kurlzawa
JF-Expert Member
- Jan 23, 2018
- 16,695
- 20,633
basi tuliza mshonoSipo serikalini wala chama
Sasa lia wewe[emoji382][emoji382][emoji382][emoji382][emoji382][emoji382]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
basi tuliza mshonoSipo serikalini wala chama
Sasa lia wewe[emoji382][emoji382][emoji382][emoji382][emoji382][emoji382]
ThibitishaJK pamoja na madhaifu yake lakini kazi yake inaonekana mpaka leo na hakuhitaji promotion kama mwendazake
Muulize mzee wakoThibitisha
Sina mzeeMuulize mzee wako
Wakuu Salaam,
Jana Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua kiwanda cha ushonaji cha Polisi kuna kauli alizitoa ambazo binafsi naona hakupaswa kuzitoa hasa kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye mtu mwenye nguvu na mamlaka na dhamana kubwa kabisa kwa sasa ndani ya JMT.
Jambo la kwanza alionyesha kushangazwa na vitendo vya matapeli wa kwenye mitandao ya simu ilhali sote tumesajiliwa kwa alama za vidole, jambo hili ni kweli linatushangaza wengi inakuaje hawakamatwi na kushughulikiwa kirahisi na bado wanaendelea, lakini yeye kwa nafasi na mamla aliyonayo alitakiwa kusimama kwenye zamu na nafasi yake kwanza kwa kuonyesha kutoridhishwa na kufutahishwa na jinsi watendaji wanavyoshughulikia swala hilo na pili atoe maelekezo ya nini anataka kuona kinafanyika tena haraka, lakini si kusema tu kuwa na yeye anashangaa, swali linabaki kuwa uongozi wake juu ya jambo hili ni upi?
Jambo la pili ni kuhusu kesi za kubambikiza, ameonyesha kuridhishwa na TAKUKURU kufuta kesi nyingi ambazo wameona hazikua sahihi, halafu akawaambia Polisi wajitafakari. Kama kiongozi liko tatizo ameliona ilikua jambo zuri angeonyesha alichokiona kisha atoe maelekezo ya utekelezaji, mfano ili kupunguza msongamano wa wafungwa JPM hakumwambia DPP ajitafakari bali alimwagiza aende magerezani aonane na mahabusi ili aone kesi za kufuta lakini pia azungumze na watu walio tayari kulipa fedha waachiwe. Hadi akafikia hatua ya kusema hayo ina maana yako mambo ambayo yeye ameyaona ambayo inawezekana watendaji wa maeneo husika either hawajayaona au wanayaona ni ya kawaida, sasa kiongozi kama mbeba maono jukumu lake ni kuwaonyesha yale anayoyaona na kuwaelekeza wayafanye.
Kama mimi kila siku ninapotoka nyumbani kwangu napita mlangoni kwa kupiga sarakasi, ukiniona ukashangaa kuwa nafanya kitu cha ajabu halafu ukaniambia nijitafakari wakati mimi naona ni kitu cha kawaida, usitegemee kuona mabadiliko.
Mama usishangae, kama sisi wananchi tusio na mamlaka, wewe ndiye kiongozi wetu uliye mbele yetu, toa maelekezo, kemea, amrisha mambo yaende.
kazi yake ipi?JK pamoja na madhaifu yake lakini kazi yake inaonekana mpaka leo na hakuhitaji promotion kama mwendazake
This is scientific!!Tatizo la mama anatoa kauli bila AMRI (of course amri halali, sio kama za Jiwe) na kutaka kitu fulani kifanyike na time frame. Mfano angelitaka Police wampe kesi zote walizonazo ndani ya say siku 7. Unampa mwanasheria anazipitia, unawashirikisha polisi??. Unatoa maamuzi unayoona ni ya haki.
Kama sheria haitendi haki inastahili kukanyagwa ama sivyo huwezi pata matokeomnapenda sana ubabe na kutozingatia sheria
Mfumo wa luku umegoma naomba unifikishie salaamMkuu uongozi sio kupayuka payuka kila kitu hadharani. Unauhakika hakuna hatua anazo chukua. Tatizo watu wamezoea drama za awamu iliyopita, na kutaka ziendelee. Acheni kufananisha uongozi wa mama na wa mwendazake, kila mmoja anaongoza kwa namna yake, kinachotakiwa ni matokeo. Tumwache mama atekeleze majukumu yake, muda aliokaa madarakani ni muda mfupi sana kuanza ku mhukumu.
... hoja nzuri! "Kushangaa kwa Rais" kimsingi sio kushangaa kwa kawaida kwa maana ya halisi ya neno hilo; kushangaa kwa Rais ni onyo na maelekezo kwa mwenye kufikiri. Waliozoea "stata mzuka" za "nimtumbue, nisimtumbueee"; "tumbuaaa" bila kushirikisha ubongo au kujali utawala wa sheria sembuse "haki ya kusikilizwa" wanadhani Rais anashangaa.Hapana yupo sahihi maana utawala wa sheria huanza kwanza kwa kusema na kuonya na baadae kiongozi anachukua hatua kama akiona hubadiliki.
Ni kweli kabisa, kila kauli huwa na amri au mamlaka inayoibeba. Nguvu ya hiyo mamlaka, ndio itategemea ni kwa kasi gani hiyo kauli itatekelezwa. Lakini kwa kauli kama unabembeleza watoto, sahau utekelezaji wenye tija.Tatizo la mama anatoa kauli bila AMRI (of course amri halali, sio kama za Jiwe) na kutaka kitu fulani kifanyike na time frame. Mfano angelitaka Police wampe kesi zote walizonazo ndani ya say siku 7. Unampa mwanasheria anazipitia, unawashirikisha polisi??. Unatoa maamuzi unayoona ni ya haki.