haki. Tegemea ushirikano wetu.
Pia soma: Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Ishu iko hivi ni kwamba kwa mtazamo wa mitandaoni tusingetegemea kuwa huko mitaani kuna watu wa kufanya, sasa kufikiri kuwa waliyofurahia kifo chake ni zaidi ya ule umati tuliyokuwa tunauona kwenye kuaga sijui umetizama nini hadi uone kuna uwezekano huo? maana ni sawa na ile issue ya maandamano ya Lissu ambayo huku mitandaoni inaonesha watu wamechoka liwalo na liwe lazima waandamane ila siku ya tukio mtaani palikuwa hakuna dalili kabisa ya watu kuwa walikusudia kuandamana wako bize na mambo yao.
Ndio nimekuuliza ni kipi kinachokufanya ufikiri kuwa kulikuwa na watu wengi waliyofurahia kifo cha Jiwe sawa na wale tuliyowaona wakimuaga Jiwe au zaidi ya wale? usikimbilie kwenye kificho cha kudai et walikatazwa kana kwamba unajua kwamba hao walikuwepo kweli kwa kiwango sawa na kile ila tatizo ni kukatazwa. Ndio maana nikatoa mfano wa maandamano ya Lissu ambayo kwa kutizama mitandaoni mlikuwa mnaonesha kabisa mpo teyari kwa lolote hamuogopi kitu wengine tukawa tunasubiri tuone hizo fujo zitakuaje kati yenu na jeshi la polisi ila kumbe mtaani hali iko tofauti kabisa na mitandaoni na ndio kile kilichotokea siku ya tukio mtaani watu wako bize na shughuli zao hawakuwa na mawazo ya kufanya maandamano hakukuwa kabisa na dalili za kwamba hawa watu walikuwa wamepanga kufanya maandamano.Akili ya Kawaida kabisa ingeweza kung'amua walioenda kuhudhuria msiba wa Magufuli, hawakuwa kwenye kitisho chochote cha kuuwawa na vyombo vya dola. Lakini waliotakiwa na Lisu kuandamana dhidi ya ushenzi kwenye uchaguzi ule, dhalimu alishaagiza vyombo vya dola viwaue, kwani hata kwenye huo uchaguzi bado aliagiza wengi kuuwawa, na waliuwawa kweli. Kwahiyo hapa unataka ulinganisho wa waliojitokeza kwa wingi wakiwa salama v/s ambao wangetoka kuandamana tayari kukiwa na amri ya kuuwawa.
Hivyo unatumia kipimo cha mazingira mawili tofauti kuonyesha kukubalika kwa dhalimu, wakati sio kipimo sahihi. Ni kweli waliofurahia kifo cha dhalimu wasingeweza kuwa wengi hadharani maana sio kitendo cha kawaida, na hakukuwa na kiwanja maalum cha wote waliofuhi kukutania ili uone wingi wao. Uwezekano wa waliofurahia kifo cha dhalimu na waliohuzunika ungeweza kuwa sawa, iwapo mazingira yote ya kuonyesha hisia za wahusika yangeachiwa. Huu ndio ukweli, hutaki meza sumu ufe.